Rais Jakaya Kikwete ametamka hadharani kuwa foleni kubwa za magari jijini Dar es Salaam ni ishara tosha kuwa sera yake ya kuleta "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania" sasa imeanza kutoa matunda kwani Watanzania wengi zaidi wamemudu kununua magari chini ya uongozi wake.
Badala ya kukiri kuwa msongamano wa magari unaoleta athari kubwa kwenye uchumi wa nchi, unatokana na serikali yake kushindwa kuwekeza pesa kwenye miundombinu na kujenga fly-overs, Rais wetu mpendwa anasema kuwa foleni barabarani ni ishara ya neema.
Nalipongeza sana gazeti ya MAJIRA kwa kufanya umakini mkubwa na kuripoti habari hii.
Matamshi haya ya Rais yanadhihirisha jinsi alivyokuwa na upeo mdogo wa kufikiri na kuongoza nchi.
Kwa maana hiyo, anataka Watanzania wafurahie foleni au wavumilie tu kwani ndiyo matunda ya maisha bora hayo.
Yeye haoni kabisa kuwa foleni hizi ni ishara kuwa serikali yake imeshindwa kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo zaidi.
Barabara hizi zimejengwa tangu enzi za Mwalimu wakati population ya Dar ikiwa ni watu laki 5 tu. Leo Dar ina zaidi ya watu milioni 4 na miundombinu ni ile ile ya zamani.
Baada ya kutoa matamshi haya mazito. Rais Kikwete sasa tunaambiwa anaenda tena ulaya kwenye shopping spree.
Safari hii anaenda Spain kuwapongeza kwa kushinda kombe la dunia ili akapewe jezi na kupiga picha na kina David Villa, Puyol, Iniesta, Xavi, Torres na Cesc Fabregas.
Pia, atafanya mazungumzo tena na Rais wa Real Madrid ili awalete kina Jose Mourinho, Ronaldo, etc waje kutalii Tanzania kwa pesa zetu sisi wote wapiga kura.
Baada ya kupiga picha na kutoa zawadi za vinyago kwa kina Drogba, Kaka, Robinho, Valdes, Luis Fabiano, etc. Sasa Rais yupo Spain kuongeza collection yake ya picha na jezi za football stars wengine.
HUYU NDIYE RAIS WETU NA SISI NDIYO WANANCHI TUTAKAOPIGA KURA ZA KUMPA MIAKA MITANO ZAIDI YA KUVURUGA NCHI YETU