Foleni za magari ni maisha bora - Kikwete

Tafadhali mtu aniamshe kama nina ota! Siwezi amini Rais anatumia uwingi wa magari Dar kama kipimo cha maisha bora kwa watanzania? hii mizaha mingine sasa ni too much! hivi ni kweli kuwa hajui kuwa huo msongamano unasababishwa na uvinyu wa barabara na pengine sio uwing i wa magari! yaani bado siamini Rais anahimiza watu wanunue hii mitumba ya magari, anahimiza nchi kuwa jalala! ooooh! God please have a mercy on us, please show us were did we go wrong!

Mambo ya Marie-Antoinette supposedly alivyowambia wafaransa "let them eat cake". Wananchi wako wana GDP Per Capita inayocheza na mstari wa $ 500, wewe unawaambia wanunue magari zaidi.

Inaonyesha JK hawafikirii modal Tanzanians, anafikiria watu fulani tu wa mijini katika mipango yake. Angekuwa anawafikiria modal Tanzanians angeona kuwaambia wanunue magari wakati hata mkokoteni hawana ni kuwatukana.
 
Hata hayo magari yangekuwa standard..lakini kati ya mikoa 26 Mkoa mmoja wenye foleni(asubuhi/jioni)ndo maisha bora..:A S-eek:???
Kama ni hivyo mbona hamsemi kama mapato yameongezeka..??? Maana katika magari kuna kodi anuai..
Mkuu punguzaga masihara...,
 
Namshauri JK aboreshe uteuzi wake kwa kuangalia watu wenye akili nzuri. matatizo ya watanzania yatapungua, traffic jamms zitapungua, mikataba mibovu itapungua, tofauti kati ya wenye nacho na wasio nacho itapungua na mipango mzuri inayotekelezeka itakuwepo.
Umasikini wa Tz siyo mali bali ni akili!
Kusoma zaidi hakuongezi akili bali kunoa akili iliyopo kichwani.
Punguza wanaoitwa wasomi wengi kuanzia Phd za kukariri, ufanisi hakuna, ushauri kwake zero!
Serikali zilizopita, wanaojiita wasomi walikuwa wachache lakini ufanisi ulionekana zaidi.
 
Ni bahati mbaya sana tunaongozwa na wanasiasa wanaoweza kusema lolote ilimradi afurahishe uma na wasikilizaji wengine ambao wengi wao wanakuwa si wajuaji wa nini kinaendelea huku duniani. Ingawa hulka ya mwanadamu ni kujilimbikizia mali ikiwa ni pamoja na magari lakini kiongozi wa nchi hatakiwi kuwaambia watu wake wanunue magari mengi kwani athari ya magari mengi si foleni tu bali hata katika uchafuzi wa mazingira. Watu wote walio makini huangalia mbali zaidi ya pua zao na si leo tu mradi umekula na kulala. Hili ndio tatizo letu kama Waafrika kwa ujumla na si Watanzania. Hata ukiwaangalia Waafrika waishio Haiti ni hivyo hivyo; mipango yao ni mibovu na viongozi wao hawana dira nzuri ya kuangalia. Ndio maana leo hii utakuta serikali ya Kiwete inajenga barabara ya Sam Nujoma ikiwa na two lanes! Na ya Mandela inakarabatiwa (bila sababu ya msingi) kwa mabilioni lakini unarudisha two lanes zile zile zilizojengwa miaka 20 iliyopita! Huu ndio upungufu wetu katika kupanga na kuangalia mbele. Utadhani huku kwetu hakuna msomi hata mmoja anayeweza kuwa kufikiria strategically na kuona kipi kitatokea miaka 60 ijayo. Wenzetu wanapanga mipango yao kuangalia kizazi kijacho kitaishi vipi lakini sisi ni kuangalia kama matumbo yetu yatashiba leo.
Utaamini kuwa underground train ya London ilijengwa miaka zaidi ya 80 iliyopita? Watu waliobuni ni watu waliokuwa wanaangalia mbali sana, si akina Kikwete na wenzake
 
sidhani kama kikwete anaelewa athari ya watu KULAZIMIKA kuwa na magari kufika makazini mwao!

hivi Kikwete kuna fani anayoiweza kweli? ooh i forgot ...kuchekea wananchi
 
yaani bado siamini Rais anahimiza watu wanunue hii mitumba ya magari, anahimiza nchi kuwa jalala! ooooh! God please have a mercy on us, please show us were did we go wrong!


Kwani hamjui....mbona mnamtaka Mungu ubaya? Kuchagua mchague wenyewe leo mnataka Mungu awaambie mmekosea wapi???? Hapo pa kumpa Mkwere na jamaa zake nchi
 
kikwete hana kosa katika kauli ile kwa sababu amewaambiwa watu wanunue magari mengi ikiwa kama njia ya kujidefence kutokana na foleni za mjini ambazo tunajua chanzo chake si wingi wa magari bali ni ubovu na uchache wa miundombinu.

pia hebu tuigeuze upande wa pili ile kauli yake mfano angesema " kutokana na wingi wa foleni TUNAWAOMBA wananchio wasinunue magari hadi tutakapofanya matengenezo ya miundo mbinu" jee huu watu si wangesema ni udikteta. kwa kauli hiyo mie naona hana kosa. ila kusema wingi wa magari ndo maisha bora . . . . . . hapo kiddooogo DKT ameteleza!!!
 
kikwete hana kosa katika kauli ile kwa sababu amewaambiwa watu wanunue magari mengi ikiwa kama njia ya kujidefence kutokana na foleni za mjini ambazo tunajua chanzo chake si wingi wa magari bali ni ubovu na uchache wa miundombinu.

pia hebu tuigeuze upande wa pili ile kauli yake mfano angesema " kutokana na wingi wa foleni TUNAWAOMBA wananchio wasinunue magari hadi tutakapofanya matengenezo ya miundo mbinu" jee huu watu si wangesema ni udikteta. kwa kauli hiyo mie naona hana kosa. ila kusema wingi wa magari ndo maisha bora . . . . . . hapo kiddooogo DKT ameteleza!!!

hawezi kuwa dikteta kama unavyosema ANAWAOMBA.........nchi nyingi duniani zinasisitiza na kuomba watu wao wapunguze kutumia magari kwa uchafuzi wa mazingira bin global warming achilia mbali foleni..........
 
yaani una mpango wa kujenga fly overs au pass over Dar au Arusha wakati sumbawanga, Namtumbo, Musoma, kigoma etc kuna watu hawajawai kuona lami?hawajui lami ikoje...wengine hata wakiona gari wanakimbia.....kwa hela gani kwanza...ivi anafanya mchezo...angesema labda hela hiyo angerekebisha reli ya kati iwe kwenye kiwango cha kimataifa na kununua mabehewa na injini za kisasa...pamoja na kuboresha bandari ya DSM, Tanga, Mtwara na Kigoma...kuweka miundombinu itakayotufanya tushindane vizuri kiutalii na kenya etc...pamoja na kwamba mambo mengine yako chini ya uwekezaji binafsi kama hao kina rites wa india etc...hivi jamani, hata kama mimi si mwanauchumi..mawazo ya mkuu wetu kama kweli aliongea hivyo, ni ya kiuchumi kweli?

gari ni necessity, si utajiri...ndio maana hata kama mtu unayo gari bado unalia mafuta garama na vitu vingine...ni necessity, asije akaenda nchi za wenzetu akasema tz inaendelea ndio maana watu wananunua magari..hiyo ni necessity...kama wangetuwekea trams na public transport za kueleweka hapa kwani hata magari tungenunua ya nini..

hivi wanachoshindwa ni nini jamani, kutandika reli upande mmoja wa barabara kuanzia kimara hadi posta na maeneo mengine ili tutumie trams kama wenzetu ulaya kuondoa hivi vipanya...futa vipanya hivi weka metro ya uhakika kila kitu mwake...hata haihitaji kujenga reli kwa juu/fly over kama wengine wanavyofikiri...treni/trams zinaenda sambamba tu na magari kwa wale walioishi ulaya...Tz kalagabaho..
 
bora sikuisoma asubuhi.......he z sick

I saw that heading kwenye gazeti la Majira kwa mbali wakati nikiwa kwenye foleni barabarani...Nikajizuia kulinunua gazeti kwa kuwa sikutaka kuamini macho yangu! Hili kweli ni jipu la kwapa!
 
I saw that heading kwenye gazeti la Majira kwa mbali wakati nikiwa kwenye foleni barabarani...Nikajizuia kulinunua gazeti kwa kuwa sikutaka kuamini macho yangu! Hili kweli ni jipu la kwapa!

ukinyanyua mkono linauma, ukishusha linauma!!! huyu kiongozi wenu sijui kama afya yake ya ubongo ni njema (samahani kama mtu atakwazika) This sickens
 
Msihangae... ni PhD holder wa Biochemistry(sore kama nimebugi), na mzee wa kuzindua na kufunga warshaz na kongamanoz!!
 
I saw that heading kwenye gazeti la Majira kwa mbali wakati nikiwa kwenye foleni barabarani...Nikajizuia kulinunua gazeti kwa kuwa sikutaka kuamini macho yangu! Hili kweli ni jipu la kwapa!

hahaha, mkuu umenikumbusha mbali kwelikweli...jipu la kwapa....hahaha, watu wanajua kutunga nahau jamani..ati ukinyanyua mkono linauma, ukishusha linauma, dah!
 
ukinyanyua mkono linauma, ukishusha linauma!!! huyu kiongozi wenu sijui kama afya yake ya ubongo ni njema (samahani kama mtu atakwazika) This sickens

Duh! Mwenzetu umeomba urai wa Rwanda au Ethiopia?
 
Hivi kuna fungu lolote limetengwa kwenye budget iliyopitishwa hivi karibuni kwa ajili ya hizo fly overs? Kama haipo hizo hela watazitoa wapi?

Halafu watu wanapiga makofi meno yote nje...!!!

Ama kweli SIKIO LA KUFA......
 
I am completely frustrated with the way Vyama Vya Upinzani have allowed Kikwete to get away with these gaffes. A week ago, President Kikwete said that he is going to deal Kimya Kimya with trouble-makers, and surprisingly opposition parties remain numb.

I am wondering if these parties are serious on winning the election, let alone removing CCM from power. They should seize the moment and use these gaffes to their advantage by showing how flawed president Kikwete’s arguments are.

Frankly speaking, if Vyama vya Upinzani are not going to rebut CCM’s innuendos then they should expect to be loose miserably in November elections! Politics is all about using your rival’s mistake to your advantage ….
 
Back
Top Bottom