Foleni za magari ni maisha bora - Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Foleni za magari ni maisha bora - Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tindikali, Jul 19, 2010.

 1. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 770
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Na Shadrack Sagati;
  HABARI LEO 18th July 2010


  Katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa kumtambulisha mgombea mwenza, Dk. Mohamed Gharib Bilal na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein katika mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salaam...Alitolea mfano wa namna Watanzania walivyopata maendeleo kwa kununua magari mengi na kusababisha tatizo la foleni na ufinyu wa barabara.

  “Sasa nawahakikishieni msiache kununua magari, endeleeni kununua kwani kuanzia mwaka kesho mipango yetu ni kujenga barabara juu ya barabara zingine,” alisema Rais Kikwete.


  [​IMG]

  Hata miji yenye mabarabara angani na chini ya ardhi na juu ya maji, bado wanahimizwa wasijilimbikizie magari. Hayo mabarabara ya angani Kikwete atayajenga lini wakati haya ya ardhini tu ni vichochoro vya matope? Huyu Rais wetu mzima jamani?
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ama ni kilaza anayeropoka bila kujua anachosema ama ni mjanja anajua sana ujinga wa watanzania hivyo anataka autumie ujinga huo kisiasa
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ama kweli Mpopo alisema kweli - The Beautyful Ones Are Not Yet Born!
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kikwete ana haki ya kusema hivyo kwa sababu ile adha ya foleni haimhusu kabisa. Ongezeni magari ndugu zangu Watanzania.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo letu watz hatupendi watu ambao ni makini ila tunapenda viongozi wasanii kama JK!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  duh.. ni wapi hasa huko? labda sijaelewa maana ya kujilimbikizia magari.
   
 7. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 770
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Tokyo, Moscow, Los Angeles, Shanghai, Sao Paolo, London, Paris, Mumbai, Bangkok, ni baadhi ya miji yenye maendeleo ya miundombinu ya barabara lakini bado kuna misongamano ya kutisha barabarani.

  [​IMG]

  Wakazi wa huko wanahimizwa kutumia usafiri wa wengi. Watu wa familia moja, kwa mfano, wanapokuwa wanaelekea maeneo mamoja wanashauriwa kutumia gari moja badala ya familia moja kujilimbikizia na kutumia magari mengi.

  Dar-es-Salaam hatuna hata mabarabara ya kutosha kama ya miji mingine yenye magari mengi na matatizo ya msongamano halafu bado tunaambiwa tuongeze magari. Ni ushauri mbovu wa kupotosha.
   
 8. G

  Gashle Senior Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kaaz kweli kweli, kwani mnategemea mtu anaecheka cheka kila dakika aseme nini? Ndio mwisho wa kufikiri kwake. Nimesoma hiyo nukuu yake, NIMECHEKA, kwa HUZUNI!
   
 9. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 770
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Hatuna mazoea ya kupeana kazi, achilia mbali uongozi, hata kazi za kawaida tu kwa misingi ya uwezo. Tunatunmia mfumo wa viujumbe, na kujuana na undugu na zamu zamu.

  Na ndio utamaduni uliozaa Kikwete.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Tindikali unataka kumpa Kikwete masomo ya carbon footprint wakati yeye anakwambia hatujafikia level ya industrialization ya kuwa concerned na carbon footprint, if anything the west ambao washaendelea siku nyingi ndio wanaotakiwa kupunguza magari, sie madongokuinama tunatakiwa tuongeze magari.

  To me the wrong thing with this, is that you don't ask people to increase cars before building the roads.You first build the roads, then you can ask people to continue to import cars. You can't account that which you haven't realized.
   
 11. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,670
  Likes Received: 21,902
  Trophy Points: 280
  Mrema kesha sema kuwa huyu ndio kiongozi makini. Nchi yetu inatia uchungu.
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Thats correct sir.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa kifupi hatuna viongozi makini, ndio maana VITIMBI haviishi.

  Btw, mmemsoma dr. Mkwere hapa?? Bwe he he he..

  Kama rais wetu mtukufu anaeza kuchezeshwa shere na wahuni au waganga njaa wachache wakampa udokta na yeye akaingia kingi, what can we expect from this guy..its fvcking unbelievable.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280


  Na huku ndiko kwenye barabara za juu ya maji na angani?

  Wakazi wa huko wanahimizwa kutumia usafiri wa wengi. Watu wa familia moja, kwa mfano, wanapokuwa wanaelekea maeneo mamoja wanashauriwa kutumia gari moja badala ya familia moja kujilimbikizia na kutumia magari mengi. [/quote]

  Ok hapa nimekupata ila ulivyotumia neno "kujilimbikizia" sijui kama ilikuwa inasema hilo.

  absolutely
   
 15. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Huyu kichaka anajua kwamba mapato mengi kwa ajili ya matanuzi yake yanatokana na kodi za magari (kodi kwenye gas, registration, import taxes, road licence, kodi za kuingiza magari barabarani, parking, n.k., n.k.). Mambo ya foleni, envirinment mtajujua wenyewe.
   
 16. tartoo

  tartoo Senior Member

  #16
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 2, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hili hata washauri wake ni vilaza tu!

  Mimi nina mashaka kuwa muda huo alisahau kuwa yeye ni raisi wa nchi....lakini hapana....alikuwa anaelezea mafanikio ya serikali yake kwa kipindi cha miaka minne na miezi kadhaa.Hakukosea, alikuwa raisi na amiri jeshi mkuu na bila hiana akatoa hii kauli ambayo inaonesha uwezo wake wa kufikiria.......
   
 17. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hahaha... hiyo ya dr mkwere imenifurahisha sana na nadhani ndiylo jina linalomfaa zaidi.... hahah...

  mi kama magari yaliyojaa bongo yangekuwa angalau nusu-mapya (achilia mbali mapya), ningekubaliana naye kuwa huenda maisha yameanza kuiona njia ya ubora japo kwa mbaaali.... sasa magari yenyewe wala si mengi na karibu yote yalitakiwa kuyeyushwa kuwa malighafi kwani hata walioyatengeneza wakisikia kuwa bado yanatumika watapigwa jakamoyo! mengi yananunuliwa yakiwa yamechakaa kupita inavyoweza kuelezeka! nchi imegeuzwa dampo la magari chakavu, na hii ni kwa sababu ya mipango mibovu ya ukuaji endelevu wa miji yetu isiyoenda sambamba na uboreshaji wa makazi na miuondombinu ya usafiri. matokeo yake public transport katika miji mikubwa tz imekuwa adhabu kali sanan kiasi cha kila anayetaka kujitetea dhidi yake kuangalia kigari japo cha mtumba kimsaidie kujikokota katikati ya foleni (jam) ya kutisha kwenda kibaruani!

  tz wala hatuna magari mengi na hivyo kama magari ni kiashiria cha maisha bora, basi ni dhahiri na maisha bora bado tunayasikia kwenye bomba tu. tatizo la tz ni miundombinu tu, kwisha kazi!
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,649
  Likes Received: 4,751
  Trophy Points: 280
  Mtoto akililia wembe mpe ,mliambiwa huyu siyo mtu makini mkampa urais, oneneni mzaha anaofanya.
   
 19. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sipati picha kama angeelezea hayo 'mafanikio' kwa masaa matano aliyoyataka ingekuwaje.
   
 20. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tafadhali mtu aniamshe kama nina ota! Siwezi amini Rais anatumia uwingi wa magari Dar kama kipimo cha maisha bora kwa watanzania? hii mizaha mingine sasa ni too much! hivi ni kweli kuwa hajui kuwa huo msongamano unasababishwa na uvinyu wa barabara na pengine sio uwing i wa magari! yaani bado siamini Rais anahimiza watu wanunue hii mitumba ya magari, anahimiza nchi kuwa jalala! ooooh! God please have a mercy on us, please show us were did we go wrong!
   
Loading...