pleti namba
Member
- Feb 17, 2015
- 91
- 32
Hawa wamarekani ni wabinafsi sana sikunyingine sijisumbui kupoteza pesa zangu na usingizi kwa ajili ya upuuzi wao
Wafilipino na boxing wapi kwa wapi?
Kazi yao ni kuchoma viazi
Pacquiao akajifunze kuchoma viazi
Boxing ina wenyewe
Floyd ndio dume
48-0
Who's next? Amir Khan?
iweke hapa mkuuBora kumbe siko pekee yangu niliyecomment kuhusu nyonyo za B.
Ha ha ha! Uoga wa Mayweather umetuharibia game. He was too defensive, passive & boring like Mourinho's chelsea. Yes, kashinda kweli lakini kwa counter attacks. Na ndio maana alikuwa booed.
Ha ha ha! Uoga wa Mayweather umetuharibia game. He was too defensive, passive & boring like Mourinho's chelsea. Yes, kashinda kweli lakini kwa counter attacks. Na ndio maana alikuwa booed.
Endelea na gubu lako lakini ujue wenzako leo wanatawazwa mabingwa.
Hawa wamarekani ni wabinafsi sana sikunyingine sijisumbui kupoteza pesa zangu na usingizi kwa ajili ya upuuzi wao
Huu mvao Wa huyu mama misichana ya bongo lazima itaiga tu!!
Uungwana ni vitendo. Manny kapigwa. Yeye alikuwa anashambulia gloves na akibahatisha ngumi mara chache. It was not an easy game, it was close lakini the best man won.
Hahaha raha sana. Best BAK najua team mayweather tulikuwa wachache sana. Same trick ya kuvizia and save his breath worked. Congrats mate
Congrats to you too Best. Naona timupakiyao wamenuna sana wanadhani ushindi unapatikana kwa kurusha ngumi hewa lol!
Kawaboa wengi kwa Statistics zipi? MyWeather kashinda ndo plan yake ilikuwa,Man P alitaka KO lkn kafeli,sasa nani mjanja aliyeshinda au aliyefeli?Mkuu, nilitaka ajiamini kama Man pac, alivyo fanya. Inaonshesha hakuwa na mpango wa kummaliza Pac bila ubishi. Naamini watu wengi includes me, nilitaka kuona Floyd anafanya vizuri zaidi kwakujiamini nasio kukimbia kimbia. Amewaboa wengi japo ameshinda.
PACQUIAO NI SHUJAA WANGU.!
Tusimkubali mtu kwa sababu ya rangi yake. Wala tusimkatae mtu sababu ya rangi yake. Kufanya hivyo ni ubaguzi. Ni vema tumkubali mtu au tukatae kwa sababu ya uwezo wake.
Kwangu mimi nakubali sana uwezo wa Manny Pacquiao. Uwezo wake ktk boxing, uwezo wake kisiasa kama mbunge, na uwezo wake wa kutetea watu wanyonge.
Historia yake inaonesha kuwa ametoka familia masikini sana. Amesoma shule hadi kuhitimu sekondari akivaa nguo zenye viraka. Lakini aliamini ipo siku Mungu atamfungulia njia. Na alipofanikiwa sehemu kubwa ya mali zake anagawana na maskini.
Licha ya kuwagawia misaada huwa anawafundisha mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi. Anasema hapendi maisha aliyopitia wengine nao wapitie.
Ni mcha Mungu mzuri. Aliposhinda Ubunge mwaka 2010 alisema si kwa nguvu zake bali ni uweza wa Mungu. Alisema "Only GOD can lift someone from nothing to something, as he did to me"
Pacquiao amekulia kwenye mabanda ya walalahoi maana baba yake hakuwa na uwezo wa kujenga nyumba. Historia yake ni very inspirational na inawasaidia wengi walio kwenye ugumu wa maisha kutokata tamaa.
Lakini licha ya kuzaliwa kwenye lindi la umasikini alijipa moyo siku moja ataweza. Alipojaribu Basketball akafanikiwa, alipojaribu siasa akafanikiwa kuwa mbunge, alipojaribu ndondi akafanikiwa kuwa bingwa wa dunia. Na amesema atagombea Urais wa Philipines akifikisha miaka 40. Mafanikio yake ni darasa tosha kwa wanaopita kwenye kipindi kigumu leo wajue kesho yao ni nzuri.
Sasa niache kumuunga mkono mtu mwema kama huyu nije kumuunga mkono "mpenda anasa" Mayweather kisa tu ni mweusi??? Hapana kwa kweli. Weusi au weupe sio kigezo cha kumfanya mtu kuwa bora.
Mimi ni muunini wa PanAfricanism lakini ktk hili nasema big NO. Mayweather anajulikana Marekani yote kwa kupenda anasa. Usipomkuta club akilewa pombe, utamkuta casino na wasichana au akicheza kamari. Picha zake nyingi kapiga akionesha ufahari wa mali alizonazo.
Picha yake ya hivi karibuni iliyorushwa na CNN na kuibua mjadala mkubwa ni ile aliyopiga akiwa ametandaza fedha chumbani mithili ya godoro kisha akalala juu yake. Fedha hizo zinakadiriwa kuwa dola bilioni 3 ambazo ni sawa na Shilingi trilioni 6.5 za kitanzania.
Hii ni karibu nusu ya bajeti ya nchi yetu. Lakini mtu mmoja kazijaza kwenye room afu kazilalia. Eti ndo mnasema tuunge mkono weusi wenzetu. To hell.!
Kama weusi ndo wa aina hii bora nisiitwe mweusi. Weusi wa kupenda anasa. Weusi wa kupenda zinaa. Weusi wa starehe za pombe na makasino. Noooo.. nasema NO.
Mimi hata Paquiao apigwe lakini atabaki kuwa shujaa wangu. Go go Paquiao. Jina lako ni Emmanuel yani "Mungu Pamoja nasi" nami nakuombea Mungu awe pamoja nawe kwenye pambano hili.
Malisa GJ.!