Vitabu kama hivyo sijui hata kama vipo mashuleni siku hizi!... hivi nyie madogo huko mashuleni huwa mnasomaga vitu gani? Umewahi angalau kusoma hadithi au kusikia stori ya "Mpiga Filimbi wa Hamelini"? Ndio hizo filimbi anaulizia mleta mada raslimali.
Kuna uzi hapa kwa hisani ya Mshana Jr unazungmzia kitu hicho hicho, Mpiga filimbi wa Hamelin! Deliver every promise. Tumshukuru Rais kwa kumbadilisha waziri wa elimu maana yalikuwa mjanga!
Ahahahaaa, baba pakaa,alisema...........
... na za bati pia zipo; hao jamaa (mgambo na sungusungu) wakizining'iniza shingoni wanajihisi ni alfa na omega! Halafu ni kama kanuni fulani hivi mifukoni lazima wawe na kadi fulani iliyochoka mbaya! Ha ha ha! Mkongwe johnthebaptist anajua sana hizo mambo.
... kabisa! Leo madogo kutwa kushinda Insta na FB hawajui kingine. TEHAMA kwa upande mwingine imeleta majanga hasa kwa vinchi kama vya kwetu. Vijana hawashugulishi brains to the maximum kilichobaki ni kuchat upumbavu tu huko whatsap na sms.Hizo wanaongelea zile tulitumia kupiga kukiwa na tukio au wakiwa wanapandisha na kushusha bendera ya Taifa.
Hizi za ala nyingi zilikua za bati, siku hizi wanaleta za plastic.
Vitu kama hivyo licha ya kuwa burudani vilichangamsha ubongo na kuongeza ubunifu. Ilihitaji kujifunza kuipuliza vizuri na kupangilia vidole ipasavyo ili zitoe mlio unaotakiwa.
Yes huu mzigo makini, YAMAHA walikuwa wanatengeza kama hizi...View attachment 2074447
Mimi niliruka sana na aina hii ya flute hadi parade
... madogo wenyewe hawa mlo wao kiepe yai la broiler kwa sana na fanta chupa zenyewe mnazichezea siku hizi? Toto la kiume linashindana wowowo na manyonyo na dada zake? Bure kabisa!Hawa wajukuu hawataweza kuzipuliza
Zipo ila kwa uchache sana.Habari wakuu.
Kwa wale ambao wamesoma elimu ya msingi miaka ya 80 watakuwa wanakumbuka tulikuwa na bendi za gwaride la shule na tulikuwa tukitumia ngoma na zile filimbi zenye matundu manane. Hizi filimbi nakumbuka zilikuwa zinatolewa na serikali kwa ajili ya mashule na pia zilikuwa zinauzwa kwenye maduka mitaani.
Tulikuwa tunafundishwa namna ya kutumia ala hii ya muziki. Ni miaka mingi sijawahi tena kuiona ala hii ya muziki ikiuzwa mahali popote. Kwa mwenye kujua kama bado zinapatikana anijulishe ni wapi. Nakumbuka zilikuwa bei rahisi sana maana zilitengenezwa kwa mrija (pipe) ya bati na kipande cha mti kwenye sehemu ya kupulizia upepo. Miaka ile nadhani bei ilikuwa kama shilingi kumi hivi!
Ngoja niangalie hapa Arusha Kuna mahali nimeelekezwa nikikosa nitakutafuta. Niachie mawasiliano pm.Mchina ametoa za plastic.
Ninaziuza dukani kwangu.
Mikoani natuma.
Unataka ngapi?
Bei 1 ni 1k TSHS
IKo vizuri Hiyo ila bei yake juuMi ni nayo ilitengenezwa na kampuni ya YAMAHA. Iko poa saana
😂😂 Mapafu dhaifu au?Hawa wajukuu hawataweza kuzipuliza
😂😂😂... madogo wenyewe hawa mlo wao kiepe yai la broiler kwa sana na fanta chupa zenyewe mnazichezea siku hizi? Toto la kiume linashindana wowowo na manyonyo na dada zake? Bure kabisa!
Umezaliwa miaka ipi Mkuu?Hizo filimbi zina Kazi gani
Ukijujua kupiga filimbi saxophone haikusumbuiHalafu mi nilikuwa fa'la sana ujue!
Eti ndo nilikuwa mkali wa kupiga filimbi, dah!!!
Sema hapo juu nimesoma kuhusu filimbi za miti... dah, hizo sikuwahi kuziona aisee!! Sasa ile hollow walikuwa wanafanya fanya vp kwa mfano kuitengeneza?!