Habari wakuu.
Kwa wale ambao wamesoma elimu ya msingi miaka ya 80 watakuwa wanakumbuka tulikuwa na bendi za gwaride la shule na tulikuwa tukitumia ngoma na zile filimbi zenye matundu manane. Hizi filimbi nakumbuka zilikuwa zinatolewa na serikali kwa ajili ya mashule na pia zilikuwa zinauzwa kwenye maduka mitaani.
Tulikuwa tunafundishwa namna ya kutumia ala hii ya muziki. Ni miaka mingi sijawahi tena kuiona ala hii ya muziki ikiuzwa mahali popote. Kwa mwenye kujua kama bado zinapatikana anijulishe ni wapi. Nakumbuka zilikuwa bei rahisi sana maana zilitengenezwa kwa mrija (pipe) ya bati na kipande cha mti kwenye sehemu ya kupulizia upepo. Miaka ile nadhani bei ilikuwa kama shilingi kumi hivi!