Ifahamu Bendi ya Kassav

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,090
Habari Wakuu, leo nimeona ni vyema nikawashirikisha kidogo kuhusu bendi moja ya zamani kidogo ambayo ilitupatia burudani sana miaka ya 1990 enzi hizo wakati ambao tulikuwa tunaonesha ujuzi wetu wa kusakata rhumba vyema ingawa hata mashairi tulikuwa hatuyafahamu. Karibu sana.

Bendi ya Kassav, mojawapo ya vikundi vya muziki vilivyo na ushawishi mkubwa katika historia ya muziki wa Karibea, ni bendi ambayo inashikilia nafasi muhimu sio tu katika eneo hilo bali pia hata kimataifa. Andiko hili litaangazia muktadha wa kihistoria wa kuibuka kwa bendi, pia nitawaangazia watu muhimu ndani ya kikundi hili, na mwisho tutatazama na kuchambua athari za muziki wao huku tukionesha kuwatambua watu mashuhuri ambao wamechangia mafanikio yao.
  • kassav.jpg
Bendi ya Kassav iliundwa mwishoni mwa miaka ya 1970 wakati wa sekeseke wa mwamko wa kitamaduni katika nchi za Karibea. Bendi hii ilianzishwa na Pierre-Edouard Decimus na Jacob Desvarieux, wanamuziki wawili kutoka kisiwa cha Guadeloupe cha Karibea cha Ufaransa, sehemu ambayo pia anatoka gwiji wa muziki, Bwana Mkubwa Francky Vincent. Enzi hizo bendi hii ilikuwa na sifa ya ajabu ya kurejesha utamaduni, na walikuwa ni wasanii waliojitolea na waliotaka kukuza urithi wao wa ndani na kupinga utawala wa utamaduni wa Magharibi. Walikuwa katika kilele sawa na bendi kama vile Les Aiglons, Les Vikings De La Guadeloupe, na Exile One.

Mafanikio ya Kassav yanaweza kuhusishwa na talanta na kujitolea kwa watu kama Pierre-Edouard Decimus, ambaye alikuwa ni mpiga gitaa la besi mahiri sana, huku Jacob Desvarieux, mpiga gitaa na mtunzi wa nyimbo mzuri sana, waliunda uti wa mgongo wa sauti ya bendi ambao ulikuwa imara sana. Walitengeneza ala tamu za muziki na waimbaji wengine, kama vile Jocelyne Beroard, Jean-Philippe Marthely, na Patrick St. Eloi, ambao walikuwa ni sehemu muhimu katika kuunda utambulisho wa kipekee wa muziki wa bendi kutoka Karibea.
kassav1.jpg

Uwepo wa bendi ya Kassav kwenye muziki wa Karibea ulikuwa ni wa kipekee sana kwani mpaka sasa wanasifiwa sana kwa kuanzisha aina ya tofauti ya zouk, mchanganyiko wa midundo ya mitindo ya muziki ya Karibea na Kiafrika. Zouk, pamoja na midundo yake na ala za muziki ambazo zilikuwa zikiimbika vyema sana na mashairi yao, jinsi walivyotunga nyimbo zao ilikuwa zikifanana kimsingi na Bendi ya Byron Lee and Dragonaires.

Muziki wa Kassav ulionyesha urithi tajiri wa kitamaduni wa Karibea, wakati huo huo ukiwavutia kila rika la jamii ya watu wa Karibea na sehemu zingine. Nyimbo zao ziligusa mada za upendo, haki ya kijamii, na fahari ya kitamaduni, ambazo zilisikika kwa hadhira kote ulimwenguni.ukipata nafasi ya kusikiliza nyimbo kama vile Sye bwa ya 1987 au Mwen Malad Aw ya 1985 utakutana na wakali wa kucheza na mashairi na ala tamu sana.
Kassav-cover-PAM.jpg

Wakati bendi nzima ilishiriki katika kuunda urithi wa Kassav, watu kadhaa walikuwa ndo roho ya bendi hii. Jocelyne Beroard, mwimbaji mkuu, aliibuka kama sauti yenye nguvu ya kike katika tasnia ya muziki ambayo inayotawaliwa na wanaume, alikuwa na roho kama ya mwanamama wa wakati huo, Judy Mowatt wale wapenzi wa reggae watakuwa wanamfahamu vyema huyu mwanamuziki.

Jean-Philippe Marthely, mtu mwingine muhimu, alijulikana kwa sauti zake laini na uwepo wa jukwaani ulikuwa ni wakuvutia sana. Ukisikiliza nyimbo ya Kay-Manman utaona namna ambavyo Marthely anaonesha utaalamu wake. Ushirikiano wa Marthely na Jacob Desvarieux ulitoa baadhi ya nyimbo za kukumbukwa katika bendi, na ushawishi wake ulisaidia kuimarisha zaidi ukomavu wa bendi hii ya Kassav kama waanzilishi wa muziki wa Karibea.
maxresdefault.jpg

Upande wa Patrick St. Eloi, huyu ni mwimbaji na mtunzi mahiri wa sauti, alipanua zaidi muundo wa sauti wa bendi. Nyimbo za kutoka moyoni za St. Eloi zilikuwa zikiwakosa sana watu kwa namna ambavyo alikuwa akiimba, ukitaka kufahamu kuwa kipaji kinanolewa vyema namna ipi basi kuna wimbo wa West Indies ambao umetendewa haki kuanzia ala yake mpaka mashairi.

Bendi ya Kassav kwa kiasi kikubwa ni imeleta mabadiliko chanya. Muziki wao umeleta utamaduni wa Karibea katika mstari wa mbele katika kuutambulisha kimataifa, na kuruhusu watu kutoka asili zote kufahamu na kufurahia mila hai za eneo hilo, ukipita mitaa ya Calle Fortaleza pale San Juan, au Nassau, Bahamas utakutana na wazee wakiwa na radio zao Panasonic RF-562D zikiwaburudisha na nyimbo mbalimbali za Kassav huku wimbo pendwa zaidi ukiwa ni Ou Lé wa 1989 na kumbuka kuwa mwaka hu undo kulikuwa na nyimbo zilizobamba sana kama vile, If You Don’t Know Me by Now uliotungwa na kuimbwa na Kenny Gamble pamoja na Leon Huff, pamoja na wimbo wa So Alive kutoka kwa bendi ya Love and Rockets.
Kassav photo.jpg

Urithi wa bendi ya Kassav ni ushahidi tosha wa nguvu ya muziki katika kuziba migawanyiko ya kitamaduni na kukuza fahari ya kitamaduni. Uwepo wao kwenye muziki wa Karibea ulimwenguni kote hauwezi kupuuzwa. Ingawa urithi wao kimsingi umekuwa mzuri, ukosoaji na changamoto zipo ambazo hatuwezi kuzitazama pasipo kuacha kuangalia mchango chanya wa bendi hii. Asante sana Jocelyne Beroard, Jean-Philippe Marthely, na Patrick St. Eloi, mmecheza vyema na majukumu muhimu katika kuwapatia tumaini watu na ulimwengu.
Asante sana Kassav!
Lickkle more!
 
Nadhani ile Kassav ya mwanzoni mwa miaka ya 1900 ilikuwa nzuri sana. Jipakulie albam yao ya miaka hiyo hapa ujionee walivyokuwa wakali
 

Attachments

  • 09. An Mwe.mp3
    9.9 MB
  • 08. Domeyis.mp3
    9.5 MB
  • 07. Konkibin.mp3
    7.6 MB
  • 06. D_zodie.mp3
    8.8 MB
  • 05. Ou le.mp3
    8.8 MB
  • 04. Rache Tche.mp3
    9.3 MB
  • 03. Wep.mp3
    9.6 MB
  • 02. Djoni2.mp3
    13.8 MB
  • 01. S_ Dam' Bonjou'.mp3
    9.6 MB
  • 10. Apre Zouk la.mp3
    8.8 MB
Back
Top Bottom