Man Rody
JF-Expert Member
- Aug 4, 2022
- 1,273
- 2,940
Habari za majukumu wakuu..
Moja kwa moja kwenye mada, haina ubishi kwamba tasnia ya mziki kwa sasa imeendelea sana wote tunashuhudia vijana wanavojituma kusukuma gurudumu la bongo fleva kusogea.. kufanya mziki ni ndoto ya mamilioni ya vijana (nikiwemo mimi) lakini kwa hali ilivo sasa uhalisia ni kua mziki una wenyewe...
Kote kwenye sector za entertainment kuna walinda mageti (gate keepers) ambao wamejipa mamlaka ya kuchagua as they please nani wa kumpekeka mjini kama wasemavyo yani kum support mtu awe brand inayoingiza pesa!
Vijana underground wengi sana wamekata tamaa kufata ndoto zao sababu ya mazingira magumu yaliyowekwa na washika dau, imagine mtu wa hali ya chini anaependa kufanya mziki studio tu ataambiwa laki 2 au 3 ku record, video ya kawaida sana tena unga mwana utakuta laki 4 mpaka 5 (mavazi,location,chakula), aseme aende radio watamdandia awapoze hata elf 50 radio ndogo, zingine mpaka 100,000 na hapo ni interview tu akitaka rotation ya ngoma yake ajipange kucheza na ma dj na kama ngoma sio nzuri sana ndo watmlia hela tu wala hatopata support anayotegemea, vituo vya t.v mambo yale yale pesa pesaa... mtu akipga hesabu anaamua akaushe tu afanye mishe zingine
Hii hali imepelekea over saturation ya mziki wetu yan wasanii wale wale kila siku hakuna ladha mpya maskion mwa watu, watu watauliza mbona wasanii kama lody music na badest 47 wametoka bila connection, ni kweli 100% kila mtu ana bahati yake kuna wasanii wametusua na underground hit iliyopenya organically ila uhalisia unabaki mazingira yamebanwa na hata ma star wa zaman waliojaribu kurudi wengi tu imewawia ugumu coz mambo yamebadilika yame take over majangili mapya.
Sasa kuna shortcut za kutusua katika mziki wetu kama kuroga sana na makafara, skendo za michongo na ma star, kama ni msichana kujirahisisha kwa wadau na zingine ila sio wote tunaweza fanya hayo so nini hatima ya bongo fleva miaka ya mbele.
Tunahitahitaj wawekezaji zaid sector ya bongo fleva, content inalipa sana sasa hivi kila kitu online!! tunahitaji music labels, michuano mbali mbali ya kusaka vipaji, nafas maalum kwenye radio na ma t.v kwa underground..hivi baraza la wasanii lina deal na wakubwa tu hawana program yoyote ya kuvumbua na kuendeleza talent mpya??
Mwishoni naweka link ya nyimbo yangu nimefanya kwa kuunga unga kwanzia audio mpaka video nimeunganisha vipande vya video za wasanii wengine mana sina budget ya ku shoot proper video, tukiwezeshwa tunaweza aisee sio kila siku wale waleee.. Wassalaam.