Orodha ya wasanii ambao bongo fleva / hiphop imewapa mafanikio makubwa

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
1. DIAMOND PLATNUMZ - CEO wa wasafi fm na tv + label, msanii pekee mwenye msururu wa ndinga za kwenda mbele

1708280743408.jpg

2. MR NICE - Ni Diamond pekee ndie alieweza kumfikia ukwasi akiwa peak, miaka hio ya 2003 inasemekana alikuwa anamiliki ukwasi wa bilioni 1 ya enzi hizo

1708280798757.jpg

3. AY - Mzee wa commercial alikuwa kawaida kiuchumi kwa upande wa muziki ila alijiongeza kutumia pesa alizopata kwenye muziki kufanya investments kadhaa kujiongezea kipato, yupo low key anafanya mambo yake kimya kimya, aliwahi kuwa msanii wa kwanza kushoot video ya milioni 50 hata kabla ya ile kesi waliyolipwa fidia yeye na Mwana Fa

1708282979227.jpg

4. PROFESSOR JAY - Jifunze, ona, sema, elimika, pitia, hamasika... Joseph a.k.a Professor Jay, inasemekana mwamba huyu alikwa analipia kazi zake, alikataa unyonyaji wa album zake kuwa chini ya label, kama ni maokoto mshua huyu kayapiga, miaka hiyo 2004 analipwa milioni 400 advance ya kuuza nakala zake, hio ni kama bilioni ya sasa.

1708280951352.jpg

5. ALI KIBA - akiwa kijana mdogo kabisa alishaanza kushika milioni 200 enzi za muhindi wa GMC, yeye anakwambia ziliisha zote kisa "utoto", lakini haikuwa mwisho wa safari yake, huyu ni msanii ambae yupo kwenye game kitambo sana japo kuna kipindi huwa anapoa sana

1708281016057.jpg

6. MWANA FA - Ni kesi ya Tigo waliyopewa fidia ya bilioni 2.1 yeye na AY ndio imemweka kwenye hii orodha, yasemekana wawili hao kila moja aliondoka na milioni 700 baada ya kuwapa chao wazee wa mgao wenye connections zao na asante za wanasheria (hakuna cha bure bongo)

1708295219914.png

7. LADY JAY DEE - Binti machozi kautendea haki mziki wetu wa bongo nao mziki ukambarikia mafanikio makubwa,

1708280909404.jpg

8. JUMA NATURE - Kwa album zake alizotoa zilizohit hata namba hii pengine haimfai, nadhani alikosa tu usimamizi mzuri wa kusimamia mapato ya kazi zake, mziki wake uliwafaidisha zaidi wengine lakini hata kwa alichoambulia ilikuwa pesa ndefu.

1708280866545.jpg

BONUS kutoka Bongo Gospel

ROSE MUHANDO - Tatizo ni mashetani yaliyomo kwenye music industry lakini huyu mama ilibidi awe juu sana, katimila sana kutajirisha wengine, pengine kaambulia 20 % ya mafanikio yake

1708300855523.png
 
Kama kuna wasanii wamepiga pesa ni F.A na AY wamevuta sana mkwanja wakakomaa na kesi ya Tigo wamelipwa Billions bado AY katimkia ng'ambo kwa Biden..F.A anavuta 27M kwa mwezi (Alisema Wasafi)F.A anadiscovery 4 ya 2022
kesi ile ilimuinua zaidi FA, kwa upande wa AY alikuwa njema kitambo, kila mtu yasemekana alikunja milioni 800 baada ya gharama za mawakili na wazee wazito wa migao
 
kwa mauzo ya kazi za muziki kama kungekuwa na haki basi Rose Muhando angekaa namba moja mbele ya wote akiwemo Diamond. Huyu mama hadi leo hii anauza albamu zake. Mwaka 2005 alijaza Sheikh Amri Abeid Stadium Arusha. Huko Kenya ndo huwaambii kitu kuhusu Rose. Tatizo ni mashetani yaliyomo kwenye music industry
 
Mr Nice alikuwa na pesa ila alikuwa mshamba enzi zake alikuwa ndio Diamond watu wa kila rika walipenda nyimbo zake , tatizo alikuwa anawapambe kutwa anatoka Dar kwenda kwao Moshi akifika analewa na kurudi , sometimes anakodisha hata ndege na crew yake.

Mwisho wa siku akafulia akakimbilia kenya ,Mr Nice alishindwa hata na Matonya kwa uwezekezaji mwenzie ana hotels mpaka kenya plus kuwa na jina kubwa ,japo Kenya Mr Nice bado anajulikana kuliko hata Tz ila hana lolote .
 
Ila vichenji chenji si bado kidogo vipo vipo vya kusomeshea madogo english medium ndo kufulia ile hadi sufuri mkuu ?
 
Mr Nice alikuwa na pesa ila alikuwa mshamba enzi zake alikuwa ndio Diamond watu wa kila rika walipenda nyimbo zake , tatizo alikuwa anawapambe kutwa anatoka Dar kwenda kwao Moshi akifika analewa na kurudi , sometimes anakodisha hata ndege na crew yake.

Mwisho wa siku akafulia akakimbilia kenya ,Mr Nice alishindwa hata na Matonya kwa uwezekezaji mwenzie ana hotels mpaka kenya plus kuwa na jina kubwa ,japo Kenya Mr Nice bado anajulikana kuliko hata Tz ila hana lolote .
Mr Nice ni msanii anayekubalika sana mpaka kusini mwa Africa huko nyimbo zake wanazielewa japo hawajui alishafulia kwenye game
 
Kama kuna wasanii wamepiga pesa ni F.A na AY wamevuta sana mkwanja wakakomaa na kesi ya Tigo wamelipwa Billions bado AY katimkia ng'ambo kwa Biden..F.A anavuta 27M kwa mwezi (Alisema Wasafi)F.A anadiscovery 4 ya 2022

Kwa Tanganyika kesi yao inawezekana kuwa inside job vilevile. Wazee wa down town wanakwambia hakuna bahati mbaya kwenye pesa ndefu, kila kitu kinapangwa halafu pasu kwa pasu. Kwetu pesa za kampuni ni shamba la bibi zubaa ufe masikini.
Ndio maana yake hii nchi ikaitwa Bongo.
 
Back
Top Bottom