TANZIA Pengo lingine kwenye tasnia ya muziki wa bongo Fleva. Richard Ramadhan Tunda afariki dunia

Feb 6, 2024
40
50
RICHARD TUNDA:KIFAA TOKA TIP TOP CONNECTION, AMEFARIKI DUNIA NI MDOGO WA MKALI WA BONGO FLEVA TUNDAMAN..

JINA: Richard Ramadhan Tunda

KUZALIWA: Februari 3, 1989 (Miaka 35)

ALIPOZALIWA: Kinondoni, Dar es Salaam..

KIFO : 16 Februari 2024.

SANAA: Muziki wa Bongo Fleva..

HISTORIA YA MAREHEMU.
Richard alikuwa ni msaniii wa mwanzo kujifunza katika kituo cha Tanzania House Of Talent (THT) ambaye anaendeleza ujuzi wake katika kundi linalofanya vema kwa sasa katika medani ya bongo fleva,Tip Top Connection.

Ni nani asiyekubali kwamba Tip Top Connection imezalisha, kukuza wasanii wenye vipaji vya muziki vya kuzaliwa na si kujifunza?.

Tip Top iliundwa na wasanii mahiri na wasiochuja kwenye fani akiwemo Harid Tunda ‘Tundaman’, Kassim Mganga ‘Cassim’,Ahmed Ally ‘Madee’, Deso na ‘first lady’ wao Khadija Shaban ‘Keysha’.

Richard Ramadhan Tunda ni mdogo wa damu wa mmoja ya nyota wa kundi la Tip Top, Tundaman ambaye kwa wanaofuatilia muziki wa bongo fleva mwaka 2007 aliwahi kutamba na kibao cha ‘Marionse’.

Kabla ya kutoa ‘Marionse’ alitoka na ‘Limekushuka aliomshirikisha Mandojo na kurekodiwa studio za Baucha chini ya mtayarishaji Maneke, wimbo huo ulifanya vena na hata kutinga ‘Top 10’ katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini, hiyo ilikuwa mwaka 2005.

Richard ni msanii aliyepata kujifunza THT akiwa ni mmoja ya wasanii wa mwanzo kabisa kwani hata kina Mwasiti, Buibui walimkuta na hiyo ilikuwa mwaka 2004 na 2008 Enzi hizo mkurugenzi wao skies ni marehemu Ruge Mutahaba.

ALIPOTOKEA.

Richard alizaliwa wilaya ya Kinonondi mnamo Februari 3, 1989 kwa baba Ramadhan Tunda afisa mstaafu wa serikalini na Mama Juliana Herman aliyekuwa daktari katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (wazazi wake wote ni marehemu).

Alianza kupenda muziki tangu akiwa mdogo huku akivutiwa zaid na msanii wa marekani Craig David, Dully Sykes na Cassim kwa hapa bongo, huku shule ya msingi akiipata Karume alipomaliza darasa la saba mwaka 2004 na kisha kusoma sekondari ya mtakatifu Laurenti alipokomea kidato cha tatu...

Marehemu kabla ya kifo chake qlikuwa anasumbuliwa na nyama za pua ndio chanzo cha kifo chake na jina lake linalofahamika ni Richard na ni mdogo ake kabisa na Tundaman baba mmoja ila mama ndio tofauti..

Nyimbo ilimpa umaarufu KWA hii Miaka ya hapa katikati ni "basi imba"

Kwenye hiyo collabo alikuwepo yenye na kaka Dudu man..

Rest in peace..

Pingo lingine kwenye kiwanda cha Muziki nchini Tanzania..

😭😭😭

#funguka.

Unakumbuka nini kutoka KWA marehemu richard Tunda.
IMG-20240216-WA0117.jpg
 
Mbona simjui. Pengo linatokea wapi hapo?
 
Huo wimbo wa Marionse nilikuwa naupenda na sikuwa najua aliyeimba ni nani.
Apumzike kwa amani.
 
Kumbe nyama za pua zinaua.

Naukumbuka wimbo huo wa basi imba. Mungu ampumzishe mahali pema
 
Back
Top Bottom