Ficha IP Adress yako kwa kutumia VPN (Android users)

Ndio VPN zinaficha IP address Sema mpaka utumie VPN za ukweli na Mara nyingi ni za kulipia kwani wewe umetumia VPN gani hiyo mpaka inaleta ads za bongo
VPN master, kitu ka hicho, hizo ads zinakuja sehemu nyingine eg kwenye browser au program nyingine kwenye simu ambazo zina ads, I mean mfano unapoingia kwenye chrome wakati unatumia VPN ambayo imekupa IP address ya Netherlands hapo nilitegemea kwenye website yoyote ninayoingia nitaona ads za Netherlands kwa sababu naonekana nipo Netherlands lakini nakutana na ads za bongo, hapo ndo napata wasiwasi kama hiyo VPN inafanya kazi kweli au magumashi tu
 
Ad networks siku hizi nyingi hazitumii IP Address kukutumia ads, zinatumia information iliyopo kwenye browser,sites nyingi zinatunza data kwenye browser yako kila unapo~browse, so ads network kama Google wanajua wewe ni mtu unapenda kufungua vitu gani, wanatumia hizo data zako kukuletea ads ambazo wanahisi utazipenda.

Bado pia kuna kuwa logged in wakati wote, mfano usipologout Facebook au Google, wana uwezo wa kumonitor karibia kila kitu unachofanya online, tena ukilogin kwenye Chrome au Firefox ndio kabisaa, Google wanajua kila website uliyofungua regardless ya IP Address yako kua nchi tofauti, wanajua unapenda sites za bongo kama JF, wanajua unachopenda kutafuta, lugha unayotumia, hizi zote ni variables zinatumika kukuletea ads. Nadhani nimeeleza kwa lugha nyepesi kabisa, kama unataka very technical details ya jinsi system nzima inavyofanya kazi uliza.
 
Nimekuelewa na chenji inabaki.... ahsante sana, so VPN nzuri ni ya kununua siyo?
 
Nimekuelewa na chenji inabaki.... ahsante sana, so VPN nzuri ni ya kununua siyo?

Za kununua ni nzuri ndiyo, zitaficha IP Address lakini kama umejipanga kufanya chochote ambacho ni illegal, hapa naongelea criminal activities kubwa sana kama kuuza madawa au ujambazi, basi ujue watafuatilia logs watakupata, ila kama ni mambo mengine we jidai tu online. Kuna tor pia ambayo ina security kubwa sana kuliko hizi VPN nyingine ila tatizo lake speed yake inakua chini kidogo sababu yenyewe inakurusha zaidi ya computer kama tano randomly kabla haijakufikisha destination, tor inayofanya kazi ni kama hivi [Wewe -> VPN -> VPN ->VPN ->VPN -> Website] ila VPN nyingine za kawaida ni [Wewe -> VPN -> Website].
 
Izi za playstore ni magumash tu. Za pc Ipo unabadili IP adress vzuri na unaweza stream hata video/ mitandao ambayo ipo limited kwa nch flani
sikubalian na wewe eti za playstore zote ni magumashi... kuna nyingine ziko vizuri tu eg.. hotspot shield, hola vpn nk.
 
Nashukuru sana watalaamu
....wala sina nia ya kufanya uhalifu wowote me raia mwema tu ila kuhide IP address ni moja ya njia za kuwa salama mtandaoni ndo maana nlitaka nijue Ahsanteni sana
 
Ads zinatumia njia nyingi kukugundua wewe ni nani moja wapo ikiwa ni cookies, cookie ni file ambalo linahifadhiwa kwenye machine yako ukitembelea site mbalimbali kwa mfano ukiingia gmail wanaweka cookie kwenye machine yako, then ukienda JF forum wakawa wanaonyesha matangazo ya google (Adsense/admob) wataisoma ile cookie na kukujua wewe ni nani kisha ndo kukuonyesha matangazo.
Kama unatumia browser unaweza kufuta cookies kwa kuingia kwenye settings za browser na kufuta browsing data.
Pia unaweza kuinstall extensions kama uBlock Origin ambayo itazuia site kama JF zisiweze kuload matangazo ya google na hivyo kupunguza uwezo wao wa kukutrack online unafanya nini.

Kwenye Apps za simu hii ni ngumu zaidi maana App inaweza kuacess identifier ambayo iko ndani ya simu yako kama IMEI na hivyo kukujua wewe ni nani hata kama unatumia VPN na hakuna njia rahisi ya kuzuia hili bila kutegemea simu yako imeundwa vipi.

VPN inaficha IP yako na muhimu zaidi inaficha mawasiliano yako (Encrypt) mtu yoyote wa katikati (ISP,serikali etc) asiweze kujua site unazoenda na taarifa unazotuma. Kuna VPN zinadai hawahifadhi logs kabisa, ila yupi wa kumwamini ndo shida.
 
Nilishawahi kujaribu kutumia VPN ya bure ya kudownload playstore, ilinipa IP addresses za Netherlands na UK, but the funny thing was, ads kwenye browser zilikuwa zinakuja za bongo, sasa swali, inakuaje nipate ads za kibongo wakati nipo Uholanzi au UK? Au IP address kubadilishwa hivyo ni kwa ajili gani? Naomba elimu hapo watalaamu
Browser nyingi zinakuwa zinatumia webRTC ambayo ina enable real time communications ambazo huitaji real IP address hvo basi kama Kuna website unatembelea ambayo inatumia webRTC API kama YouTube lazma itajua IP address yako whether una VPN au la
 
Kuna kitu kinaitwa Virtual Private Network.. naomba kuelimishwa ni kitu gani na kinafanya kazi vipi?
 
hii ni network ambayo huficha adress ya mtu pindi anapokuwa mtandaoni mfano wewe uko tanzania lakini ukifanya installation ya VPN utapata options ya kuchagua location mfano US
 
Habari zenu wadau,mi nina wazo (pengine ntakuwa nakosea maana sijabobea kwenye mambo ya IT).
Kwa mfano mtu ukiwa na blog na tuseme google adsense (pengine na mitandao mingine kama ipo) wanakulipa kulingana na watazamaji watakavyokuwa wengi kwenye blog au website yako,sasa je siwezi kufanya tricks za kuwa nabadilisha address na kisha kutembelea mwenyewe hizo page huku niki-count au kupata viewers wengi wakati ni mimi mwenyewe? naomba msaada wenu wataalamu.
c.c chief mkwawa,njunwa wamavoko
 
At one point in time Google watakukamata na utajutia account yako yako ya adsense!
Kipindi ukiwa na mawazo kama haya kuna wanadamu wengine mamillion wanajaribu kufanya huo uhuni tena unfortunately kwa kutumia zile zile VPN common hivo hata google inawawia rahisi kujua uhuni huu!
 
Back
Top Bottom