Ficha IP Adress yako kwa kutumia VPN (Android users)

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
31,918
63,915
Habari wadau, ngoja niende moja kwa moja kwenye mada.

IP Adress (Internet Protocol) ni anwani ambayo device mfano simu au computer inakua nayo pindi inapokua imeunganishwa na intaneti hivyo mtu mwingine kuweza kujua mmiliki wa hiko kifaa ni nani.
VPN (Virtual Private Network) ni simulator ambayo itafanya IP adress yako isijulikane uhalisi wake haswa ni wapi.

Muda gani wa Kutumia VPN?
Unaweza kutumia vpn muda wowote utakaohisi faragha yako inaingiliwa, lakini mara nyingi VPN hua tunatumia tukiwa tunataka access na huduma ambazo ili nizipate inabidi niwe nchi fulani (hili ndiyo lengo la huu uzi). Mfano Netflix inasapoti baadhi ya nchi ukiwa na VPN unaweza kuonesha upo Marekani na ukaaccess Netflix vizuri tu.

Binafsi hua natumia kupakua vitabu ambavyo hua vinatolewa bure kwa nchi fulani tu.

Jinsi ya Kuiseti VPN Yako
Apps mbili ambazo zinaaminika katika kutoa huduma ya VPN ni Tunnel Bear na Express VPN hizi zinasapoti kila platform i.e windows, android, Mac, ios.
Isipokua Tunnel Bear haisapoti kwenye Linux

Kwa watumiaji wa Android; (Tutatumia Express vpn)
1: Utaingia playstore utaenda eneo la kusearch na kuandika 'tunnel bear' au 'express vpn' (bila hizo alama). Utainstall mojawapo ya hiyo uliyochagua.

1481745289931.png



2: Ukishainstall utakua unaifungua nayo itakupa option ya kuchagua uwe unaonekana uko nchi gani. Utachagua nchi unayotaka.

1481745318235.png


3: Utaoneshwa kua imekubali hapo unakua umeshatengeneza VPN yako.


1481745357329.png



4: Enjoy Netflix.

N.B.
Hizo huduma zote ni in app purchase, utatakiwa kununua ili kuwa upgraded, Express vpn itakupa siku saba za free trial ila Tunnel Bear haikuwahi kunipa ultimatum ya kuupgrade.

Zinahitaji ujiunge kwa email kabla hujaaccess zaidi.
 
Mkuu nikitaka kujua IP Adress yangu inakuaje..??
Kuna njia mbili kutegemea na muda huo unatumia either wifi au bando la mobile.
Kama unatumia wifi
>Nenda kwenye settings

>Kwenye ribon ya connectivity ingia kwenye wifi.

>Kisha wifi settings.

>Chagua wifi ambayo unaitumia kwa muda huo kisha iclick itakuonesha signal strength, security na IP Adress

Kama hutumii wifi kuna mitandao ukiingia unatajiwa IP Adress yako mfano whatip.com
Au hata ukigoogle unaweza kuiona mfano ukiandika my ip address ukisearch unaletewa ip address yako.
 
Hapa ni kama kuna kaharufu ka usalama kiaina kwa hizi apps, nangoja mrejesho kwanza kabla nisijekuwa najichomesha mwenyewe na kuwarahisishia kazi jamaa zangu.
 
Hapa ni kama kuna kaharufu ka usalama kiaina kwa hizi apps, nangoja mrejesho kwanza kabla nisijekuwa najichomesha mwenyewe na kuwarahisishia kazi jamaa zangu
Hahahahahahaha siwezi kuwachoma ndugu zangu bwana. Mimi nimetumia sana Tunnel Bear kwa ajili ya kupakua vitabu ambavyo watu waliopo Marekani ndiyo wangeweza kupakua.
 
Hapa ni kama kuna kaharufu ka usalama kiaina kwa hizi apps, nangoja mrejesho kwanza kabla nisijekuwa najichomesha mwenyewe na kuwarahisishia kazi jamaa zangu
Mkuu katika vpn hakuna longo longo. Kama mtoa mada alivyo sema kuwa yeye anaitumiaje VPN.
Itumie kwa faida na sio kwa hasara.
 
Mimi ninataka kudownload YouTube music vipi naweza fanikiwa maana haipos supported Tanzania.
 
Free VPN zipo nyingi tu kwanini uone ni hizo mbili tu?
Katika hizo mbili zilipofanyiwa review hiyo express VPN iligewa asilima 96 kwa mia na tunnel bear asilimia 78 kwa mia, pia urahisi wake umenisukuma kuzitumia hizi.

Mkuu unatumia ipi?
 
Hahahahahahaha siwezi kuwachoma ndugu zangu bwana. Mimi nimetumia sana Tunnel Bear kwa ajili ya kupakua vitabu ambavyo watu waliopo Marekani ndiyo wangeweza kupakua.
Asante mkuu kwa mada yako swafiii kabisa naomba kufaham mitandao ipi unatumia kupata vitabu maana natafuta vitabu vya mifungo ni adimu sana kupata Asante
 
Asante mkuu kwa mada yako swafiii kabisa naomba kufaham mitandao ipi unatumia kupata vitabu maana natafuta vitabu vya mifungo ni adimu sana kupata Asante
Kabla hujalazimika mpaka kutumia vpn jaribu kwanza bookboon.com na wenyewe wako vizuri pia.
 
Katika hizo mbili zilipofanyiwa review hiyo express vpn iligewa asilima 96 kwa mia na tunnel bear asilimia 78 kwa mia, pia urahisi wake umenisukuma kuzitumia hizi.

Mkuu unatumia ipi?
Nitumie vpn ya nini? Huyo unayemuhofia kuijua IP Adress yako ana jinsia gani?
 
Back
Top Bottom