Nadhani imefika muda mashabiki tumeanza kua na unrealistic expectations. Tunategemea kushinda kila mechi, as if team nyingine hazina watu wenye akili.
We have a very thin squad with no proper substitutions, na hao wachezaji wazuri wanaoanza kila siku tayari wamekumbwa na fatigue. Joules Kounde amecheza mechi zote msimu huu za club na team ya taifa kwa dakika tisini. Pedri amepumzika mechi sio zaidi ya mbili, same to Yamal. Dani Olmo ni very injury prone, na ametoka kuuguza majeraha juzi tu. Kutegemea hawa watu waendelee kucheza kila siku, na kwa ubora uleule ni kuwaonea.
SIo rahisi kupambania treble kwa hiki kikosi finyu tulichonacho. Hapa tunaenda kucheza mechi 5 mfululizo ndani ya siku 15. Ndani ya hizo mechi tano, kuna Inter mara mbili, na Madrid mara mbili. Kufanya rotation hakuepukiki.
Mimi kwa sasa sidhani kama tutashinda treble. Tukishinda Laliga na Copa del Rey, kwangu itakua mafanikio tosha. Hii team imetoka mbali. Transfer market ikifunguliwa, tuongeze wachezaji, tuwe na kikosi kipana, ndio tupambanie treble!