Mobodro na hawa Burma TV wote wanatoa Huduma sawa. Wote wanaonyesha soka via live streaming. Ni sawa useme vodacom na Tigo. Hivyo haipatikani katika mobodro.
Barca kuna walinzi wanne(Jordi Alba, Samuel Umtiti, Clement Lenglet, Tomas Verlmaelen)wanaotumia mguu wa kushoto. Mechi kama ya jana baada ya Pique kucheza namba mbili walinzi wa katikati wote wawili walikua wanatumia mguu mmoja tu kitu ambacho sio afya sana na jana kulikua na makosa madogo madogo mengi yaliyotokana na beki kukatika japo hayakuleta madhara kwa sababu ya kipa. Bado naamini tulikosea kumuuza Mina anaetumia miguu yote na anaejua kuruka vichwa.