We color footbal ndio theme ya barcelona -Mosaic ya siku ya El classico inajieleza -post match analysis
Kama tulivyokatabiri Barca fans ,Julien Lupetegue atafukuzwa mapema kabla ya Mourinho imeshatokea... labda tuwakumbushe madrid fans ambao ni short memory baada ya Barcelona kuinywesha goli 4-0 Madrid 2015 ,November 21 rafel banitez alifukuzwa.. ndio Zidane aka take over ,turudi kwenye mada
First half ya game Velverde kama kawaida aliamini aki concentrate forces kwenye upande wa kushoto tuta win...,hii style inatumika na contegency plan ya Jordi Alba (for me is the best in the world LB kwa sasa hivi) ya ku overlap kama winger mwenye speed kali ,tuliona matunda..,Nacho baada ya kuwa defender aligeuzwa na kua mkimbizaji na matunda yake yalizaa magoli mawili .Hii style Jordi Alba anapanda juu kidogo kwenye line moja na midfielders Arthur,Rakitic na Busquets kwenye nusu ya kushoto mwa uwanja ,huku wakiwa wanagongeana passes za ku penetrate na ku hold wakiwa makini ku exploit spaces zinazoachwa na adui meanwhile ,lenglet kama central defender anasogea space aliyoiacha Jordi Alba (anaiziba kama LB) at the same time first line attackers (coutinho,Suarez na Rafinha ) wana collapse kwa kuja katikati lakini stricker anabakia kwenye position yake (suarez) ,but rafinha ambaye alicheza fake right winger(namba 7) anaongezeka upande ule ule wa kushoto kama free player hii style inawajaza wachezaji wengi upande wa kushoto mwa dimba.
Muda huo huo inaleta balance ya ku absorb surprise attacks kutoka kwa opponent in case mkiwa dispossessed na mpira -mkishambuliwa (Lenglet atazuia,midfielders zitakufukuza adui pia na mtu wa mwisho anakua beki 5 na namba mbili RB) na advantage nyingine yule free player Rafinha ata collapse hadi kuja ku defend mipira pia .Mkifanikisha kupenyeza mipira ni either LB atapiga crosses katikati ambako mtakua wengi na ku score au watu wa katikati wanapenyeza mipira huku wakipasiana na kusababisha madhara golini kwa adui na option nyingine mpira utahamishwa upande na kwenda kulia ambako adui anakua ameacha spaces kibao kitu ambacho kitamchanganya na kumsababishia madhara -Hii ni alternative ya kwanza ambayo kipindi cha kwanza iliwaumiza Madrid.. hata ukiangali mipira mingi ilitokea kushoto kwa uwanja (left flank)
kipindi cha pili Velverde alitumia combinations ambayo kidogo Lupetegui ali anticipate kwa kumuingiza Vasquez ,lengo lilikua nini?alijua wakati Barcelona wanashambulia pamoja na kwamba kunakua na contigency plan lakini in reality space ya LB bado inakua wazi sema inazuiwa tu namba hivyo basi akiweza kui exploit speed na crosses(outers) Vasquez ataweza kupiga mipira mirefu katikati ili aweze kufunga na moya ya weakness yetu alikua anaijua kidogo mara nyingi mipira ya juu ya crosses inatuumizaga na kufungwa unexpected goals ;Tofauti na kipindi cha kwanza Madrid walibadilisha mashambulizi kwa kutumia kushoto kwetu ambako waliona ndio weak tofauti na mwanzo ambako walitumia kulia kwa S.Roberto ,walifanikisha kupata goli na walifanikiwa kukaa na mipira pia ...na goli la zao la cross za dogo vasquez ,lakini kama ilivyo kawaida ya elite players wa Barca(Barcelona unapohamishiwa pale unapimwa IQ pia) wakabadilisha pattern wakawa wanacheza mipira sana katikati na right flank (Ivan rakitic ,Busquets asikuambie mtu hawa watu wana IQ ya hali ya juu sana -usiwaone wapole ) ,ilimlazimu Suarez kushuka katikati sasa ,Jordi akaacha ku overlap ikawa game ya ku win katikati ya dimba ... ndio maana ukienda kumuuliza Tony Kros na Modric taja jina Arthur Melo... wanaweza wakakimbia it was a nightmare with about 96% passes accuracy ,hapa aliekua ana overlap sasa akawa S.Roberto....(king of Ramontada )
.Kumbuka style ya mwanzo ilimfanya S.Roberto kuwa redundant kidogo alikua anaonekana ana defend sana (first half) ,ila hapa akawa anaonyesha vipaji vyake .. alikua ana dribble,anapiga crosses, anapiga penetrating passes kinyume chake Coutinho kule mbele kushoto akawa redundant (hatumiki sana) ,muda huo huo Madrid wakawa wanatumia mechanism ile ile ya mwanzo wanashambulia S.Roberto anapotoka na kushoto hakupitiki tena ,velverde akasema yap this is the time for substitution ,Semedo is so good kwenye ku defend ili azibe kabisa mianya against the weak team meanwhile S.Roberto akae kule kule juu afanye coordination ya mashambulizi... muda huo huo Coutinho kachoka nimuingize mtu ambaye ataleta pace za kukimbizana na vyenga vingi si mwingine ni the "cricitized" guy Dembele
Hakika vijana walifanya kazi waliyotumwa substitution kuanzia dakika ya 74 ilizaa goli tatu ,Artulo vidal dakika ya 79-80 aliingizwa tu ili alete balance kama pillars za team pale katikati hakufanya masihara nae pia alipata kutimiza ndoto yake ya kuifunga Madrid kutoka pass safi kabisa ya Othman Dembele
Overall opportunities :Tulitengeneza chances za kufunga 12 na tuliweza kufunga 05
My sketch :
Adieu....!!