Gazeti la michezo la ufaransa, France football magazine wamemwomba msamaha kiungo wa Barcelona na spain Andre Aniesta kwa kutompa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2010 ambayo ilichukuliwa na mchezaji mwenzake wa Barcelona Leonel Messi.
Iniesta ambaye aliisaidia Baca kupata vikombe vya laliga na UCL msimu wa 2009/2010 na kuiwezesha timu yake ya taifa Spain kunyakuwa kombe la dunia kwa kufunga goli la ushindi dhidi ya uholanzi alishika nafasi ya pili nyuma ya Messi na mbele ya Xavi Hernandez.
Gazeti hilo linasema tuzo hiyo alistahili Iniesta na si Messi kama ilivyotokea.
Tuzo ya mchezaji bora duniani hutolewa na gazeti la michezo la ufaransa la france football magazine.