FastJet: Mwanza - Kilimanjaro nauli tsh 32,000... (Bila VAT)

Kwa hesabu ya haraka haraka Nauli + VAT + 20kg ya mizigi itakuwa Tshs 45,760. Msosi utajiju. Sa masaa mawili au moja nalo unakula nini kama sio uroho tu!
 
kwani kutoka mwanza had arusha inachukua dakika ngapi hadi ubebe mavyakula? chakula unakula mwanza maji unaenda kunywa arusha. mia

ndege zifanyazo safari za ndani hwa hawagawi heavy meals, ila vyakula vidogo vidogo tu vya kupoteza muda na kuchangamsha mdomo...Arusha - Mwanza sijui huchukua muda gani, ila Mwanza - Dar ni kama saa moja na robo hadi unusu
 
kwa hesabu ya haraka haraka nauli + vat + 20kg ya mizigi itakuwa tshs 45,760. Msosi utajiju. Sa masaa mawili au moja nalo unakula nini kama sio uroho tu!
acheni ukauzu ,midomo si itanuka
 
Uongo tu huo ni usanii. Kwani wamekuja wangapi na mbwembwe hizo kumbe utapeli.hakuna biashara ya mama ntilia kwenye issue ya usafiri wa ndege. Duniani kote huwa ni ghali sasa huyu ati 32,000 Tsh ! hata ukaweka navat of 18% is unthinkable na uongo
wabongo tumezoea kunyonywa kweli
 
eheheeee na rubani mwenyewe ni wewe dah watakomaje
Unamaakili wewe mpaka natamani nikutoa hapa ka jf nikuhug member wote wakishuhudia. na hivi nishamaliza mafunzo ya urubani kitu mtoto Smile pembeni ....
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa nasikiliza afisa wao clouds fm asubuhi, anasema chakula ndani ya ndege ni cha kulipia ila unaruhusiwa kuingia na chakula chako ambacho hakitawaudhi abiria wenzanako. Mizigo nayo itakuwa inalipiwa; kilo ishirini za mwanzo ni shilingi elfu nane na kila kilo inayozidi ni shilingi elfu nane.

Kwahiyo Noah Marufuku??
 
kwani kutoka mwanza had arusha inachukua dakika ngapi hadi ubebe mavyakula? chakula unakula mwanza maji unaenda kunywa arusha. mia

kama unaenda mwanza lazima ndege isimame sehemu zifuatazo
chalinze:kununua korosho
saranda singida: kula kuku lunch
tabora :kununua asali na mawe ya sumu ya nyoka
mia
 
Hizo ndio ndege ambazo wanasema ni za bei rahisi
Sasa nnahisi kabisa kuwa humu ndani badala ya kupewa sandwich tutakuwa tunapewa UBUYU


Mkuu hii ni kama Ryan Air kwa Ulaya. Wao pia chakula unalipia pamoja na mizigo ila hand luggage nafikiri maximum kilo 8 ni bure. Wao pia ukitaka kuingia wa kwanza unalipia.
 
halafu Wi-Fi bei ya nauli ni 32,000Tshs sio 35,000Tshs kama ulivyobainisha kwenye heading....

Mabadiliko tuyakubali ndugu zangu, tusianze vikwazo hata safari moja haijaanza,wengine wanavutia wateja,mara watashindwa mnapata wapi uwoga?kwanini historia ndio yamekua maisha yenu?Wajaribu kwani kushindwa dhambi?Wakijipanga wataweza na kila raia aliekua akiota ayapandaje ndege atapata fursa ya kupanda.
Wataweza tu ondoeni hofu tuwatie moyo na kuwaunga mkono.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom