FastJet: Mwanza - Kilimanjaro nauli tsh 32,000... (Bila VAT)

Usafiri wa ndege unaweza kuwa rahisi hapa Tz kama kungekuwa na ndege nyingi kuleta ushindani. Lakini bei inakuwa kubwa kwa sababu ya kutokuwepo ushindani. Kumbukeni ile ndege ya akina Diallo ilikuwa 75000 MWZ - DAR lakini waliihujumu, sasa ni grounded!

Ile walijihujumu wenyewe baada ya sakata la Richmond kuibuka. Nakumbuka nilikuwa na ticket wiki hiyo ikabidi kusafiri na shirika lingine. Chezea Laigwanan wewe
 
Jamani naomben ukweli katika hii nami nipande ndege kidigo nitie baraka maisha yangu npo mwanza familia ipo dar
Hey, but muwe macho manake tatizo kubwa kwa jamaa wa budget airlines, wakati mwingine uamua kuskip services, kukwepa gharama, na kumaximize profit sasa hapo, du ni kuomba Mungu kwenye hizo trip wasiwe wanakwepa scheduled services za ndege zao! Anyway, good start!
 
acheni ukauzu ,midomo si itanuka

Acheni uroho wa msosi kwenye ndege. Kwani ukiwa kwenye daladala mfano Mbezi kwenda Posta ambapo wakati mwingine unaweza kutumia zaidi ya masaa mawili unakula chochote? Halafu dkk 50 tuu unataka upakie misosi??
Mimi nadhani ni bora ukaachana na chakula, ukiweza hata mamizigo ya zaidi ya kg20 ya nini kama ni safari ya kawaida na sio kuhamia? Big up kwa hilo kampuni, walau tunaona mwelekeo wa kupumua nauli za ndege.
 
Safi sana kumbe ruksa kubeba kande, mihogo, ulanzi, mbege, rubisi mbona raha
 
Kwenye hizo ndege tusishangae kukutana na jamaa kama wanaopandiaga Chalinze na mabox yao ya juice na biskuti na ili kumaximise profit inaweza ikawa inajaza kama treni ya Mwakyembe
 
Kwa hesabu ya haraka haraka Nauli + VAT + 20kg ya mizigi itakuwa Tshs 45,760. Msosi utajiju. Sa masaa mawili au moja nalo unakula nini kama sio uroho tu!

umesema ukweli,uroho tu!!unapanda na pipi Toffie tu inatosha!!!mbona tunakaa kwenye foleni masaa 3 hata karanga watu hatununui na zinapitishwa dirishani?waweke tu magazeti inatosha
 
Jamani sidhani kama sheria za usafiri wa anga unaruhusu mtu kupanda na chakula ndani ya ndege
 
Mimi nawapa BIG up sana hawa Fast jet
Kuhusu kula safarini sioni kama kuna umuhimu wowote hapa. Safari ya ndege ndogo kama C404 (caravan ya watu 12) au C408 - inatumia masaa mawili tu (Dar/JRO) ndege kubwa inatumia around saa moja na nusu TUUUUU??? unahitaji kula nini??? Labda kwa wale wenye matatizo..... naamini pipi zitakuwepo kwa ajili yao!!!
 
Hii ni kampuni mpya inayoanza safari za ndege, nauli ni bila VAT.

Kwa Dar office zipo mitaa ya Samora opp Wizara ya Nishati na madini karibu na Steers.
Ninavyojua mimi, ni kuwa hakuna VAT kwenye usafiri wa umma (basi, treni, ndege etc). So, kama wamesema nauli ni TZS 32K, basi ni hiyo pekee na haiwezi kuwa na VAT....labda kama alikuwa anamaanisha "airport tax" ambayo mara nyingi ni nominal amount (ilikuwa elfu tano lakini kuanzia 1st July 2012 ni elfu kumi kwa safari za ndani)
 
Usafiri wa ndege unaweza kuwa rahisi hapa Tz kama kungekuwa na ndege nyingi kuleta ushindani. Lakini bei inakuwa kubwa kwa sababu ya kutokuwepo ushindani. Kumbukeni ile ndege ya akina Diallo ilikuwa 75000 MWZ - DAR lakini waliihujumu, sasa ni grounded!

Mkuu na hawa wawe makini sana, wanaweza kufanyiwa hujuma; kuna shirika moja linaonekana limejizatiti kuteka usafiri wa hanga nchini, tusipo kuwa wangalifu ATC itabaki kuwa historia.
 
umesema ukweli,uroho tu!!unapanda na pipi Toffie tu inatosha!!!mbona tunakaa kwenye foleni masaa 3 hata karanga watu hatununui na zinapitishwa dirishani?waweke tu magazeti inatosha
Tena waswahili wengi wakiwekewa magazeti ya udaku dah itakuwa burudani kwao
 
Ninavyojua mimi, ni kuwa hakuna VAT kwenye usafiri wa umma (basi, treni, ndege etc). So, kama wamesema nauli ni TZS 32K, basi ni hiyo pekee na haiwezi kuwa na VAT....labda kama alikuwa anamaanisha "airport tax" ambayo mara nyingi ni nominal amount (kama elfu tano au sita hivi kwa safari za ndani)

Hapo kwenye bold, nauli zimepanda kuanzia mwaka huu wa bajeti. Kwa wasafiri wa ndani ya nchi ni 10,000
 
  • Thanks
Reactions: SMU
madogo wa boarding wakifunga shule,ndege itapigwa machata hiyooo......itabidi waweke migambo huku ndani,waTZ hawachelewi kuiba mapazia humo
 
32,000 inaweza kua nauli ya mwenye ndege tu, kodi hua ni Airport tax na bima pia. Msishangae zikafika mpaka 80,000 na Mizigo
 
Back
Top Bottom