Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Sina cha kusema, maneno yamenikauka. Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi, tulikuwa bado tunakuhitaji bt Mungu ameona ni vema upumzike. We will miss you Regia. Pumzika kwa amani dada!!
 
Farewell my Lady Regia Mtema, sina la kuzungumza wala sina nguvu ya kusoma na kuchangia mada hii na zote zinazohusiana na Mpambanaji..mtanisamehe, inaniweka ktk mtihani mkubwa sana..
- Maasalaaam!
 
Niliposikia sikuamini, lakini wanamageuzi hatuna budi kukubaliuana na matokeo haya ya kuumiza sana lakini tusikate tamaa, tawi moja la mti linapokatwa hutoa nafasi kwa matawi mengine mengi kuchipua na hilo ndilo litakalotokea kwa wanamageuzi.. Natoa pole kwa wanafamilia na uongozi wa chama kwa ujumla..
 
Niliposikia sikuamini, lakini wanamageuzi hatuna budi kukubaliuana na matokeo haya ya kuumiza sana lakini tusikate tamaa, tawi moja la mti linapokatwa hutoa nafasi kwa matawi mengine mengi kuchipua na hilo ndilo litakalotokea kwa wanamageuzi.. Natoa pole kwa wanafamilia na uongozi wa chama kwa ujumla..
Fred loong tyme Kaka upo???
 
RIP GS Regia,
kwa kweli ulikuwa unahitajika, lakini Mwenyezi MUngu alikuitaji zaidi
 
Namlilia Regia,
Alitamani kuiona Tanzania ikiwa bora zaidi na ambayo watu wake wanafurahia matunda ya nchi yao kwa haki, usawa na umoja. Tunaposema alikuwa ni mwanaharakati hatutii chumvi. Wengi tumeshuhudia jinsi ambavyo amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa ambao wamekomazwa kwenye mitandao hii. Amekuwa jasiri kuliko wanasiasa wengi wakongwe kuja na kupitishwa kwenye tanuru la maoni ya JF na kila wakati ambapo ulifikiria kuwa labda amekwazika na hatorudi tena Regia alirudi na alirudi akiwa mpya kabisa. Aliweza kusimama katika moto bila kuungua na kama aliungua haikuwa rahisi kujua!MMM
Nipo safarini, nasikia habari hizi mwili unapigwa na ganzi. Nyota imezimika!!

Wiki chache zilizopita aliweka uzi wake wa yale aliyoyafanya mwaka mzima. Wengi tulisema sasa tunaona wabunge wa wananchi. Alieza kile mola alichomjalia, kumbe alikuwa anatuaga! Loh!
Ni kama alikuwa anasema nawaachieni majukumu ya taifa, yeye alifanya alichokiweza.

MM amesema mengi kuhusu wasifu wake, naongezea kuwa alikuwa ni kiungo muhimu sana katika taifa hili. Hali yake ya maumbile haikumzuia kufanya kile alichotakiwa kukifanya na taifa. Alizunguka huku na huko kuiangalia Tanzania.

Nakumbuka aliweka uzi kuhusu aliyoyaona Singida kwa uchungu na hisia sana.
Kwa umri wake Regia ali accomplish mengi kupita matarajio. Alikuwa na mengi lakini Mola ndiye mangaji.

Ni simamzi na majonzi.

Namlilia Regia, Mwenyezi mungu mpuzishe kwa amani
 
RIP Regia Mtema,Sisi tulikupenda Mungu amekupenda zaidi.
 
Hofu yangu kubwa ni marehemu Regia kusahaulika mapema tu katika siasa na maisha. Tufanyeje ili tuendelee kumtajataja mara kwa mara? Sijasikia kama kaacha mtoto; CHADEMA sijasikia watamuenzi vipi; BUNGE letu lina kumbi nyingi tu ndani ya ule mjengo, angalau kaukumbi kamojawapo kaitwe kwa jina lake. Huko kwao Kilombero sidhani kama watapata shida kumuwekea kumbukumbu sahihi na ya kudumu. Humu JF akina Invisible watajua wafanyeje ili tubaki nae Regia angalau kwa miaka miwili mitatu. Ameanzisha thread nyingi humu. Mimi naye tulibishana kidogo kwenye ile ya baada ya uchaguzi mdogo wa Igunga. Hakuwa sahihi mara zote lakini alikuwa sahihi mara nyingi sana.
Umati ule wa jana pale msibani ni ishara tosha kuwa Regia alikubalika sana.
 
Napenda kuchukua nafasi hii nikiwa mjumbe wa H/kuu ya CCM wilaya ya ilala kuwapa pole Viongozi,wanachama na wapenzi wa Chadema kwa msiba wa Mbunge wao wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe R.Mtema,Mwenyezi mungu awpe nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Ahsante Magamba.
 
Shemeji Regia,
Kutoka rohoni kwangu na kwa niaba ya familia yangu, shemeji yangu Regia Mungu akupe faraja ya moyoni
popote ulipo kwa kulala salama,
 
Regia, inakuwa vigumu mno kuamini kuwa hauko nasi tena!
Hatutakuona hadi mwisho wa maisha yetu!..
Mungu amempenda zaidi....kwani alikuwa na uwezo wote wa kukuacha uishi!..

Huko uliko, mungu akupumzishe kwa amani....

Ukweli, tulikuwa tunakupenda sana, sana pendo l dhati............

Mwisho, ........basi bwana, machozi yananitoka, siwezi kuandika tena machozi yananitoka........
Baadae, ntakuandikia Regia dada, mbunge wangu, mpendwa wangu, lala pema pema huko uliko.....
 
Mungu wangu, ni juzi tu tarehe 10 January aliweka thread ya kukusanya maoni na kero za wananchi kupitia wana jf na mrejesho ulikuwa mzuri sana.
MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU REGIA MAHALA PEMA PEPONI. BWANA AMETOA BWANA AMETWAA KAZI YAKE HAINA MAKOSA.
 
JF has lost one of its greater thinker
JF will never be the same again
RIP Hon. Regia Mtema
 
Its too hard to take this, ingekuwa ninaweza tungebadili hili lakini Bwana ndiye alitoa kilicho chema na Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe, farewell my loving sister! miss you always
Mama Joe
 
Dada yetu mpendwa pumzika kwa amani huko uliko!
 
Back
Top Bottom