BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,847
Hapendwi mtu bila kuifanyia mikataba yote ya madini marekebisho au kuiandika upya mikataba hiyo.
Serikali sasa yaweka wazi faida ya Buzwagi
Mwandishi Wetu
HabariLeo; Tuesday,October 02, 2007 @00:02
SERIKALI imesema mkataba wa Buzwagi umeboreshwa kwa masilahi ya taifa ikilinganisha na mikataba ya zamani ya madini, na kutaja faida za mradi huo wa uchimbaji dhahabu. Kutokana na hali hiyo, Serikali imesema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuwa katika kusaini mkataba wa Buzwagi, sheria na taratibu za nchi zilikiukwa, si za kweli na zina lengo la kuupotosha umma.
Taarifa ya Serikali iliyotolewa Dar es Salaam jana, ilisema mkataba wa Buzwagi uliandaliwa Tanzania na wataalamu wa hapa nchini na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini. Serikali ilieleza kuwa wataalamu waliohusika katika mchakato wa majadiliano ya mkataba huo na Kamati ya Ushauri ya madini iliyoupitisha, wote ni wazalendo na wakati wote walihakikisha masilahi ya nchi yanawekwa mbele.
Kulinganisha na mikataba mingine iliyotangulia, mkataba huo wa Buzwagi unavyo vipengele vilivyoboreshwa zaidi, ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Vipengele ambavyo vimetajwa na serikali kuwa vimeboreshwa ni kupungua kwa asilimia 80 kwa mwaka wa kwanza na asilimia 50 miaka inayofuata; Kodi za zuio kwa kazi za kitaalamu kuongezeka kutoka asilimia tatu hadi kufikia asilimia tano.
Eneo jingine ni kodi za zuio kwa gharama za utawala kuongezeka kutoka asilimia tatu hadi asilimia 15; Masharti ya kununua bidhaa na huduma mbalimbali nchini; na kuchangia mfuko wa uwezeshaji dola za Marekani 125,000 kwa mwaka.
Serikali pia imesema ujenzi wa mgodi utakapokamilika na uzalishaji kuanza rasmi inatarajiwa kwamba miaka 10 ya kwanza ya uendeshaji wa mradi huo utakuwa na faida nyingi, ikiwamo mrahaba na kodi nyingine zinatarajiwa kufikia dola za Marekani milioni 198.8. Faida nyingine zilizotajwa na serikali ni ajira kwa Watanzania 696 wa fani mbalimbali; kodi zinazotokana na mishahara ya wafanyakazi (PAYE) dola za Marekani milioni 50.3 na ujenzi wa laini ya umeme utakaogharimu dola za Marekani milioni 30.
Laini hii itawezesha upatikanaji wa nishati ya umeme ambayo ni pamoja na maeneo ya mji wa Kahama, vijiji vya Mwine, Chapulwa, Mwendakulima, Sangiwa, ilisema taarifa hiyo na kutaja faida nyingine kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya uchumi na jamii kama vile shule na zahanati katika maeneo yanayozunguka mgodi.
Hivi karibuni pamejitokeza baadhi ya wanasiasa hususan kutoka vyama vya upinzani kutoa matamshi hadharani, kuwatuhumu viongozi kadhaa wa umma walioko madarakani sasa au awamu zilizopita kuwa walikiuka taratibu au kuvunja sheria kwa kusaini mikataba ya madini, ilisema taarifa hiyo. Serikali ilisema viongozi hao wamejaribu kupotosha umma juu ya tafsiri sahihi za sheria inayoongoza mikataba hii.
Vile vile kuna jitihada za makusudi za kuuhadaa umma kwamba kusainiwa mkataba wa Buzwagi kulikiuka taratibu na sheria za nchi, ilisema taarifa hiyo. Katika kuwaelimisha wananchi, serikali imeelezea mchakato wa mkataba huo kwa kueleza kuwa mikataba ya uendelezaji wa madini ya mwaka 1998 inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya madini kuingia makubaliano na mmiliki au muombaji wa leseni kubwa ya uchimbaji madini.
Taarifa ilisema kwa mujibu wa kifungu hicho, Waziri hutakiwa kupata ushauri wa Kamati ya Ushauri ya Madini kabla ya kusaini mkataba. Kampuni tanzu ya Barrick iitwayo Pangea Minerals ilipatiwa leseni ya utafutaji wa madini katika eneo la Buzwagi wilayani Kahama, Shinyanga kuanzia mwaka 2003.
Baada ya utafiti wa miaka takriban mitatu, kampuni ya Pangea Minerals iliwasilisha maombi yake serikalini ili kuingia mkataba wa uendelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini katika eneo hilo. Maombi hayo yaliambatanishwa na upembuzi yakinifu wa mradi huo. Timu ya wataalamu wa serikali ilianza majadiliano na kampuni ya Pangea Minerals kuanzia Mei mwaka jana kwa nia ya kuingia katika mkataba. Kufikia Februari 16 mwaka huu, taratibu zote za kisheria kwa ajili ya kusaini mkataba huo zilikuwa zimekwisha kukamilika na hatimaye mkataba huo kutiwa saini Februari 17 mwaka huu.
Katika hatua nyingine, malumbano juu ya suala la ufisadi na rushwa yanaweza yakafikia kiwango cha kuleta mafarakano na uhasama katika jamii yakizidi kiasi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jaji Mstaafu Mark Bomani alisema kutokana na malumbano ya ufisadi yanayotokea kwa sasa, vitendo vya rushwa na ufisadi ni lazima vipigwe vita kwa nguvu zote, lakini sheria za kutuwezesha kufanya hivyo na sababu za kufanya hivyo vipo, kinachotakiwa ni utashi wa kufanya jambo hilo.
Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved