Faida ya Buzwagi ni hii: Serikali

Je huu mkataba wa Buzwagi uliandaliwa Danmark kama alivyoomba JK alipokuwa kwenye ziara ya kule? Kama Wanadish ndo waliotuandalia basi afadhali tuendelee kuyakalia madini yetu.
 
Hebu niuliuze swali la kijinga: hivi kama Karamagi asingesaini ule mkataba London Tanzania tungepata hasara gani?
 
Leo nimeshinda na wasi wasi sana maana tangia balaa la Buzwagi na matamko ya Serikali kuwa mengi mno na yanapishana na kulazimisha watu kukubali wayasemayo wao , najiuliza hata kama Usalama wa Taifa hili upo. Maana mikataba pekee mambo ni haya je Tanzania kama Nchi ni salama kiasi gani ?Wamemwita Zitto muongo lakini tumeshuhudia uongo wa wabunge wa CCM wakiwamo mawaziri mara nyingi . Mfano wa last Budget session hata mambo ta vivuko yalisemwa kwamba ni safi lakini juzi moto umewaka Ukerewe mbele ya waziri Mkuu na Chenge , Walisema maji Tanzania nzima yanaenea kwa asilimia 70 lakini Dar pekee hakuna maji, barabara wakasema zimetapakaa kila kona ingia Dar pekee utajionea.Lakini wao kila siku ni hadithi na kupigiana makofi. Inatisha hii jamani
 
The government says that the contract was prepared in Tanzania, and by Tanzanians. That is interesting! Why was a contract that was prepared in Tanzania by Tanzanian experts taken to London to be signed by a Tanzanian Minister in a hotel? That is what the government should have elaborated on.

We care about what is in the contract rather than who prepared it. People can be bought. Why is the government unwilling to let our MPs see the contract? Why is the contract a secret?

One can't help laughing when one sees what the government puts forward as the goodness of the contract. The Miner will contribute to the government empowerment fund $125,000 per annum. That is peanuts! The operation will take away from us more than $125 million per annum! The government says the miner will pay tax on 20% of his expenses. Why should he not pay tax on 100% of his costs as we all do?

We want one thing and one thing only: let our representatives debate and agree or reject each contract proposal before it is signed. Why is the government so vehemently opposed to this? Why should the people not have the right to vet how their inheritance is sold off?
 
Mkuu Moshi hapo ni kweli kabisa ulichoongea lakini huoni kama kila mkataba kujadiliwa na wabunge wote itakuwa kama ni chaos na mwanzo wa rushwa na upendeleo usio na maana...nafikiri nchi yeyote inayoheshimu utawala wa sheria huwa ina guidelines zake za mikataba inayoingia ambayo ni kama law of the land.
 
Serikali pia imesema ujenzi wa mgodi utakapokamilika na uzalishaji kuanza rasmi inatarajiwa kwamba miaka 10 ya kwanza ya uendeshaji wa mradi huo utakuwa na faida nyingi, ikiwamo mrahaba na kodi nyingine zinatarajiwa kufikia dola za Marekani milioni 198.8. Faida nyingine zilizotajwa na serikali ni ajira kwa Watanzania 696 wa fani mbalimbali; kodi zinazotokana na mishahara ya wafanyakazi (PAYE) dola za Marekani milioni 50.3 na ujenzi wa laini ya umeme utakaogharimu dola za Marekani milioni 30.
======
Kwa miaka kumi ,Tanzania tulitakiwa kupata USdollar198.8 million .
 
Leo nimeshinda na wasi wasi sana maana tangia balaa la Buzwagi na matamko ya Serikali kuwa mengi mno na yanapishana na kulazimisha watu kukubali wayasemayo wao , najiuliza hata kama Usalama wa Taifa hili upo. Maana mikataba pekee mambo ni haya je Tanzania kama Nchi ni salama kiasi gani ?Wamemwita Zitto muongo lakini tumeshuhudia uongo wa wabunge wa CCM wakiwamo mawaziri mara nyingi . Mfano wa last Budget session hata mambo ta vivuko yalisemwa kwamba ni safi lakini juzi moto umewaka Ukerewe mbele ya waziri Mkuu na Chenge , Walisema maji Tanzania nzima yanaenea kwa asilimia 70 lakini Dar pekee hakuna maji, barabara wakasema zimetapakaa kila kona ingia Dar pekee utajionea.Lakini wao kila siku ni hadithi na kupigiana makofi. Inatisha hii jamani
Tumeshajua nani mnafiki
 
Hapendwi mtu bila kuifanyia mikataba yote ya madini marekebisho au kuiandika upya mikataba hiyo.

Serikali sasa yaweka wazi faida ya Buzwagi
Mwandishi Wetu
HabariLeo; Tuesday,October 02, 2007 @00:02

SERIKALI imesema mkataba wa Buzwagi umeboreshwa kwa masilahi ya taifa ikilinganisha na mikataba ya zamani ya madini, na kutaja faida za mradi huo wa uchimbaji dhahabu. Kutokana na hali hiyo, Serikali imesema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuwa katika kusaini mkataba wa Buzwagi, sheria na taratibu za nchi zilikiukwa, si za kweli na zina lengo la kuupotosha umma.

Taarifa ya Serikali iliyotolewa Dar es Salaam jana, ilisema mkataba wa Buzwagi uliandaliwa Tanzania na wataalamu wa hapa nchini na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini. Serikali ilieleza kuwa wataalamu waliohusika katika mchakato wa majadiliano ya mkataba huo na Kamati ya Ushauri ya madini iliyoupitisha, wote ni wazalendo na wakati wote walihakikisha masilahi ya nchi yanawekwa mbele.

“Kulinganisha na mikataba mingine iliyotangulia, mkataba huo wa Buzwagi unavyo vipengele vilivyoboreshwa zaidi,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Vipengele ambavyo vimetajwa na serikali kuwa vimeboreshwa ni kupungua kwa asilimia 80 kwa mwaka wa kwanza na asilimia 50 miaka inayofuata; Kodi za zuio kwa kazi za kitaalamu kuongezeka kutoka asilimia tatu hadi kufikia asilimia tano.

Eneo jingine ni kodi za zuio kwa gharama za utawala kuongezeka kutoka asilimia tatu hadi asilimia 15; Masharti ya kununua bidhaa na huduma mbalimbali nchini; na kuchangia mfuko wa uwezeshaji dola za Marekani 125,000 kwa mwaka.

Serikali pia imesema ujenzi wa mgodi utakapokamilika na uzalishaji kuanza rasmi inatarajiwa kwamba miaka 10 ya kwanza ya uendeshaji wa mradi huo utakuwa na faida nyingi, ikiwamo mrahaba na kodi nyingine zinatarajiwa kufikia dola za Marekani milioni 198.8. Faida nyingine zilizotajwa na serikali ni ajira kwa Watanzania 696 wa fani mbalimbali; kodi zinazotokana na mishahara ya wafanyakazi (PAYE) dola za Marekani milioni 50.3 na ujenzi wa laini ya umeme utakaogharimu dola za Marekani milioni 30.

“Laini hii itawezesha upatikanaji wa nishati ya umeme ambayo ni pamoja na maeneo ya mji wa Kahama, vijiji vya Mwine, Chapulwa, Mwendakulima, Sangiwa,” ilisema taarifa hiyo na kutaja faida nyingine kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya uchumi na jamii kama vile shule na zahanati katika maeneo yanayozunguka mgodi.

“Hivi karibuni pamejitokeza baadhi ya wanasiasa hususan kutoka vyama vya upinzani kutoa matamshi hadharani, kuwatuhumu viongozi kadhaa wa umma walioko madarakani sasa au awamu zilizopita kuwa walikiuka taratibu au kuvunja sheria kwa kusaini mikataba ya madini,” ilisema taarifa hiyo. Serikali ilisema viongozi hao wamejaribu kupotosha umma juu ya tafsiri sahihi za sheria inayoongoza mikataba hii.

Vile vile kuna jitihada za makusudi za kuuhadaa umma kwamba kusainiwa mkataba wa Buzwagi kulikiuka taratibu na sheria za nchi, ilisema taarifa hiyo. Katika kuwaelimisha wananchi, serikali imeelezea mchakato wa mkataba huo kwa kueleza kuwa mikataba ya uendelezaji wa madini ya mwaka 1998 inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya madini kuingia makubaliano na mmiliki au muombaji wa leseni kubwa ya uchimbaji madini.

Taarifa ilisema kwa mujibu wa kifungu hicho, Waziri hutakiwa kupata ushauri wa Kamati ya Ushauri ya Madini kabla ya kusaini mkataba. Kampuni tanzu ya Barrick iitwayo Pangea Minerals ilipatiwa leseni ya utafutaji wa madini katika eneo la Buzwagi wilayani Kahama, Shinyanga kuanzia mwaka 2003.

Baada ya utafiti wa miaka takriban mitatu, kampuni ya Pangea Minerals iliwasilisha maombi yake serikalini ili kuingia mkataba wa uendelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini katika eneo hilo. Maombi hayo yaliambatanishwa na upembuzi yakinifu wa mradi huo. Timu ya wataalamu wa serikali ilianza majadiliano na kampuni ya Pangea Minerals kuanzia Mei mwaka jana kwa nia ya kuingia katika mkataba. Kufikia Februari 16 mwaka huu, taratibu zote za kisheria kwa ajili ya kusaini mkataba huo zilikuwa zimekwisha kukamilika na hatimaye mkataba huo kutiwa saini Februari 17 mwaka huu.

Katika hatua nyingine, malumbano juu ya suala la ufisadi na rushwa yanaweza yakafikia kiwango cha kuleta mafarakano na uhasama katika jamii yakizidi kiasi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jaji Mstaafu Mark Bomani alisema kutokana na malumbano ya ufisadi yanayotokea kwa sasa, vitendo vya rushwa na ufisadi ni lazima vipigwe vita kwa nguvu zote, lakini sheria za kutuwezesha kufanya hivyo na sababu za kufanya hivyo vipo, kinachotakiwa ni utashi wa kufanya jambo hilo.

Copyright TSN 2006 All Rights Reserved
Hata mimi nimeona , umeboreshwa sana , asante ccm .
attachment-13-2.jpg
 
Back
Top Bottom