Fahamu undani wa mnyama simba

Fahamu undani wa mnyama simba

Uzazi wa simba unapishana vip maana naona kama umri wao ni mfupi....na simBa anazaa akifikisha umri gani.....
Kwa kawaida simba huzaa mda wowote katika mwaka either mara moja au mbili na kuhusu umri wa kuzaa huanza kuzaa wakishafikisha umri wa miaka miwili lakini huanza kubalehe wakishafikisha miezi 18 na wakishabalehe watoto madume hufukuzwa kwenye ile family ili wakajitegemee lakini watoto majike hubaki kwenye ile family ili kuendeleza uzao
 
mm bado nahitaji kujua elimu zaidi ya simba inakuwaje simba wa buga za selegeti anapanda kwenye miti huku wale wa poli la akiba selou awapandi juu ebu nijuze mkuu
 
Mkuu mbona unatuchanganya? Unasema Simba hulala saa 16 na kuwinda kwa saa 8 halafu hapo hapo unasema akiwa honeymoon hugegeda kila baada ya dakika 7
Sasa vipi atagegeda kila baada ya dakika 7 na yeye 16 hrs huwa amelala tuu? Au kwenye honeymoon huwa halali kwa 16 hrs?
We nawe ndio huelewi kitu
 
Hii elimu imenifanya nimpende mnyama huyu, tatizo kuna timu moja ya matopeni inatumia jina hili, hicho ndicho nisichokipenda.
 
Lakini mbona Tembo wana ushirikiano saba na wanatembea kwenye makundi - hivi Simba wanaweza kuwa na ujasiri wa kumshambulia Tembo kweli?

Simba kwa kawaida hawashughuliki na tembo mkubwa, kwani kumkamata ni kama haiwezekani vile, labda huyo tembo awe mgonjwa au dhaifu kabisa.., mara nyingi wakitaka kuwinda tembo wanavizia watoto au ndama wa tembo japokuwa kuwakamata nao hao si kazi ndogo kabisa na hata simba wanalijua hilo.. Hivyo ni nadra sana kukuta simba wakishughulika nao....
 
Simba jike aliyekomaa kuzaa anaishi katika familia yao kumbuka madume yanakuja nakuondoka ila majike daima wanabaki na koo yao daima wao wanaishi kama mabibi.mama.shangazi.mabinamu katika kaya yao pia kukumbusha tena ikitokea mwezao mmoja anakaribia kufa wanajua kuwa mwezao haponi na wale Wa umri wake wanamsindikiza safari yake ya mwisho na wanamuacha wanaondoka zao

Hii sehemu imenisisimua na kunisikitisha sana.
 
Kwa kawaida simba huzaa mda wowote katika mwaka either mara moja au mbili na kuhusu umri wa kuzaa huanza kuzaa wakishafikisha umri wa miaka miwili lakini huanza kubalehe wakishafikisha miezi 18 na wakishabalehe watoto madume hufukuzwa kwenye ile family ili wakajitegemee lakini watoto majike hubaki kwenye ile family ili kuendeleza uzao
Kwa maana hiyo wale mabinti hupandwa na baba zao?
 
GJY6QL3NGwd4KSZ23Hu-ofox_UQj0UkGiONUj2nWsvmvB-nKHo9a6I_tazn0_X5UhA=h900

Simba kwa kiingereza anafahamika kama lion na jina lake la kisayansi (scientific name) anafahamika kama panthera leo na koo(Genus) yake ni panthera, hii koo panthera inajumuisha na wanyama wengine ikiwemo tiger wa bara la asia, chui, American jaguar, na mnyama anaefahamika kama puma au mountain lion.

Simba yupo kwenye order ya wanyama walaji wa nyama almaarufu carnivore na familly yake inaitwa felidae, hii familly ya felidae inajumuisha paka wote wanaopatikana duniani ikiwemo wanaofugwa manyumbani, paka pori, simba, chui, tiger, jaguar na wengineo jamii ya paka ikiwemo cheetah(Duma).

Simba ndiye paka mkubwa Africa na anashika namba mbili duniani baada ya tiger ambaye anapatikana barani Asia pekee dunia nzima na simba pekee ambaye huishi katika makundi miongoni mwa wanyama jamii ya paka na kundi lao linaitwa(pride) pia simba ni wanyama wanaopendelea kuishi maeneo wazi yenye nyasi(Open area) kama ngorongoro crater na Serengeti national park.

Simba pia anafikia hadi uzito wa kg 220-250 kwa dume na upande wa jike ni kg 100-120 na katika familia ya simba ni majikee pekee wanaofanya shughuli ya uwindaji (hunting ) na madume wao hubaki na watoto na majike wakishaua mnyama simba dume ndo huanza kula kisha watoto na baadaye jike ilihali wao ndo wawindaji.

Pia simba ndo wanyama wanaoongoza kwenda fungate (Honeymoon ) na huenda kwa takribani wiki mbili, iko hv kwa kuwa hawa wanaishi katika makundi dume na majike ikitokea katika ile familia kama kuna jike ambaye yuko heat hua anamchukua dume wanaenda mbali kidogo na ile familia kwa ajili ya kufanya mating kwa huo muda wa wiki mbili na kabla ya kwenda fungate kwa kawaida yule jike anayehitaji kwenda fungate na dume huwa anamuwindia dume chakula kizuri chenye mafuta ambacho kitamshibisha yule dume na wakiwa fungate huwa hawali kitu chochote wanakunywa maji tu kwa huo mda wa wiki mbili na huwa wanajamiana kila baada ya dakika saba (sasa ebu fikiria siku ina dakika saba ngapi na kwa huo mda wa wiki mbili dume atampanda jike mara ngapi).

Simba pia hupendelea kuwinda wanyama kama mbogo, pundamlia, nyumbu na baadhi ya swala na kwa kawaida simba dume ana uwezo wa kula hadi Kilo 15 za nyama na akishakula hizo kilo 15 huwa anauwezo wa kukaa siku tatu mpaka wiki moja bila kula halafu ndo anakuja kuwinda tena.

Katika kuwinda kwao wanatumia staili kuu tatu ya kwanza ni sporting ( wanaangalia mnyama wa kumuwinda), ya pili ni stalking ( wananyemelea ) na ya mwisho ni ambush ( kuvamia) na wakishakamata mnyama huwa wanakimbilia kuuma shingoni ili kumbana pumzi(suffocate) na sio kunyonya damu kama wengi wanavyodhani na kwa kawaida simba jike hubeba ukauzito kwa mda wa miezi 3 na anazaa kuanzia watoto 2-4.

Sasa unaweza ukajiuliza kama jike la simba hubeba ujauzito kwa huo mda na kujifungua watoto wengi mbona simba ni wachache? Iko hv hawa wanaishi kwenye makundi dume akimiliki majike wake na huwa hawa madume wenye familia wanachallengiwa na madume ambao hawana familly kwa ajili ya kimiliki zile familly na ikumbukwe sio madume wote wa simba wanamiliki familia sasa ikitokea kwa bahati mbaya huyu simba mwenye family akapigwa na dume mwenzake ambaye hana family huyu dume ambaye hana family atachukua ile family ya yule dume aliyempiga na kuitawala yeye na kwenye ile family akikuta kuna watoto wa yule dume aliyempiga atakachofanya huyu dume atawaua wale watoto wote kwa sababu hawezilea damu isiyoyake na anafanya vile ili jike mwenye wale watoto apatwe na uchungu aingie kwenye heat ili ambebeshe mimba yake na kama kwenye ile familia kuna jike mwenye ujauzito atakachofanya huyu dume atamchukua yule jike atamtoa nje ya family na ataforce kumpanda hadi ile mimba itoke then anampachika mimba yake.

Vile vile hawa simba dunia nzima wanapatikana Africa na Asia na katika bara la asia wanapatikana pale india pekee katika msitu unaoitwa geyforest. Vilevile hawa simba ndo wanyama wanaoongoza kulala kwa siku hulala masaa 16 na kufanya kazi masaa 8 na kawaida wanawinda usiku na wakati mwingine mchana pale hali inaporuhusu na hawa ni wachangamfu mchana na usiku (diurnal and nocturnal ) yaani wao huona usiku na mchana. Huyo ndo bwana simba (king of jungle ) kama wengi wanavyopenda kumwita.
Chanzo cha makala hii nzuri?
 
Back
Top Bottom