Je wajua kuwa simba dume mmoja akiwa anavamia na wenzake madume mfano matatu kabla ya kukutana nakupigana wanapeana vitisho vya mngurumo na endapo yule mmoja anayevamia akatoa mkali zaidi ya wale wanaokuja watatu wale watatu wanaghairi kuja wanajua mwezao ni mkali na ananguvu kubwa kuliko wao.pia simba dume anapovamia na wenzake na mfano wawili na kuendelea simba jike wale Wa yule anayevamia wanaweza kuamua kumsaidia dume au kutomsaidia.kwanini wanamsaidia kupigana.kama kuna watoto wadogo ambao wameshakua na wanajua akishindwa dume basi watoto wao watauliwa pia wanamsaidia kama yule dume ameishi kwa upendo mkubwa na wale wanaweke na kwanini simba majike yanpoamua kutomsaidia mwanaume pindi wanapovamia kwasababu dume limezeeka kwao kuna kuwa hakuna ulinzi wakuaminika kwa ajili ya watoto wao na mji wao pia simba jike wanapenda kupandwa na simba mwenye uwezo bora na nguvu ili kutoa watoto bora.pia je mnajua kuwa kila simba wanakaya zao ambazo daima zinatengenishwa na kwa kuweka alama ya mikojo ya simba dume ambao ndio walinzi wakuu wafamilia.je wajua kuwa ikitokea kwa simba majike yakavuka mpaka Wa kwenda kuwinda na watoto zao na wakakumbana na masimba jike wakaya nyingine ambao ndio eneo lao wale waliovamia atakama wako wengi wanakimbiasana na ikitokea walikwenda na watoto wao wanawaacha nyuma na wale waliowafumania kama wale watoto wakiwa wadogo sana hawahui na watawaacha mpaka mama yao atakapowaita kwa mlio maalumu.