Fahamu undani wa mnyama simba

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Jul 25, 2016
533
1,000
GJY6QL3NGwd4KSZ23Hu-ofox_UQj0UkGiONUj2nWsvmvB-nKHo9a6I_tazn0_X5UhA=h900

Simba kwa kiingereza anafahamika kama lion na jina lake la kisayansi (scientific name) anafahamika kama panthera leo na koo(Genus) yake ni panthera, hii koo panthera inajumuisha na wanyama wengine ikiwemo tiger wa bara la asia, chui, American jaguar, na mnyama anaefahamika kama puma au mountain lion.

Simba yupo kwenye order ya wanyama walaji wa nyama almaarufu carnivore na familly yake inaitwa felidae, hii familly ya felidae inajumuisha paka wote wanaopatikana duniani ikiwemo wanaofugwa manyumbani, paka pori, simba, chui, tiger, jaguar na wengineo jamii ya paka ikiwemo cheetah(Duma).

Simba ndiye paka mkubwa Africa na anashika namba mbili duniani baada ya tiger ambaye anapatikana barani Asia pekee dunia nzima na simba pekee ambaye huishi katika makundi miongoni mwa wanyama jamii ya paka na kundi lao linaitwa(pride) pia simba ni wanyama wanaopendelea kuishi maeneo wazi yenye nyasi(Open area) kama ngorongoro crater na Serengeti national park.

Simba pia anafikia hadi uzito wa kg 220-250 kwa dume na upande wa jike ni kg 100-120 na katika familia ya simba ni majikee pekee wanaofanya shughuli ya uwindaji (hunting ) na madume wao hubaki na watoto na majike wakishaua mnyama simba dume ndo huanza kula kisha watoto na baadaye jike ilihali wao ndo wawindaji.

Pia simba ndo wanyama wanaoongoza kwenda fungate (Honeymoon ) na huenda kwa takribani wiki mbili, iko hv kwa kuwa hawa wanaishi katika makundi dume na majike ikitokea katika ile familia kama kuna jike ambaye yuko heat hua anamchukua dume wanaenda mbali kidogo na ile familia kwa ajili ya kufanya mating kwa huo muda wa wiki mbili na kabla ya kwenda fungate kwa kawaida yule jike anayehitaji kwenda fungate na dume huwa anamuwindia dume chakula kizuri chenye mafuta ambacho kitamshibisha yule dume na wakiwa fungate huwa hawali kitu chochote wanakunywa maji tu kwa huo mda wa wiki mbili na huwa wanajamiana kila baada ya dakika saba (sasa ebu fikiria siku ina dakika saba ngapi na kwa huo mda wa wiki mbili dume atampanda jike mara ngapi).

Simba pia hupendelea kuwinda wanyama kama mbogo, pundamlia, nyumbu na baadhi ya swala na kwa kawaida simba dume ana uwezo wa kula hadi Kilo 15 za nyama na akishakula hizo kilo 15 huwa anauwezo wa kukaa siku tatu mpaka wiki moja bila kula halafu ndo anakuja kuwinda tena.

Katika kuwinda kwao wanatumia staili kuu tatu ya kwanza ni sporting ( wanaangalia mnyama wa kumuwinda), ya pili ni stalking ( wananyemelea ) na ya mwisho ni ambush ( kuvamia) na wakishakamata mnyama huwa wanakimbilia kuuma shingoni ili kumbana pumzi(suffocate) na sio kunyonya damu kama wengi wanavyodhani na kwa kawaida simba jike hubeba ukauzito kwa mda wa miezi 3 na anazaa kuanzia watoto 2-4.

Sasa unaweza ukajiuliza kama jike la simba hubeba ujauzito kwa huo mda na kujifungua watoto wengi mbona simba ni wachache? Iko hv hawa wanaishi kwenye makundi dume akimiliki majike wake na huwa hawa madume wenye familia wanachallengiwa na madume ambao hawana familly kwa ajili ya kimiliki zile familly na ikumbukwe sio madume wote wa simba wanamiliki familia sasa ikitokea kwa bahati mbaya huyu simba mwenye family akapigwa na dume mwenzake ambaye hana family huyu dume ambaye hana family atachukua ile family ya yule dume aliyempiga na kuitawala yeye na kwenye ile family akikuta kuna watoto wa yule dume aliyempiga atakachofanya huyu dume atawaua wale watoto wote kwa sababu hawezilea damu isiyoyake na anafanya vile ili jike mwenye wale watoto apatwe na uchungu aingie kwenye heat ili ambebeshe mimba yake na kama kwenye ile familia kuna jike mwenye ujauzito atakachofanya huyu dume atamchukua yule jike atamtoa nje ya family na ataforce kumpanda hadi ile mimba itoke then anampachika mimba yake.

Vile vile hawa simba dunia nzima wanapatikana Africa na Asia na katika bara la asia wanapatikana pale india pekee katika msitu unaoitwa geyforest. Vilevile hawa simba ndo wanyama wanaoongoza kulala kwa siku hulala masaa 16 na kufanya kazi masaa 8 na kawaida wanawinda usiku na wakati mwingine mchana pale hali inaporuhusu na hawa ni wachangamfu mchana na usiku (diurnal and nocturnal ) yaani wao huona usiku na mchana. Huyo ndo bwana simba (king of jungle ) kama wengi wanavyopenda kumwita.
 

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
8,675
2,000
Sasa hapo kwenye kugegeda ndio amenimaliza........yaani anagegeda kila baada ya dakika saba duuuuuh
 

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
5,865
2,000
Simba kofi lake ni kilo50
Simba ni mnyama mwenye aibu kupindukia hawez kukuangalia usoni.
Pride kubwa duniani iko serengeti ina simba karibu 45 wanaishi pamoja.
Simba wakiwa wanakula hawana uchoyo hata simba jirani anaweza kupita hapo na kula bila bughuza.
Simba top speed yake 60-75 kph.
Simba dume hawindi sababu lizito.ukisikia simba kaingia kijijini anakula mifugo ni simba mzee au dhaifu aliefukuzwa na vijana ili aachie familia yake damu moto.simba dume akifika miaka2 anatakiwa akajitegemee aondoke ktk familia kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom