Fahamu undani wa mnyama simba

Fahamu undani wa mnyama simba

Nashukuru mkuu kwa kunifahamisha vizuri sana na umeniongezea mnyama Puma asante, lakini nina swali,mimi nilivyokuwa najua mnyama Cheetah (duma) ndio mwenye spidi sana kuliko wote kumbe sio hivyo au sijakuelewa vizuri ??
Ndio cheetah ndio mnyama mwenye kasi kuliko wote speed yake ni 110sqkm per hour
 
Kumbuka wanyama awafanya ngono kwa starehe kama sisi.wao mpaka wanawake wapate joto la kushika mimba na dume anapewa taarifa na jike kwa ishara zao maalumu
Kweli mkuu wanyama hawajamiani kwa ajili ya starehe bali hujamiana kwa kipindi maalumu ili kuongeza uzazi katika familia
 
Asante wakuu tumejifunza mengi,swali langu ni kuwa,inakuwaje wanyama pori wengine tunakula na wengine hatuli?mfano simba,je pengine umeshafanyika utafiti kuwa aina fulani za wanyama zinafaa kuliwa na zingine hazifai au tunabahatisha tu?
Mkuu kwa kawaida kila kiumbe duniani kinaliwa ila inategemea na imani ya mtu lakini viumbe hai vyote vinaliwa
 
Wajua kuwa simba wengi wanauwa na Buffalo. Je wajua kuwa pembe ya Buffalo pigo lake nikali kuliko sumu ya nyoka na simba wanajua hilo na ndio maana wanapominda buffalo wanakuwa makini sana kutopigwa pembe.je wajua kuwa simba anapowinda buffalo wanapomkamata lazima wamfunge mdomo ili asitoe mlio kwani akilia tuu wanakuja wenzake kumuokoa.pia wajua kwanini simba anatoa mlio mkubwa sana kwa sababu koromeo lake limeundwa kwa mfumo Wa duara na kuna ngozi yenye mafuta laini ndani yakoromeo inayomsaidia kutoa sauti kubwa
Sio buffalo tu simba wanapowinda mnyama yoyote huwa wanajihadhari wasipigwe pembe maana ngozi yao ikipata jeraha huwa ni vigumu kupona na kuhusu kukaba koo hiyo inafanyika kwa wanyama ambao ni carnivore na wanafanya vile ili kumnyima pumzi mnyama yoyote wanayemuwinda isipokuwa tu kwa mbwa mwitu ambao huweza kumuua mnyama bila kumsuffocate
 
Mkuu
Hilo nakubaliana na wewe,
Swali langu ni kuwa; Kwenye pride moja kuna uwezekano wa majike wengi je hili dume litakutana nao wote katika muda tofauti wakiwa kwenye joto?
Inategemea kwenye ile pride kuna madume wangapi maana kuna pride nyingine zenye madume zaidi ya mmoja
 
tupeane elimu km hizi na tembo naye anaenda hanimuni kwa muda gani mkuu
Tembo wao hawaendi fungate ila jike akiwa kwenye heat huwa anatoa harufu flani itakayomwashiria dume kuwa yupo kwenye heat lakini wao hawaendi fungate. Fungate ni kwa simba pekee
 
Simba jike aliyekomaa kuzaa anaishi katika familia yao kumbuka madume yanakuja nakuondoka ila majike daima wanabaki na koo yao daima wao wanaishi kama mabibi.mama.shangazi.mabinamu katika kaya yao pia kukumbusha tena ikitokea mwezao mmoja anakaribia kufa wanajua kuwa mwezao haponi na wale Wa umri wake wanamsindikiza safari yake ya mwisho na wanamuacha wanaondoka zao
Kaka una point sana na unawajua sana hao Paka wakubwa, sema hueleweki vizuri kabisa, sijuhi ni simu unayotumia au ni haraka ya kuandika
 
Sidhani kama hata swala kama yupo huko. Maana kuna mzungu alikuja hapa bongo, alikimbia mjusi eti anasema ameona kamnyama chumbani
Swala wapo mkuu maana kuna swala wa aina nyingi mfano kuna hawa wenye mapembe kama matawi ya miti wanaitwa deer ni miongoni mwa swala wanaopatikana American, Asia na Europe
 
Sidhani kama hata swala kama yupo huko. Maana kuna mzungu alikuja hapa bongo, alikimbia mjusi eti anasema ameona kamnyama chumbani
na nyie mmezidi uchafu mpaka kuishi na mijusi chumbani, inawezekana mnaishi na mipanya, mikunguru, mipaka mwitu nk, vinginevyo asante sana ww muanzisha uzi kwa kuwa nimejua tabia za watu.
 
Simba hawez kumrukia mwendesha pikipiki anaekatiza mbugani kama Mikumi!!?
 
na nyie mmezidi uchafu mpaka kuishi na mijusi chumbani, inawezekana mnaishi na mipanya, mikunguru, mipaka mwitu nk, vinginevyo asante sana ww muanzisha uzi kwa kuwa nimejua tabia za watu.
Kukaa kwako mjini unajifanya hujawahi ona mjusi ndani ya nyumba, nyie ndo wale mnawakataa hata wazazi wenu eti kisa ni mzee. Kwa kusema hivyo watu wajue eti wewe ni msafi!! Ebo mbuzi kasoro mkia.
 
Back
Top Bottom