Fahamu sifa kubwa ya Infinix Hot 10 PLAY zaidi ya Samsung A02S

Mkuu, huibiwi, pia hulazimishwi wala hakuna atakayekushawishi upeleke simu yako kwa fundi, fundi simu ni kama daktari wa binadamu, mmiliki ukiona unashindwa kutatua tatizo husika ndipo utakapojikuta unawaona wenye ujuzi

Na hizo simu ukipeleka kwa fundi usidhani atahangaika kurecovery password, hapana

Atakachokifanya ni kuiondoa kabisa, anaiondoaje? sasa hapa ndo linapokuja suala la matumizi ya vifaa kama pc na boxes(ambazo bei zake zimechangamka)

Hivyo fundi atakachokifanya anakupa bei kulingana na ugumu wa kazi na vitendea kazi vitakavyotumika hivyo usidhani unaibiwa au unadanganywa

Kama unajijua una kichwa kizuri kutunza kumbu kumbu ni jambo jema ila usiseme kwamba mafundi simu ni wezi hii ni kazi kama kazi zingine maana watu wananunua microscope mpaka 5 milions kwa ajili ya ufundi simu hivyo unapoambiwa simu flani gharama yake ni kiasi fulani usiropoke eti unaibiwa kama ni hivyo simu yako kama ikitokea umesahau password ihifadhi mpaka utakapoikumbuka (hii mara nyingi huwa nawaambia wateja)
Tena huwa namwambia achague moja kati ya mambo mawili aweke simu kwenye droo ili afanye jitihada za kukumbuka password au atoe pesa ifutwe

Binafsi wapo wateja wanaokuja kuniomba ushauri ni simu gani ya kununua kati ya Oppo, Vivo, xiaomi na Samsung
Huwa nawaambia ukweli tu, "KAMA UNAKICHWA KIZITO KWENYE MASWALA YA KUKUMBUKA PASSWORD NUNUA SAMSUNG, ILA KAMA UNA KICHWA CHEPESI NA UNAJIJUA HUWEZI KUSAHAU PASWORD JICHAGULIE KATI YA OPPO, VIVO AU XIAOMI"
Inafutwaje
 
Uongo infinix inafast charge ya 10w, na hiyo 6000 mha inakuwa full charge in 2 hrs...
 
Infinix Hot 10 Play haijawahi kuwa high End .

High end ni kina Sam S21 &Co.. (Flagship)
Mimi nimeshatumia hizo Infnix, Tecno vizuri kabisa lakini amini amini nakwambia hizo ni upupu tu ndio mana nikahama na sina mpango wa kurudi huko
Huo ni mtazamo wako hot play ni simu za high end low budget phone wewe kama kutoa 3M ndo unaoan high end ni sawa lakini both phone run android q...na ndo kitu kizuri kwenye open operating system, tutanyanyapiana kwenye hardware features.. lakini tunatumia the same operating system
 
Habari nimeona ni share na nyinyi hii,

Katika ushindani wa soko la simu kampuni nyingi za simu zimejikuta zikitoa simu zenye kushabihiana sifa. Kwa leo tuliangalizie kwa ndani simu aina ya Infnix Hot 10 Play na Samsung Galaxy A02s.na mwisho wa makali hii nadhani tutakuwa tumepata kufahamu ipi ni simu sahihi.

kwako kotokana na matumizi yako.

Screen-Shot-2021-03-12-at-12.14.25.png


Sifa za Ndani (CPU, Chipset, RAM na ROM)

Kwa upande wa sifa za ndani, Infinix Hot 10 Play inakuja na CPU yenye uwezo zaidi hadi Octa- core (2×2.0 GHz Cortex-A75 & 6×1.8 GHz Cortex-A55), huku Galaxy A02s ikiwa nyuma yake kwa kuwa na CPU yenye uwezo wa hadi Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53.

Mbali na hayo, Infinix Hot 10 Play inakuja na Chipset ya MediaTek Helio G35, wakati Galaxy A02s inakuja na Chipset ya Qualcomm Snapdragon 450. Chipset zote zinakuja na uwezo tofautin ani rafiki hata katika uchezaji games kupitia simu hizo.

Kwa upande mwingine wa RAM, Infinix Hot 10 Play inakuja na RAM ya GB 4, huku Galaxy A02s yenyewe ikiwa inakuja na RAM kati ya GB 3. Tukiangalia uhifadhi wa ndani, Galaxy A02s inakuja na ROM ya GB 32, huku pia Infinix Hot 10 Play nayo inakuja na ROM ya hadi GB64.

Uwezo wa Battery

Infinix Hote 10 Play ni moja kati ya simu ambayo ipo kwenye list ya simu zinazodumu na chaji zaidi mwaka 2021, hii ni kwa sababu simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa hadi 6000 mAh, huku ikiwezeshwa na teknolojia ya kufanya ijae na chaji kwa haraka yaani Fast charging yenye uwezo wa 10 Wh. Galaxy A02s yenyewe inakuja na battery ya 5000 mAh, huku nayo ikiwa na Fast charging ya hadi 18 Wh.

Muundo

Kwa kuanza, tuakiangalia muundo wa simu zote mbili, zote zimetengenezwa kwa plastiki, hii ikiwa na maana muundo wa nyuma wa simu hizi ni plastiki, na hata fremu yake pia ni plastiki. Kwa nyuma Infinix Hot 10 Play inakuja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint, huku Galaxy A02s yenyewe ikiwa haina sehemu hiyo kabisa.

Kioo
Kwa upande wa kioo Infinix hot 10 play inakuja na kioo kikubwa wa inch 6.82, huku Galaxy A02s ikiwa inakuja na kioo cha inch 6.5. Mbali na hayo, kioo cha Infinix Hot 10 Playkimetengezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, wakati kioo cha Galaxy A02s kikiwa kimetengezwa kwa TFT/PLS IPS. Kwa upande wa resolution simu zote mbili zinakuja na uwezo wa 720p.

Kamera

Kwa upande wa kamera Samsung Galaxy A02s na Infinix Hot 10 Play zote zinakuja na kamera kuu za nyuma za Megapixel 13, huku Galaxy A02s ikiwa na kamera mbili zaidi zenye Megapixel 2 kila moja. Hii inafanya simu ya Galaxy A02s kuwa na Kamera tatu, huku Inifnix Hot 10 Play ikiwa na kamera mbili kwa nyuma.

Kwa upande wa kamera za mbele, Infinix Hot 10 Play inakuja na kamera ya Megapixel 8, huku Galaxy A02s ikiwa inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 5. Pia kamera hiyo ya Infinix Hot10 Play inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps. Vilevile Infinix Hot 10 Play inakuja na LED flash kwenye kamera ya mbele, wakati Galaxy A02s yenyewe haina sehemu hiyo.

Mfumo wa Undeshaji
Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji, Galaxy A02s inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Android 10, huku Inifnix Hot 10 Play nayo pia ikija na mfumo wa Android 10 ambao ni Go Edition. Simu ya infinix inakuja na mfumo mpya wa XOS 7, wakati Galaxy A02s ikiwa inakuja na mfumo wa One UI.

Uwezo wa Battery

Infinix Hote 10 Play ni moja kati ya simu ambayo ipo kwenye list ya simu zinazodumu na chaji zaidi mwaka 2021, hii ni kwa sababu simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa hadi 6000 mAh, huku ikiwezeshwa na teknolojia ya kufanya ijae na chaji kwa haraka yaani Fast charging yenye uwezo wa 10 Wh. Galaxy A02s yenyewe inakuja na battery ya 5000 mAh, huku nayo ikiwa na Fast charging ya hadi 18 Wh.

Bei za Makadirio
Kwa upande wa Bei, Inifnix Hot 10 Play inapatikana kwa bei ya makadirio kuanzia TZS 350,000 wakati Galaxy A02s inapatikana kwa bei ya makadirio kuanzia TZS 450,000. Kumbuka bei hizi ni makadirio na zinaweza kubadilika kulingana na eneo unalo nunua simu hizi.

Upatikanaji
Kwa sasa simu zote zinapatikana hapa Tanzania, huku Infinix Hot 10 Play ikiwa inapatikana kupitia kwenye maduka ya kampuni ya kutoa huduma za simu ya Tigo Tanzania, pamoja na maduka ya simu ya Infinix kote Tanzania ikiwa na ofa ya GB 18.
Android 10 Go edition ni ya hot 10 lite na play ya 32gb na 2gb ram pia ina cpu tofauti na 64gb
 
Umejitahidi mkuu ila umetupiga kamba sana.

Samsung A02 ni low end kushinda A10 series, Aggrey nimepita ni laki 3 hata sijaingia deep, bei yake itakuwa 250k ama chini ya hapo Sababu A11 ndio ipo teritorry ya 300k.

Pia G35 haina core za Cortex A75, Bali ni cortex A53 tu. Na hio infinix inakuja na G25 ambayo ndio ina cortex A75.

Pia hio infinix base version ni 2gb ram na 32Gb storage wakati A02 ni 3gb ram na 32gb, zote Zina option ya 4GB ram na 64Gb storage.

Na 6000mah bila fast charging unachaji siku nzima. Ukisahau tu kuichaji usiku imekula kwako.

Infinix ina micro USB na Ao2 ina type C
Mkuu nisaidie jinsi ya kujua original charger ya 15w.
 
Mkuu nisaidie jinsi ya kujua original charger ya 15w.
1. Angalia kwenye charger yenyewe kwanza Wana andika.

2. Download app inaitwa Accubattery hii ni nzuri kutestia fast charging, Iache kwa muda ichaji Kisha fungua app kuangalia. Volt x ampere ndio unapata idadi ya hizo watts.

3. Android versions baadhi huandika pia kama simu ina charge slow, kawaida ama faster.

Sema kama simu haisupport 15w fast charging, hata kama charger inasupport haisaidii.
 
1. Angalia kwenye charger yenyewe kwanza Wana andika.

2. Download app inaitwa Accubattery hii ni nzuri kutestia fast charging, Iache kwa muda ichaji Kisha fungua app kuangalia. Volt x ampere ndio unapata idadi ya hizo watts.

3. Android versions baadhi huandika pia kama simu ina charge slow, kawaida ama faster.

Sema kama simu haisupport 15w fast charging, hata kama charger inasupport haisaidii.
Thanks mkuu
 
Yaani hawa jamaa wanasikiliza story za vijiweni kwamba infinix na tecno sio simu kumbe wananunua infinix na tecno za elfu 7,ndio maana nikamwambia anunue hizo za bei kubwa hakika hatorudi kwenye misamsangi....Hata samsung za bei rahisi nazo ni mbovu tu speed kobe....Ukitaka kula nyama chagua iliyonona.
Kuna vtu vinashangaza sana mfano mtu anasema tecno au inifinx sio sim bila ata kuelezea vzur maana kuna ifininx nyng au tecno nyng zimezd ayo wanayosema masim mtu ananunua samsung kwa lak tano alaf anataka kushindanisha na tecno au infinx ya lak moja na nusu iv samsung mfano a10 ikaizd ubora tecno camon 16 au samsung s2 ikaizid uwezo infinix note 7 ,mwingne anakuambia tecno na inifinx sio sim alaf anaisifia oppo wakat karbu kila ktu wanashea ,kuna aja kuanza kufanisha bei kwanza sio kusema tu aina fulan sio sim na kingne kimpendacho mtu na ndio maana pamoja na sifa na ubora wa iphone lkn badp weng wao wanazikataa sima za china wanatumia samsung na nyngne kutoka uko uko china
 
Infinix Hot 10 Play haijawahi kuwa high End .

High end ni kina Sam S21 &Co.. (Flagship)
Mimi nimeshatumia hizo Infnix, Tecno vizuri kabisa lakini amini amini nakwambia hizo ni upupu tu ndio mana nikahama na sina mpango wa kurudi huko
we jamaa nikitaka kununua simu nitakutafuta unipipe ushauri unaonekana uko nondo kiaina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom