Infinix kama BMW

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Kampuni Bora ya simu inayokuja kwa kasi afrika transsion holding wametoa toleo jipya la Infinix aina ya Note 30 VIP kwa kushirikiana na kampuni Bora ya magari ulimwenguni Bmw.

Muundo wake uko poa sana haswa ukishika unaweza sema madini flani hivi kwa nyuma Kuna 3D light yenye mistari mitatu kama rangi ya bmw inayokupa ishara ya kuonyesha nguvu, ufanisi , spidi.

imekuja ikiwa na themes za bmw zenye kuvutia, chaji Yenye 68W wired na wireless ambayo ni 50W ndani ya nusu saa simu inajaa ikiwa na betri lenye 5000Mah.

processor yake ni MediaTek Dimensity 8050 Mtk 6893 inakupa uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali Kwenye simu bila kupata sana joto na kuganda Ganda kwani unaweza cheza game huku ukiwa una chati na wengine.

InfinixBmw%20%E2%80%93%205.jpg

Kioo chake ni AMOLED display kikiwa na high resolution ya 120Hz inayo fanya kuwa smooth wakati unaitumia bila kusahau fingerprint ndani ya kioo cha mbele.

kamera yake Iko poa sana maana Ina 108mp + 2mp + 2mp ikiwa na 4k resolution inayokufanya huwe na uwezo wa kuchukua video Kwenye mazingira yoyote Yale.

kamera ya mbele 32mp inatoa picha natural bila filter yoyote unavimba,imekuja ikiwa na ram yenye 8Gb mpaka 12Gb pamoja na storage kuanzia 128Gb na 256Gb.

kwa maelezo zaidi tembelea maduka ya Infinix Tanzania
 
duuh nikisikia neno infinix au tecno basi sihitaji maelezo mengi tena na hiyo mediatek ๐Ÿง‘โ€๐Ÿฆฏ๐Ÿง‘โ€๐Ÿฆฏ
 
Back
Top Bottom