Fahamu matokeo ya meditation

..........SISI NI NANI (WHO ARE WE)❓........
✍️✍️✍️✍️What define us?✍️✍️✍️✍️

Sehemu ya kwanza.

Muandishi ni 👇👇

🤜Na Dogoli kinyamkela

Sisi ni viumbe Nuru(we are light being),sisi ni Nuru yenyewe, sisi ni Chanzo(source), sisi ni mmoja/moja(we are one),sisi ni MUNGU, sisi ni ADAM/ATUM/ATOM...

Mliosoma Atomic physics mtanielewa japo hamkupewa lishe nzima Leo napaacha..

Ebu nijaribu hivi!!.....

MWILI ili uweze Kuitwa MWILI unaudwa na Muunganiko wa Viungo vingi ambavyo ni
🔸Kichwa...
🔸Shingo..
🔸Mikono...
🔸Kiwiliwili...
🔸Miguu..nakadharika,nakadharika
mfano...👇

◾Kichwa kina Ubongo,masikio,macho, kinywa(Midomo,ulimi,meno),Nywele,n. K

◾Mikono Ina viganja,viwiko,vidole na kucha..

◾Kiwiliwili Kuna Tumbo, Moyo, Ini, mbavu, njia za haja kubwa na ndogo n. K....

◾Miguu Ina mapaja, magoti, ugoko na kanyagio

👉Hivi vyote vikiunganishwa huitwa MWILI( mmoja/moja) unaotokana na Viungo vingi, kwahiyo Viungo hivyo vinapata sifa ya Kuitwa MWILI/BODY kwa sababu Viungo hivyo vimesababisha uwepo wa mwili na bila Viungo hivyo huyo kiumbe mkubwa MMOJA mwenye Viungo vingi akikosa hivyo Viungo hawezi kuwepo, hakutokuwepo kitu kiitwacho MWILI.

👉Kwa mfano Kichwa Kikijiona chenyewe kuwa ni mkuu kuliko Viungo/sehemu zote za mwili, Ebu fikiria Tumekikata kichwa Kisha tukakiweka pembeni, Sasa JE Kuna yeyote atakiita kichwa kuwa ni MWILI? Kwa hakika hapana Bali jamii itasema "HIKI NI KICHWA CHA MWILI WA BINADAMU" Kwamba tayari kimepoteza sifa ya kuwa MWILI. sijui mfano huu ninaeleweka?

👉Sasa hata Katika Dhana(nadharia) ya Mungu, we are all gods and Goddess. Kwamba sote ni Mungu wa kike kwa kiume, Na kitenda wili na Fumbo la Imani ni Kwamba tunafikiri sisi ni tofauti kwa kutazama mwonekano wetu wa sura za nje, kumbe sisi sote ni mmoja yule yule kivipi?

👉Anaitwa THE ONE Yani MMOJA, sindio MUNGU ni mmoja kwa mujibu wa Imani/Dini yako? Sasa sisi sote Kwa pamoja ni KIUMBE MMOJA MKUBWA (MUNGU) hatembei, haendi mbele Wala nyuma Bali yeye ni UFAHAMU (consciousness) mmoja tu yupo tuli/ametulia. Kwamba tunaona sisi ni viumbe tofauti tunaofanya kazi tofauti mfano Huyu anakula, yule analima na Mwingine anaendesha Gari na yule Amelala... Lakini kumbe ni Kiumbe MMOJA tu anayeyafanya hayo yote kwa Pamoja. Ukiingia kwenye injili ya Siri iliyofichwa na kutolewa kwenye biblia na msahafu iitwayo injili ya Yohana(THE SECRET GOSPEL OF JOHN) utamuona huyo THE ONE ameelezewa kwa uzuri kabisa humo

👉Tukirudi nyuma nilisema sheria namba moja Katika sheria za ulimwengu(universal laws) iitwayo "Sheria ya umoja wa Mungu(THE LAW OF DIVINE ONENESS) inasema kila kitu kimeunganishwa na kitu kingine hivyo hakuna utengano Kwa sababu kila kitu ndani yake kina Chanzo ambacho ni nishati/energy ama Katika Dini huiita " ROHO" na uzuri Wana Dini pasipo shakha huamini Mungu ni Roho ijapokuwa Huwa hawajui kuwa wanaomtafuta nje yumo ndani yao kwani sisi sote ni viumbe vya Kiroho tunavaa hii miili yetu ya kifizikia kwa Kusudio maalumu Kwamba tupo Katika ulimwengu wa utashi wa chini(3D) ili kukuza Ufahamu wetu ili tushift/tuhame kuelekea Katika ulimwengu(Dimensions) za juu zaidi na tusiendelee Kuzaliwa hapahapa Duniani, ni muhimu kutambua kuwa neno KUFA halipo Bali tuseme kushift frequence(kubadili mwonekano wetu na hata mazingira Kwa sababu nishati/nguvu/energy can neither be created nor destroyed Yani nishati(Roho) haikuumbwa na Wala Haina mwisho(haifi),Ndiomaana tunasema Universal energy au Cosmic energy ndiye muumbaji Yani MUASISI WA VITU VYOTE, Yaani Alpha (zero Quantum Energy)

✍️Wewe mgeni, wewe MTU wa Dini Ebu jiulize maswali haya machache Tena jiulize ukiwa mbele ya kioo, fanya hivi👇

◾Kaa mbele ya kioo chako...
◾Ongea na mtu aliye mbele yako anayefanania na wewe kwa 100%
◾Jiulize Mimi ni Nani?
◾Hizi nguo nilizo zivaa ni za Nani? Hakika utajijibu kuwa ni zako lakini ukitambua kuwa wewe sio hizo nguo.
◾Jiulize huu mkono ni wa nani, hakika unauakika kuwa ni mkono wako huo Ila unajua kuwa wewe sio huo mkono,
◾Jiulize Tena huo mwili unaouona Katika hicho kioo ni WA Nani? Kwa ufasaha akilini utajijibu kuwa huu ni MWILI WANGU, Sasa kwanini Automatically unajitenga na huo mwili?

Sasa swali Kama huo ni mwili wako, JE wewe ni Nani, wewe ni kitu gani haswa❓

Jitafute..... 🚶

Somo litaendelea......

Imeandikwa na Dogoli kinyamkela... ✍️

Kalibun jijini Whatsapp 👇🏼👇🏼

 
Kumfanya mtu asikufuatilie basi tafuta kichupa kidogo urefu wa kidole kisha weka unywele wake alafu nenda katupe kwenye maji yanayotiririka
 
Ukiona mgonjwa wenu kafariki ghafla basi hiki ndicho KINACHOTOKEA

Huwa wanachukua udongo wa kaburi kisha wanaweka chini ya kitanda cha mgonjwa

Wakiwa na lengo la kupoteza maisha yake

Wanachukua udongo wa upande wa kushoto wa kaburi yaani sehemu ya moyo wa marehemu hapo ndipo wanachimba na kuchukua udongo kwa mkono Baada ya kuchimba ndipo wanaweka chini ya kitanda cha mgonjwa
 
Nakuonea huruma sana; kwa sababu misingi ya yote unayoongea humu mimim nayafahamu sana. Siku nikipata nafasi nitakutafuta; itakuwa ni miaka kadhaa ijayo mbele; unaweza ukatimia hata muongo mmoja. Nitakutafuta
 
Hivi kwa nini meditation inakuwa link sana na dini za buddhism na hinduism na sio sana kwa Abrahamic religions
Catholic pia wanafanya sana meditations, mfano zile sala za ekàristi, Gregorian chants, hata zile order za monks na friers kama Franciscan monks/friars, Benedictines, Cappucins nk. Wanafanya sana Meditations
 
Mwendelezo ,somo la meditation.

Uzingativu paji la uso.

Katika utulivu unaoendelea kuupata,endelea kuzingatia kwenye paji la
uso,Endelea na kuendelea,
Sasa iache Pumzi na hata usiisikie Tena ,yaani sahau kama unapumua,Bali zingatio lako liwe kwenye paji la uso.
UTAONA mwili unaanza kama kufa Ganzi,endelea na Hali hiyo,kadri unavyoendelea
,UTAONA mwili wako unayeyuka ,unakuwa huuoni Tena mwili ,hujioni ,hata mahala/ramani ulipo huioni kiakili.

Wengine baada ya utulivu mkubwa huanza kuona miale ya Mwanga,Mwanga mkali ,viumbe mbalimbali,wewe endelea na utulivu.

Katika hatua hii ya meditation ,endelea kuwepo katika hatua hiyo ,endelea kuvuna mitetemo katika Hali hii,hakikisha ufahamu wako ndio unaona/umewaka.
Huu ni ufahamu wa nje ya maumbile/mwili.
👇👇👇
Faida za kufanya meditation ipasavyo.

👉machale yako yanakuwa ya juu sana/mitetemo/intuition.
Yaani unaweza ukaifikiria pesa na ikaja muda huo huo,ni vyema kuwaza yaliyo mema,kwa maana ukifikiri lililo baya litakupata.

👉kujiponya mwenyewe.
Meditation inaponya,pale Kundalini inapoamka ,uzima hupatikana ,chakra zako zinapofunguka hakuna ugonjwa utakao Baki ndani yako/utajiponya mwenyewe.

👉kuwa mtu wa maono.
UTAONA Kila kitu katika ulimwengu wa kiroho na asilimia kubwa vitatokea katika ulimwengu wa mwili.
Hapa ndipo tunapokuja kupata waonaji wa kiroho,Manabii na watu wenye karama mbalimbali hii ni kwa sababu ya utulivu huo.

👉kuwa mponyaji.
Unapofikia level za juu (kutembea katika nguvu ya Mwanga na Sauti).
Wewe unakuwa mponyaji ,hakuna kitu kitakushinda ,unakuwa mponyaji wa Ulimwengu,utaponya watu ,utaponya wanyama na vitu vyote vinavyokuzunguka.

👉kutokufa/kuishi milele.
Unapokuwa unafanya meditation ,unakuwa unajiwasha ndani mwako na hatimae kujua wewe ni nani katika ulimwengu huu,na kukamilisha kusudi lako.hivyo kufanya kutokuzaliwa Tena katika maumbile.

Hizo ni baadhi tu ya faida za meditation,ila faida zipo nyingi sana.
 
Kutoka nje ya mwili/Astral projection.

Ni kitendo Cha kutengana na mwili wako huu wa nyama.

Ni kile kitendo Cha mwili wako wa ndani kutoka nje ya mwili.

Kutoka nje ya mwili hufanyika kwa Namna mbili
Moja kujiandaa kwa kutulia kwenye utulivu.

Mbili ni kupitia kwenye ndoto.

Utokaji huu wa kupitia utulivu,mtu huweza kutoka nje ya mwili na kwenda mahala popote pale,huku akijua kabisa kuwa nipo nje ya mwili na kuuona mwili wake wa nyama ulipolala.

Tendo hili ni moja ya Namna ya kuiimarisha kiroho ,japo Sio Lazima kutoka nje ya mwili

Watu wengi hutaka kutoka nje ya mwili lakini hushindwa ,kutokana na kukumbana na kadhia ya maumivu ya mwili kama kudhani anakabwa na jinamizi ,kumbe ni dalili ya kutoka nje ya mwili,

Ukiweza kuivumilia Yale maudhi kwa sekunde 10 tu,utaweza kutoka nje ya mwili,ukifanikiwa kutoka nje ya mwili ,unashauriwa kutokwenda mbali kwa wale wanaoanza.

Tendo hili la kutoka nje ya mwili SI chochote katika utambuzi wa kiroho,kwa maana mwili huu wa ndani ,bado ni Mwili wa maumbile uliojishikiza katika mwili huu wa nyama.

Kwa hiyo utokaji huu upo wa aina mbili kama nilivyokwisha kusema ,watu wengi hutoka nje ya mwili bila wao kujua kupitia ndoto za usiku.

PInahitaji mazoezi ya kutosha ili kuwa mzoefu wa kutoka nje ya mwili.
 
Mimi nikijaribu kufanya Meditation akili inagoma kutulia kabisa adi nashindwa kuona chochote 👉 msaada nifanyaje ili akili itulie sehemu moja ?
 
Mkuu muendelezo wa hapa tuletee kama inawezekana lakin
 
Duh!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…