Fahamu matokeo ya meditation

Fahamu matokeo ya meditation

..........SISI NI NANI (WHO ARE WE)❓........
✍️✍️✍️✍️What define us?✍️✍️✍️✍️

Sehemu ya kwanza.

Muandishi ni 👇👇

🤜Na Dogoli kinyamkela
1737712967368.jpg


Sisi ni viumbe Nuru(we are light being),sisi ni Nuru yenyewe, sisi ni Chanzo(source), sisi ni mmoja/moja(we are one),sisi ni MUNGU, sisi ni ADAM/ATUM/ATOM...

Mliosoma Atomic physics mtanielewa japo hamkupewa lishe nzima Leo napaacha..

Ebu nijaribu hivi!!.....

MWILI ili uweze Kuitwa MWILI unaudwa na Muunganiko wa Viungo vingi ambavyo ni
🔸Kichwa...
🔸Shingo..
🔸Mikono...
🔸Kiwiliwili...
🔸Miguu..nakadharika,nakadharika
mfano...👇

◾Kichwa kina Ubongo,masikio,macho, kinywa(Midomo,ulimi,meno),Nywele,n. K

◾Mikono Ina viganja,viwiko,vidole na kucha..

◾Kiwiliwili Kuna Tumbo, Moyo, Ini, mbavu, njia za haja kubwa na ndogo n. K....

◾Miguu Ina mapaja, magoti, ugoko na kanyagio

👉Hivi vyote vikiunganishwa huitwa MWILI( mmoja/moja) unaotokana na Viungo vingi, kwahiyo Viungo hivyo vinapata sifa ya Kuitwa MWILI/BODY kwa sababu Viungo hivyo vimesababisha uwepo wa mwili na bila Viungo hivyo huyo kiumbe mkubwa MMOJA mwenye Viungo vingi akikosa hivyo Viungo hawezi kuwepo, hakutokuwepo kitu kiitwacho MWILI.

👉Kwa mfano Kichwa Kikijiona chenyewe kuwa ni mkuu kuliko Viungo/sehemu zote za mwili, Ebu fikiria Tumekikata kichwa Kisha tukakiweka pembeni, Sasa JE Kuna yeyote atakiita kichwa kuwa ni MWILI? Kwa hakika hapana Bali jamii itasema "HIKI NI KICHWA CHA MWILI WA BINADAMU" Kwamba tayari kimepoteza sifa ya kuwa MWILI. sijui mfano huu ninaeleweka?

👉Sasa hata Katika Dhana(nadharia) ya Mungu, we are all gods and Goddess. Kwamba sote ni Mungu wa kike kwa kiume, Na kitenda wili na Fumbo la Imani ni Kwamba tunafikiri sisi ni tofauti kwa kutazama mwonekano wetu wa sura za nje, kumbe sisi sote ni mmoja yule yule kivipi?

👉Anaitwa THE ONE Yani MMOJA, sindio MUNGU ni mmoja kwa mujibu wa Imani/Dini yako? Sasa sisi sote Kwa pamoja ni KIUMBE MMOJA MKUBWA (MUNGU) hatembei, haendi mbele Wala nyuma Bali yeye ni UFAHAMU (consciousness) mmoja tu yupo tuli/ametulia. Kwamba tunaona sisi ni viumbe tofauti tunaofanya kazi tofauti mfano Huyu anakula, yule analima na Mwingine anaendesha Gari na yule Amelala... Lakini kumbe ni Kiumbe MMOJA tu anayeyafanya hayo yote kwa Pamoja. Ukiingia kwenye injili ya Siri iliyofichwa na kutolewa kwenye biblia na msahafu iitwayo injili ya Yohana(THE SECRET GOSPEL OF JOHN) utamuona huyo THE ONE ameelezewa kwa uzuri kabisa humo

👉Tukirudi nyuma nilisema sheria namba moja Katika sheria za ulimwengu(universal laws) iitwayo "Sheria ya umoja wa Mungu(THE LAW OF DIVINE ONENESS) inasema kila kitu kimeunganishwa na kitu kingine hivyo hakuna utengano Kwa sababu kila kitu ndani yake kina Chanzo ambacho ni nishati/energy ama Katika Dini huiita " ROHO" na uzuri Wana Dini pasipo shakha huamini Mungu ni Roho ijapokuwa Huwa hawajui kuwa wanaomtafuta nje yumo ndani yao kwani sisi sote ni viumbe vya Kiroho tunavaa hii miili yetu ya kifizikia kwa Kusudio maalumu Kwamba tupo Katika ulimwengu wa utashi wa chini(3D) ili kukuza Ufahamu wetu ili tushift/tuhame kuelekea Katika ulimwengu(Dimensions) za juu zaidi na tusiendelee Kuzaliwa hapahapa Duniani, ni muhimu kutambua kuwa neno KUFA halipo Bali tuseme kushift frequence(kubadili mwonekano wetu na hata mazingira Kwa sababu nishati/nguvu/energy can neither be created nor destroyed Yani nishati(Roho) haikuumbwa na Wala Haina mwisho(haifi),Ndiomaana tunasema Universal energy au Cosmic energy ndiye muumbaji Yani MUASISI WA VITU VYOTE, Yaani Alpha (zero Quantum Energy)

✍️Wewe mgeni, wewe MTU wa Dini Ebu jiulize maswali haya machache Tena jiulize ukiwa mbele ya kioo, fanya hivi👇

◾Kaa mbele ya kioo chako...
◾Ongea na mtu aliye mbele yako anayefanania na wewe kwa 100%
◾Jiulize Mimi ni Nani?
◾Hizi nguo nilizo zivaa ni za Nani? Hakika utajijibu kuwa ni zako lakini ukitambua kuwa wewe sio hizo nguo.
◾Jiulize huu mkono ni wa nani, hakika unauakika kuwa ni mkono wako huo Ila unajua kuwa wewe sio huo mkono,
◾Jiulize Tena huo mwili unaouona Katika hicho kioo ni WA Nani? Kwa ufasaha akilini utajijibu kuwa huu ni MWILI WANGU, Sasa kwanini Automatically unajitenga na huo mwili?

Sasa swali Kama huo ni mwili wako, JE wewe ni Nani, wewe ni kitu gani haswa❓

Jitafute..... 🚶

Somo litaendelea......

Imeandikwa na Dogoli kinyamkela... ✍️

Kalibun jijini Whatsapp 👇🏼👇🏼

 
Kumfanya mtu asikufuatilie basi tafuta kichupa kidogo urefu wa kidole kisha weka unywele wake alafu nenda katupe kwenye maji yanayotiririka
1737728713721.jpg
 
Ukiona mgonjwa wenu kafariki ghafla basi hiki ndicho KINACHOTOKEA

Huwa wanachukua udongo wa kaburi kisha wanaweka chini ya kitanda cha mgonjwa

Wakiwa na lengo la kupoteza maisha yake

Wanachukua udongo wa upande wa kushoto wa kaburi yaani sehemu ya moyo wa marehemu hapo ndipo wanachimba na kuchukua udongo kwa mkono Baada ya kuchimba ndipo wanaweka chini ya kitanda cha mgonjwa
1737748644699.jpg
 
MWANZO MPAKA UFUNUO NI SISI
Sehemu ya kwanza (1)

Imeandaliwa na kuandikwa na Dokta Dogoli kinyamkelaView attachment 3200051

Hiki ndicho kinachotokea Sasa ukiwa kwenye nafsi ya chini ( lower self), ambayo inaingozwa na dini, Katiba, makanisa, misikiti, Pamoja na mashirika mengi ya kijamii ambayo yenyewe yapo kwa ajili ya kukutia hofu.na kufanya Uzidi kujiona wewe Ni wa chini tu.
Nakuonea huruma sana; kwa sababu misingi ya yote unayoongea humu mimim nayafahamu sana. Siku nikipata nafasi nitakutafuta; itakuwa ni miaka kadhaa ijayo mbele; unaweza ukatimia hata muongo mmoja. Nitakutafuta
 
Hivi kwa nini meditation inakuwa link sana na dini za buddhism na hinduism na sio sana kwa Abrahamic religions
Catholic pia wanafanya sana meditations, mfano zile sala za ekàristi, Gregorian chants, hata zile order za monks na friers kama Franciscan monks/friars, Benedictines, Cappucins nk. Wanafanya sana Meditations
 
Mwendelezo ,somo la meditation.

Uzingativu paji la uso.

Katika utulivu unaoendelea kuupata,endelea kuzingatia kwenye paji la
uso,Endelea na kuendelea,
Sasa iache Pumzi na hata usiisikie Tena ,yaani sahau kama unapumua,Bali zingatio lako liwe kwenye paji la uso.
UTAONA mwili unaanza kama kufa Ganzi,endelea na Hali hiyo,kadri unavyoendelea
,UTAONA mwili wako unayeyuka ,unakuwa huuoni Tena mwili ,hujioni ,hata mahala/ramani ulipo huioni kiakili.

Wengine baada ya utulivu mkubwa huanza kuona miale ya Mwanga,Mwanga mkali ,viumbe mbalimbali,wewe endelea na utulivu.

Katika hatua hii ya meditation ,endelea kuwepo katika hatua hiyo ,endelea kuvuna mitetemo katika Hali hii,hakikisha ufahamu wako ndio unaona/umewaka.
Huu ni ufahamu wa nje ya maumbile/mwili.
👇👇👇
Faida za kufanya meditation ipasavyo.

👉machale yako yanakuwa ya juu sana/mitetemo/intuition.
Yaani unaweza ukaifikiria pesa na ikaja muda huo huo,ni vyema kuwaza yaliyo mema,kwa maana ukifikiri lililo baya litakupata.

👉kujiponya mwenyewe.
Meditation inaponya,pale Kundalini inapoamka ,uzima hupatikana ,chakra zako zinapofunguka hakuna ugonjwa utakao Baki ndani yako/utajiponya mwenyewe.

👉kuwa mtu wa maono.
UTAONA Kila kitu katika ulimwengu wa kiroho na asilimia kubwa vitatokea katika ulimwengu wa mwili.
Hapa ndipo tunapokuja kupata waonaji wa kiroho,Manabii na watu wenye karama mbalimbali hii ni kwa sababu ya utulivu huo.

👉kuwa mponyaji.
Unapofikia level za juu (kutembea katika nguvu ya Mwanga na Sauti).
Wewe unakuwa mponyaji ,hakuna kitu kitakushinda ,unakuwa mponyaji wa Ulimwengu,utaponya watu ,utaponya wanyama na vitu vyote vinavyokuzunguka.

👉kutokufa/kuishi milele.
Unapokuwa unafanya meditation ,unakuwa unajiwasha ndani mwako na hatimae kujua wewe ni nani katika ulimwengu huu,na kukamilisha kusudi lako.hivyo kufanya kutokuzaliwa Tena katika maumbile.

Hizo ni baadhi tu ya faida za meditation,ila faida zipo nyingi sana.
 
Kutoka nje ya mwili/Astral projection.

Ni kitendo Cha kutengana na mwili wako huu wa nyama.

Ni kile kitendo Cha mwili wako wa ndani kutoka nje ya mwili.

Kutoka nje ya mwili hufanyika kwa Namna mbili
Moja kujiandaa kwa kutulia kwenye utulivu.

Mbili ni kupitia kwenye ndoto.

Utokaji huu wa kupitia utulivu,mtu huweza kutoka nje ya mwili na kwenda mahala popote pale,huku akijua kabisa kuwa nipo nje ya mwili na kuuona mwili wake wa nyama ulipolala.

Tendo hili ni moja ya Namna ya kuiimarisha kiroho ,japo Sio Lazima kutoka nje ya mwili

Watu wengi hutaka kutoka nje ya mwili lakini hushindwa ,kutokana na kukumbana na kadhia ya maumivu ya mwili kama kudhani anakabwa na jinamizi ,kumbe ni dalili ya kutoka nje ya mwili,

Ukiweza kuivumilia Yale maudhi kwa sekunde 10 tu,utaweza kutoka nje ya mwili,ukifanikiwa kutoka nje ya mwili ,unashauriwa kutokwenda mbali kwa wale wanaoanza.

Tendo hili la kutoka nje ya mwili SI chochote katika utambuzi wa kiroho,kwa maana mwili huu wa ndani ,bado ni Mwili wa maumbile uliojishikiza katika mwili huu wa nyama.

Kwa hiyo utokaji huu upo wa aina mbili kama nilivyokwisha kusema ,watu wengi hutoka nje ya mwili bila wao kujua kupitia ndoto za usiku.

PInahitaji mazoezi ya kutosha ili kuwa mzoefu wa kutoka nje ya mwili.
 
Mimi nikijaribu kufanya Meditation akili inagoma kutulia kabisa adi nashindwa kuona chochote 👉 msaada nifanyaje ili akili itulie sehemu moja ?
 
SEX ENERGY CULTIVATION.
SEHEMU YA 02.
🤜Na Dogoli kinyamkelaView attachment 3202727

👉Kutoruhusu kumwaga mbegu zako either kwa kujiepusha na mapenzi au punyeto kwa muda mrefu haimaanishi kuwa umeweza kuivuna nguvu hii muhimu ya ngono, hapo ulichofanikiwa ni kuzuia nguvu zako za ngono kupotea.

👉Nishati ya ngono huhifadhiwa kwenye korodani (Testis) kwa wanaume, inaweza kuwa katika hali baridi au hali ya moto, nishati baridi ni nzito kuliko nishati moto, lakini kiujumla nishati ya ngono ni nzito kuliko nishati zingine.

👉Wanafizikia wanatuambia viyoyozi huwekwa juu na sio chini kwa sababu hewa baridi ni nzito kuliko hewa ya joto, kwa hiyo ni lazima tu hewa baridi itashuka chini kwa sababu ya uzito wake.
Kwa hiyo hata katika mwili, nishati ya ngono haiwezi kujipandisha yenyewe kwenda juu, kichwani ni jukumu lako kuipandisha juu nishati hii ili uweze kupata mwamko wa kiroho na faida zingine kede kede.

👉Baada yaTafiti za kisayansi kuhusu tiba za sindano (Acupuncture) ilipendekeza kwamba, mifereji ya nishati (Energy Channels) hupatikana maeneo kunakopatikana mishipa ya damu na neva kwa wingi (blood vessels and Nerves endings) katika mwili.

👉Sasa ili uweze kupandisha nishati hii, kwanza inakupasa ufungue mifereji ya nishati na sakiti ya mzunguko mdogo wa ndani (-Microcosmic Orbit-) ya mwili.
Nishati hutiririka katika mifereji mikubwa na midogo katika mwili, wataalamu wa sindano za tiba(/Acupuncturist) Hutambua kwamba mfereji mkuu wa nishati umepita katika uti wa mgongo, vivyo hivyo Sakiti ya mzunguko wa nishati huanzia kwenye kwenye msamba, hupanda juu kwenye uti wa mgongo hadi kwenye kichwa kisha hushuka mpaka kwenye kitovu na kumalizikia kwenye msamba(perinium).

👉Upumuaji unaojumuisha uchezaji wa korodani, husaidia kufungua mifereji mbali mbali ya nishati na kuunda sakiti ya mzunguko wa nishati mwili.
Baada ya kufanya Mazoezi ya upumuaji unajumuisha uchezaji wa korodani, nishati baridi ya ngono huanza kupandishwa juu kuelekea kichwani kupitia njia ya mfereji mkuu wa nishati ulipita katika uti wa mgongo,

👉kinachopandishwa juu sio mbegu za kuime bali ni nishati, Nikola tesla hakua mjinga alivyosema "If you want to find the secrets of the universe, think in terms of energy, frequency, and vibration" akimaanisha kwamba "Ikiwa unataka kupata siri za ulimwengu, fikiria kwa misingi ya nishati, masafa, na mtetemo." Baada ya kuielewa nukuu hiyo ndio ulikua mwanzo wangu wa kujifunza ni kivipi kila kitu kimeundwa kwa nishati, hivyo sikukurupuka kuanza kuchambua Ngono/penzi katika mtazamo wa nishati.

👉Mwanaume ukisisimka kingono, nishati moto ya ngono huzaliwa, katika fizikia, nishati ya "kinetic" huzalishwa pale tu mtu au kitu chenye uzito kitakapo kuwa katika mwendo, seli za mbegu za nguvu za kiume (Sperms) huwa katika speed fulani pale unaposisimka na nishati huzaliwa.
Kwa namna hiyo, hivyo ndivyo nishati ya ngono huzaliwa, na nishati hiyo either ikiwa baridi (Yin energy) au moto (Yang energy) hutakiwa kupandishwa juu kupitia mfereji mkuu wa nishati uliopo kwenye uti wa mgongo, kwenye uti wa mgongo hutambuliwa kama mfereji mkuu wa nishati sababu ya wingi wake wa neva, neva zote za mwili hutokea hapo. Na usisahau kwamba taarifa hupita kama charge za umeme katika mfumo wa neva, hivyo kuzaliwa kwa nishati.

👉Nishati ya ngono huzaliashwa kwenye korodani, sehemu ambapo mbegu za kiume hutengenezwa, zikianza kupandishwa juu hufika katika eneo la "hiatus" mwanzo wa mfupa wa "sacram" sehemu hii huchukuliwa kama pampu, inayosukuma nishati ya ngono ili iweze kupanda juu kwenda kwenye ubongo, pia kwenye ubongo kuna pambu ya cranium ambayo huirudisha nishati chini.

👉Iwapo kukawa na kizuizi katika pambu hizi mbili, basi nishati hukwama kupanda juu, na mazoezi ya upumuaji wa uchezeshaji korodani (Dance of the Testis Exercise) husaidia kufungua vizuizi hivyo. Imethibitishwa kitaalamu kwamba, Mijongeo midogo ya Jointi za mifupa ya "cranium" ya nane hutokea pale tu unapopumua, haswa haswa upumuaji wa uchezeshaji korodani.

👉Upumuaji huu huimarisha jointi za mifupa ya cranium, hivyo kusaidia uzalishwaji wa kimiminika cha "cerebrospinal fluid" ambacho ni muhimu katika utendaji kazi wa neva na mtiririko wa nishati. Kuimarika kwa jointi za mifupa husaidia kupunguza na kuondoa maumivu makali ya kichwa yasiyotibika (i.e migraine headache, matatizo ya shingo na matatizo ya uoni ) uponyaji huu hutokea baada ya kuimarishwa utendaji kazi wa neva.

👉Wiki hii ntakua free kidogo, hivyo mjiandae kwa elimu kuhusu mazoezi ya upumuaji ili muanze kufungua mifereji ya nishati iliyofungwa na kutengeneza sakiti ya mzunguko wa Nishati.
Hiyo ni hatua ya awali ya kupandisha nishati ya Kundalini kama inavyojulikana katika tamaduni za kihindu.
Be humble, jiepushe na umwagaji usio na faida, kisha tutamaliza na namna ya kubadilishana nishati ya kike (yang energy) na nishati ya kiume (yin energy) /Ying yang ☯️ balansing kwa kutumia ngono takatifu.

ITAENDELEA....
✍️ Dogoli kinyamkela Is Always Dogoli kinyamkela
Be humble Just stay connected with Me, stay connected with Us, The serpent Bloodline serpent 🐍
Mkuu muendelezo wa hapa tuletee kama inawezekana lakin
 
Duh!
MEDITATION 🧘
🗣️Watu mbalimbali wamekuwa wakianza kupata ufahamu juu ya meditation na wengine tayari wameshaanza kujifunza kufanya kitendo kicho.

🧘🏾‍♀️Meditation ni kitedo cha muhimu kwani kina faida kubwa na wengi waliojitolea muda wao kujifunza meditation (mfano mimi), wamenufaika na meditation.

🗣️ Mwalimu wako Dogoli kinyamkela Nimeona nielezee katika Uzi huu View attachment 3200053na ninaamini itawasaidia wengi wambao wangependa kujua.

***

✍️Kwanza kabisa, kabla ya kufanya meditation ni kufahamu lengo la meditation ni nini, ni muhimu ukufahamu akili ni nini, inafanyaje kazi, energy zinazomzunguka mtu, utambue vyema baadhi ya maelezo ambayo yatasaidia mtu kujua uelewa kidogo kuhusu meditation.

👊Kutambua hivyo itakusaidia kufahamu jinsi meditation inavyofanya kazi katika ufahamu.

👉Tukianza na sababu ya meditationa ni kuweza kufahamu akili yako inavyofanya kazi, kujiepusha na mateso/shida ndogondogo, huepusha hasira, hukupa uwezo mkubwa wa kuwa m'bunifu mfano kama wewe ni mchoraji, mwanamuziki n.k, inakusaidia kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yako.

✍️ Na kama utaweza kuwa na maamuzi mazuri katika choices mbalimbali katika maisha itakusaidia sana kwani msingi wa maisha ni choices tunazoweka kila siku na kila saa.

🧘🏾‍♀️ Ukishaweka nia sahihi juu ya meditation kinachofuata ni kufahamu nini kinatakiwa kiwepo kabla ya kufanya meditation. Pia katika imani nyingine kama Wahindi na Wabudha, viongozi wao wa imani wanapata nguvu ya kiimani, ufahamu na wanafunuliwa jicho la tatu kupitia meditation.

🤔 Hata sayansi nayo inaamini Enlightenment inaweza kutokea katika meditation na kumfanya mtu afunguke kiimani.

🧬 Meditation inabadili mpaka DNA na kumpa mtu enlightenment (Ipo siku nitaelezea experience/hali ya enlightenment inakuwaje).

Kuandaa Sehemu ya Meditation.

🧘🏾‍♀️Andaa sehemu nzuri na maalum ambayo utakuwa unafanya meditation.

🛕Mfano inaweza ikawa chumbani unapolala, chagua sehemu au eneo ambalo utakaa chini vyema bila usumbufu, penye hewa nzuri na safi (fresh air), penye hali ya hewa cool au ya kawaida.

🗣️ Ni vyema kuchagua sehemu ambayo hauitumii kwa shughuli nyingine au mfano ukiwa haupiti sana eneo hilo au huweki vitu unavyotumia eneo hilo.

✍️ Ni kwa sababu itapunguza kuwazawaza pale utakapokuwa unataka kunyamazisha akili, inaepeusha kumbukumbu za eneo hilo kuja wakati wa meditation, pia ni vyema kwani meditation ni kama sala, ni kitendo kisafi hivyo ni vyema eneo la kufanyia sala na meditation kuwekwa katika hali nzuri.

📚Ukishachagua eneo unaweza ukaweka vitabu vyako vya imani katika eneo hilo, inategemeana na imani yako.

🥼 Halafu ukishamaliza kinachofuatia tafuta mto wa kukalia ambapo utaukalia. Tafuta mto mzuri ambao ukiukalia hautaumia (kwani utakuwa unakaa kwa muda mrefu). Halafu tafuta nguo za kuvaa ambazo hazibani na zilizo comfortable.

🧘🏾‍♀️Chagua wakati maalumu ambao utakuwa unameditate. Ni vyema kutumia dakika 20 na kuendelea katika kumeditate. Pia meditate kila unapoamka na kila kabla ya kulala.

🧘🏾‍♀️ Baadaye utakapoweza kumeditate vyema utaweza hata kumeditate kwa dakika moja katika kila lisaa.
Ukishajianda hivyo kinachofuatia ni kukaa na kumeditate.
🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️

👆👆 Huo hapo juu kwenye hizo emoji nilizoziweka ndiyo mkao ambao utakaokaa wakati wa kumeditate

👆Huo ni mkao mzuri katika meditation kwani una faida zifuatazo.

🧘🏾‍♀️Unakusaidia damu kuzunguka maeneo ya juu ambapo ndipo sehemu zenye umuhimu katika meditation, zinasababisha energy kutoka kwenye dunia kupitia kwenye uti wa mgongo na kukupa utulivu wakati wa meditation, pose linasaidia chakula kumeng'enywa vyema kutokana na damu kuwepo katika utumbo mdogo vyema.

🗣️Ni mkao mgumu kukaa, mwanzoni miguu huwa inakufa ganzi kutokana na kubanwa lakini amini nakwambia ukijilazimisha baada ya muda mfupi maumivu yanaisha kabisa na unaweza kukaa muda mrefu sana bila kuumia kabisa.

Kuanza meditation

✍️ Ukiwa umeshakaa, kinachofuata ni kuanza meditation. Ukishakaa, relax hakikisha kila kiuongo kimerelax, unganisha mikono yako ubebane pamoja, hisi upendo mwilini mwako, shukuru kwa afya uliyonayo, shukuru kwa jinsi mwili unavyokulindia roho yako iliyohifadhiwa na mwili, hisi furaha, peace, and love within. Halafu vuta pumzi kubwa tano. Vuta pumzi ndani taaaaratibu, halafu pause kidogo then toa pumzi njee.

✍️ TAARATIBU TENA. Wakati huo weka mawazo kwenye pumzi. Baada ya kuvuta pumzi kubwa tano endelea kuvuta pumzi kikawaida huku ukiweka akili kwenye pumzi inavyoingia na kutoka.

🧘🏾‍♀️Unaweka akili kwenye pumzi kwa lengo la kutoweka akili kwenye mawazo. Akili ya mwanadamu haiwezi kukaa bila mawazo. Unapomeditate unaweka wazo kwenye pumzi tu, unaangalia jinsi pumzi inavyoingia na kutoka na kufeel energy inayoingia na kutoka mwilini. Uwe umefunga macho.

🗣️Ni vigumu kwa mara za mwanzo kwa sababu, ni vigumu kutuliza akili katika wazo moja kwa muda mrefu ila we jitahidi kufocus kwenye pumzi tu. Baada ya muda, wakati hauwazi wala haufuati kinachokuja akilini ukiwa unaweka mawazo yako katika kutazama tu jinsi pumzi inavyoingia na kutoka mwilini utaanza kuhisi umeme unakuzunguka mwilini, au kichwa kinakuwa kizito, au umeme unapanda na kushuka kwenye uti wa mgongo na utaanza kuhisi mwili mzima umerelax, hapo utakuwa katika hisia ya meditation. Ni hisia nzuri maana zinakufanya unarelax na mwili unajitengenezea umeme wake.

Asili kweli imejaa mafumbo
by Dogoli kinyamkela

🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️🧘🏾‍♀️

DIBAJI
Mshana Jr
 
Back
Top Bottom