bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 754
- 1,747
KWANINI WATU WANAKUNYWA POMBE? JE POMBE INA FAIDA NI HATARI KWA AFYA?
Pombe (ethanol) ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi duniani, lakini ndani ya mwili wako hufanya kazi kama kemikali yenye nguvu inayobadilisha namna ubongo na mwili vinavyofanya kazi. Hii ndiyo sababu mtu akinywa hubadilika haraka kutoka utulivu hadi kulewa, kucheka, kutukana au kuyumba.
POMBE NI NINI MWILINI?
Kitaalamu, pombe ni kemikali inayoitwa Ethanol. ambayo inaingia mwilini kupitia tumbo, kisha utumbo mdogo Inaenda moja kwa moja kwenye damu hadi ubongo
HATARI ZA POMBE MWILINI
Pombe si chakula ni kemikali inayoweza kuathiri mwili kwa kiwango kikubwa. Kwanza inaanza na ubongo hupunguza uwezo wa kufikiri na hupunguza maamuzi sahihi, kisha kwenye Moyo na Ini huathiri ini (liver damage) na huongeza hatari ya presha na magonjwa ya moyo.
Lakini inachochea Tabia hatarishi kama kupata ajali, kuanzisha vurugu, kufanya maamuzi mabaya, kuwa mlevi wa Kupindukia (addicted) , kuharibu Ini na hata kupelekea matatizo ya akili.
JE POMBE INA FAIDA YOYOTE?
Kwa kiwango kidogo sana Pombe inaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo (relaxation) baadhi ya tafiti zinaonyesha inaweza kusaidia moyo kwa kiasi kidogo ndomaana utasikia nina mawazo sana ngoja nikanywe pombe nitulize Akili Kidogo 😄. Lakini: faida zake ni ndogo kuliko hatari zake zikizidi matumizi
KWA NINI MTU AKILEWA ANAYUMBA-YUMBA?
Hii ni kwa sababu pombe inaathiri sehemu ya ubongo inayoitwa Cerebellum. Sehemu hii ndani ya ubongo kazi yake kubwa ni kusimamia uratibu wa mwili sasa pombe ikiingia hapo inachanganya signal za ubongo matokeo yake miguu hushindwa kubalance na kuanza kuyumba yumba (hii ndio sababu wakuu)
KWA NINI MTU ANATUKANA AU KUONGEA BILA KUJIZUIA?
Pombe pia ikifika Katika ubongo huathiri sehemu ya ubongo inayoitwa Prefrontal cortex. Sasa sehemu hii nayo ndiyo “control center” ya tabia za mwili. Sasa ikizimwa kidogo tu mtu hupoteza self-control anaanza kusema au kuongea vitu ambavyo kawaida angeficha
Ndiyo maana anaanza kutukana, anacheka hovyo, anatoa siri zake au za watu na anafanya vitu vya ajabu anaweza kujisaidia hata mbele za watu bila aibu
KWA NINI WENGINE HUONGEA “KINGEREZA” WAKILEWA?
Hapa sasa ndo pazuri unamkuta mtu anapiga yes no kama kaenda shule 😄 ila Hii si kwamba anajua lugha mpya hapana ni kwa sababu ubongo unatoa vizuizi (inhibition) Sasa mtu anajaribu kuiga au kusema alichowahi kusikia mahali, kwahiyo ni confidence ya uongo wala hana huo ujuzi na pombe ikiisha hata hiyo Yes no mara bring me water inaondoka 😄
JE,KAMA POMBE NI HATARI, KWA NINI HAIPASUI CHUPA?
yupo mlevi mmoja aliwahi kuniambia kama tunasema pombe ni hatari mwilini kwanini isinge pasua chupa?😄
Swali kali sana japo alilewa ila ukweli ni kwamba pombe si gesi, ni kioevu na haina pressure ya kulipuka na zile chupa zake zimeundwa kubeba kioevu salama.
Kwahiyo uhatari wa pombe upo ndani ya mwili sio Kwenye chupa.
Je kwanini pombe inakimbilia chini? Mtu anapata hamu na nguvu ya kufanya mapenzi? Na je Kwanini inatoa kitambi na je imeandikwa asitumie kwa mtu chini ya miaka 18 mfano kwa bahati mbaya mtoto amekunywa nini kitamtokea?
muendelezo wa pombe episode 2 kazi mnayo 😄