Bila shaka unaongelea Miti ya Korosho ile ya Kizamani.Umbali kati ya Shimo na Shimo ni 12M .Eka moja wastani miti 30
Umbali kati ya Shimo na Shimo ni 12M .Eka moja wastani miti 30
Ubarikiwe sana mkuu.
Waweza kuniunganisha hapo ulipo nunua namimi nikanunue?Asante sana..kuna mtu kanishawishi niingie kwny hiki kilimo kulikuwq na fursa ya kununua mashamba mkoa wa Lindi kwa sh 50,000 kwa heka nimeshalipia eka 20,wiki ijayo nataka niende huko nikaone eneo na nianze matayarisho.
Tuendelee kujuzana kuhusu hili suala.
Mkuu Lumumba asante sana kwa taarifa kwa kweli nimekuwa nafuatilia sana mada zako especially kwenye zao la korosho na nimekuwa interested sana najaribu kukusanya data maana nataka nifanye uwekezaji mkubwa sana kwenye hilo zao kwa kuanzia kama heka 100 swali langu je kwa tanga kama nitapata eneo na nikafanikiwa kulima wanunuzi wanakuja maeneo hayo au ndio mpaka tusafirishe kupeleka kusini au pwani na calcurated risk ya hili zao ni zipi
HABARI,
"mahavanga,
Hujakosea kwa kipimo chako hicho nakubaliana na wewe kabisa hata ukitaka miti 20 kwa heka inawezekana ,Kama umefatilia post zangu zote nilieleza vema,Kama mkulima anafanya kilimo cha mchanganyiko na mazao mengine kama mahindi,mtama,ufuta alizeti n.k ni sawa ila kama ni zao la korosho tu ni matumizi mabaya sana ya aridhi sana mita 12 duh.
Ndugu mikorosho ya kubebeshwa na ya kisasa huwa haitanuki sana nitatuna picha moja kutoka mahali mkorosho wa miaka 10 haujazidi mita 3 upana kwa kila upande na kila mwaka wanavuna zaidi ya kilo 20 kwa mti mmoja hapo ndani ya mita 12 zako umeacha mikorosho miwili inayoweza kupandwa Hapo kati na bado ungeweza kupanda mazao mafupi kama maharage N.K.
Unaweza kupanda idadi kubwa ya miti kwenye heka moja baada ya mika 10 na kuendelea inapozidi kubanana ndipo unapunguza mmoja mmoja ila tayari mti unakuwa umeshakupa mavuno kwa zaidi ya miaka 10 haingii akilini uwache eneo wazi kusubiri miaka 20 ibanane Duh Tusipende kukariri lazima tujiongeze tufate maelekezo ya pembejeo ila kuna mambo mengine lazima kujiongeza, India kati ya nchi zinazoongoza kwenye kilimo hicho kwa heka moja wanapanda mpaka miti 150-200 sasa wewe ndugu ukisema miti 30 Tusibweteke na aridhi tuliyokuwanayo tuangalie kuwekeza sehemu ndogo unavuna kikubwa.TEKNOLOGIA.TECHNOLOGY
LUMUMBA
Ndugu PatriceLumumba juzi waligawa miche nimepata miche ya kutosha shamba langu la ekari 5 miche 150 hii inayogawiwa huko lindi, swali ni je niipande hiyo hiyo au nitafute hii ya kubebeshwa? Mawazo yangu yananiambia kama nipande miche hiyo hiyo halafu niandae kitalu changu nibebeshe mwenyewe halafu nipande katikati ya hii ambayo inatangulia ili ku-Maximize profit niweze kuingiza mpaka miche angalau 80 kwa kila ekari je nakuwa nipo sahihi? naona kama msimu huu nikingojea ya kubebeshwa naweza chelewesha malengo hasa ukizingatia gharama kuinunua nataka kuminimize cost kwa kuiotesha mwenyewe na kuibebesha mwenyewe somo kwenye videos zako limenikaa vyema,HABARI,
senyaba,
Karibu niwie radhi kwa kuchelewa kukujibu majukumu yalibana.Hongera kwa kwa uamuzi uliochukuwa huo ni uwekezai mkubwa sana na nimefurahi uliposema kwa kuanzia kwa hiyo una mipango ya zaidi ya heka 300 hongera.Tanga ni kati ya maeneo ya kwanza kabisa kwa ulimaji wa korosho kwa ujumla pwani yote ya bahari ya Hindi kuanzia Mtwara mpaka Tanga korosho inakubali kwenye hilo usiwe na wasiwasi na kuhusu wanunuzi hilo nalo halina shida kuna vikundi vingi vya ushiriki wewe utachagua kikundi cha kujiunga na wanunuzi ni wale tu watakaopitishwa na Serikali Nenda ofisi za mkuu wa mkoa wana taarifa zote pale.Kwa upande wa risk kweli zipo hakuna kitu kisicho na risk mojawapo ni kununua mbegu kwenye vyanzo visivyo thibitishwa hili unaweza kukuza mti usio na ubora tafuta vyanzo vizuri vya mbegu.
LUMUMBA
Lumumba nakuelewa sana aise! Naandaa maswali yangu 12 yakuuliza kesho! Naamini utanipa majibu yenye ujazo
Ubarikiwe sana aise..
Asante Lumumba, kila mtu niliekuwa namconsult alinipa hesabu ya miche 28 hadi 30 kwa ekari, hadi nikapata shamba la ekari 4 hapo mtwara nikapiga hesabu zangu nikaona ni dogo sana kwani nitavuna kiasi kidogo cha korosho.
Ningekuwa nimepata majibu kama haya na maelezo yaliyoshiba i would have decided otherwise. Nimeshangaa kuona inaweza kufika miche zaidi ya 3000 kwenye hizo ekari kumbe kwa maelezo niliyokuwa nayo mwanzo hapo hata miche 1000 haingeingia shambani.
Asante sana
Duh aisee mkuu, umeona mbali sanaAsante sana mkubwa kwa jitihada zako za kutuelimisha na kuhamasisha ukulima huu wa korosho,
Samahani nina swali ambalo lipo nje kidogo na mada yako ya leo,ni hivi kuna taarifa kuwa sababu ya korosho yetu kuwa na soko ni kwa kuwa inatoka msimu ambao duniani kote hawavuni.
Je, ni habari za ukweli?ikiwa ni kweli vipi mikoa mingine ambayo ndo kwanza wanahamasishwa kulima? Nao itatoka msimu mmoja na korosho za kusini?
Nimependa hapo uliposema.
Duniani hakuna kuchelewa hadi unaingia kaburini..nami naongezea "utakachokifanya hapa duniani siyo lazima ukifaidi wanaweza kufaidi Hata wanao"
Wana jamvi! Nataka kuanzisha shamba la korosho la ukubwa wa 32 acres! Naomba wenye utaalaam na kilomo hiki wanijuze juu ya hatua muhimu za kuzingatia tukianzia na kusafisha shamba kwani kwa sasa ni msitu kabisa ambao haujawai limwa chochote!
Pili garama mbali mbali kwa kila hatua na any other information ambayo unadhani itanisaidia!
Natanguliza shukrani!
Wana jamvi! Nataka kuanzisha shamba la korosho la ukubwa wa 32 acres! Naomba wenye utaalaam na kilomo hiki wanijuze juu ya hatua muhimu za kuzingatia tukianzia na kusafisha shamba kwani kwa sasa ni msitu kabisa ambao haujawai limwa chochote!
Pili garama mbali mbali kwa kila hatua na any other information ambayo unadhani itanisaidia!
Natanguliza shukrani!
HABARI,
"fungafunga,
Ndugu Hongera Tena kwa kuwa na kiasi hicho cha shamba kwani kama ukifanikiwa kupanda shamba lote unauhakika wa kuwa na miti sio chini ya elfu 3 ambacho ni kiasi kikubwa sana kwa kuanzia.
Nakushauri upande mikorosho iliyo bebeshwa kwani unaweza kupanda idadi kubwa kwenye shamba dogo pia inauvumilivu mkubwa wa magonjwa na inatoa mazao mapema.
Kwa kuandaa shamba ukisha safisha nivema kama mengi ni majani itakuwa vema kama ukiyachoma moto huwa inasaidia kuangamiza magojwa mbalimbali yaliyokuwa kwenye mimea hiyo ya mwanzo.
Umbali kati ya shimo na shimo unaweza kuweka kati ya mita 5-6 na umbali kati ya mstari unaweza kuweka mita 6-7,
kwa vipimo hivyo unaweza kuwa na mashimo 100-120 kwa heka moja.
Na uchimbaji wa mashimo unaweza kuchimba sentimeta 50 kwenda chini na upana wa sentimeta 50,Ni vema udongo wa juu nusu ya shimo yani sentimeta 25 ukautenga na ule wa chini wa sentimeta 25,Huu udongo wa juu utautumia kuchanganya na mbolea ya samadi wakati wa kupanda mmea.
Inashauriwa kupanda mmea wakati wa mvua na kabla ya kupanda changanya ule udongo na mbolea na kuacha kwa wiki mbili ili kuwezesha samadi kuchanganyika vizuri na udongo ndipo upande mmea.
Wakati wa kupanda unashauriwa kuweka ule udongo uliochanganya na samadi ujae robo ya shimo ndipo upande mmea wako na na wakati wa kufukia fukia nusu ya shimo kwa utaratibu huo utakuwa umefukia shimo lako na mmea kwa robotatu hiyo itasaidia kuacha eneo la maji kutuama wakati wa mvua au wakati wa kumwagilia na pia mmea kupumua vizuri.
Hii nimekupa picha kidogo juu ya maandalizi hayo ila nakushauri nenda Kituo cha naliendele Nimeweka post zake kadhaa hapa na anuani zake pale utapata maelekezo mengi juu ya magojwa na tiba zake kwakuwa mradi wako unaonekana ni mkubwa huna budi kufika pale.
Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com
LUMUMBA
Wana jamvi! Nataka kuanzisha shamba la korosho la ukubwa wa 32 acres! Naomba wenye utaalaam na kilomo hiki wanijuze juu ya hatua muhimu za kuzingatia tukianzia na kusafisha shamba kwani kwa sasa ni msitu kabisa ambao haujawai limwa chochote!
Pili garama mbali mbali kwa kila hatua na any other information ambayo unadhani itanisaidia!
Natanguliza shukrani!