Jamani mmeshinda poa!
Wanawake / Mabinti baadhi wamekuwa watumiaji wazuri wa limbwata kama
sehemu ya kuongeza chachu ktk mahusiano yao ya mapenzi. Zifuatazo ni
baadhi ya teknolojia maarufu ama niseme pendwa za limbwata. Waweza
kuongeza yoyote ile uijuayo
:
Kinyama
Hii kitu kuna siku Mkuu
MziziMkavu aliielezea
vizuri tu. Katika hili, kipande kidogo cha nyama mfano wa mnofu mmoja wa
mshikaki huwekwa katika
maku ya mtaka tiba, kwa muda wa siku
kadhaa kulingana na masharti ama maelekezo ya mganga husika fundi,
baadae kinyama hiki hupikwa na sehemu nyingine ya kitoweo kama mboga na
kuliwa. Mlengwa wa limbwata ataathirika mara tu baada ya kula mlo
uliohusiha mboga yenye kinyama hiki! Wanaoipenda njia hii wanasema ni
ngumu sana kumuagua mwanaume alielishwa kinyama
Maji ya mchele:
Hii ni aina nyingine ya teknolojia ya limbwata. Ni kwamba kwa kutumia
njia hii, maji ya kawaida hupelekwa kwa mganga kwa ajili ya kazi husika,
na kisha maji hayo hurudishwa nyumbani, mwanamke mhusika huyatumia maji
ya dawa haya kuoshea
maku na baadae huyatumia kuoshea mchele ama
hata kupikia kabisa! Limbwata hili hufanya kazi kwa mlengwa baada ya
mlengwa kula chakula kilichopikwa kwa maji tajwa! Wanaoipenda njia hii
wanasema ni ngumu sana kumuagua mwanaume alienyeshwa maji hayo, na
kwamba ili kumuagua lazima apatikane fundi Yule Yule aliefanya yake!
Kisomo:
Nyingine. Hii haisemwi sana, ni kama siri kubwa, huwa haijulikani hasa
ni aina gani ya kisomo hufanyika lakini wateja na wafuasi wa limbwata
la aina hii wanakiri kuwa, mwanaume aliesomewa (msomaji ni fundi
mganga) huwa ni zaidi ya kondoo, kwa maana ya kuwa maisha yake yote
yaliyobaki yanakuwa ni yale ya ndio mzee kwa mwanamke alietengeneza!
Wanaoipenda njia hii wanasema sio nzuri sana kwa vile fundi mwingine
yoyote anaweza akafanya kisomo kinyume.
Kifaranga:
Hapa mwanamke mhitaji huagizwa na fundi kupeleka kifaranga, na mara
nyingi ni cha kuku. Fundi humfanyia kazi Kifaranga huyu katika karakana
yake, namna fundi anavodili na kifaranga hiki ndio ndio kazi halisi ya
kumuinamisha mme ama mpenzi wa mtu, kifaranga huyu hubaki ktk himaya ya
fundi kwa maisha yake yote, na namna kifaranga huyu anavolelewa na huyu
fundi, na kufuata anavotaka mfugaji, ndio hivo hivo mlengwa
atakavopelekwapelekwa! Njia hii inachangamoto moja kubwa, usalama na
uhai wa kifaranga huwa ni tatizo, na iko subjected to frequent updates!
Jina kuningnizwa juu ya mti:
Hii inafanana na kisomo. Tofauti ni kwamba, baada ya fundi kufanya kazi
yake, huku jina la mlengwa likiwa limenuiwa, karatasi lililoandikwa jina
hili (jina la mwanaume mlengwa) huenda kuninginizwa katika moja ya mti
mrefu ambao ni sharti uwe mbali na wanapoishi wapenzi ama wanandoa hao,
wakati mwingine inahusisha mkoa mmoja hadi mwingine! Wanasema
kusipokuwepo na upepo, mwanaume huwa mjanja mjanja, lkn upepo ukivuma
kidogo tu, mwanaume huyu akili huruka na kumuwaza aliemtengeneza! Ili
upone kutoka katika limbwata hili, lazima huu mti utafutwe na kikaratasi
kikatwe, ndio utapona!
Kaburi la mtoto
Hapa kuna vitu hufukiwa. Kama ilivo limbwata la hapo juu, limbwata hili
linahusisha madawa na majina ya mlengwa. Kaburi husika hutafutwa maeneo
ya mbali sana. Madawa na majina ya mlengwa hufukiwa katika kaburi la
mtoto. Hapa huponi mpaka kaburi lipatikane na kazi ifanyike hap!
Unyayo kucha ama kinywele:
Hapa kuna mchanganyiko wa ufundi unaotumika. Wapo wanaotumia mchanga wa
unyayo, wapo wanaotumia kipande cha v.u.z.i, wengine hutumia hata
c.h.u.p.i ya mlengwa, lakini yote kwa yote ni kwamba fundi atadili na
mlengwa kutumia aina mojawapo ya nyenzo hizi! Mafundi wengi inasemekana
ni wataalamu wa kuagua wahanga wa njia hii!
Kazi kwenu wapenda michepuko!