Fahamu kuhusu Uchawi wa Mapenzi (Limbwata) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fahamu kuhusu Uchawi wa Mapenzi (Limbwata)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mwiba, Mar 30, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nasikia kuwa dawa hii huwa baadhi ya wake huwalisha waume zao, na baada ya hapo mume huwa kama zuzu analoambiwa hana upinzani yaani chochote kile kutoka kwa mkewe huwa anakifuata.

  Je dawa hii mtu anaweza kumpa mkewe au kumlisha mkewe ? Na ni kweli ipo na inafanya kazi kama nilivyojaribu kusema au nilivyosikia!
  =========================
  ==============================
  =============================
  =============================
   
 2. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hakuna libwata duniani nijuavyo mimi...LIMBWATA ni wewe mwenyewe.
   
 3. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi pia naamini hakuna dawa kama hiyo. Nadhani ni concept tu ila wajanja wanaitumia njia hii kuvuna pesa za wajinga.
   
 4. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #4
  Mar 31, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hmm! kama unataka kujua kama unaweza kumpa mkeo ,kanunue then ujaribu kwake uone kama itafanya kazi,usiogope kujaribu,kujaribu ndio kujifunza kwenyewe huko.

  naona ndugu yangu mkeo amekushinda hadi unataka kumuekea madawa? mlete kwangu nimpatie limbwata origino.
  [​IMG]
   
 5. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu hamna libwata wala nini...Maneno tu hayo ya watu!!
   
 6. S

  Shingo Senior Member

  #6
  Mar 31, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 127
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Limbwata ni fikra potofu kama zilivyo fikra zingine potofu. Wapo wanaotumia fikra hii kujinufaisha na hawa utawakuta huko kwenye mitaa ya watu waliochoka wakiwa na mbango makubwa kuelezea tiba wanazo toa. Nenda kawaulize, limbwata ni mojawapo ya huduma wanayoitoa na inawapa kuendelea kuwepo.
   
 7. S

  Shingo Senior Member

  #7
  Mar 31, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 127
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  B: If the husband is the one who look for money then there is logic if some is spent on his own interrests. Men who spend money this way has motivation to look for more and are hardworkers and they usually are not only satisfied by single source of income. In fact the type of men you are discouraging are the ones who are entrepreneurs and hardworkers.

  Money earned only for wife and family is useless. MEN OR WHOEVER WINS THE BREAD HAS TO SPEND ALSO ON THEIR OTHER INTERRESTS TO KEEP GOING!!!
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  watu wanajidai lakini limbwata lipo

  watu wa kanda ya ziwa ndio mchezo wao sana wanaume/wanawake
  na kila mara mtu inabidi aka renew kwa mganga, kwa hiyo hela pia zinakua zinaenda kwa mganga. wa mama wa mjini maarufu ndio mchezo wao siku hizi hata masista duu.

  na limbwata ndio linawapa waganga hela ya kuishi mjini limbwata ni kama sigara kwenye duka kwa ajili wanasiasa ni wachache kama vijisenti, wateja wengi ni wanawake
   
 9. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Karibu uswazi,then you will know kama limbwata lipo or not.

  HII KITU IPO inaexist ,siyo hadithi na zidi kumwomba MUNGU isijepiga hodi nyumbani kwako.IBAKIE KUWA HADITHI YA KUSIMULIWA.

  KATIKA NDOA ,WASHAURI NI WENGI ATI...
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Jamani akina mama na akina dada wengi siku hizi wanaamini sana kwa mambo ya kumbana mke/mchumba/boyfriend/sugar daddy, you name all!! Zamani tujisikia kwa makabila machache kama yale ya Unyamwezi na usukumani lakini sasa ni kwa almost Tz nzima, yaani hata wachaga ambao walitegemewa kutojishughulisha na mambo haya, wamo siku hizi.

  Ninachotaka kusema ni kuwa kwa nini upeleke pesa yako kwa maganga ili kutafuta kupendwa au kutumbua hela za mwanaume!!! Tafuta za kwako, kula jasho lako. Ukienda uswahilini ndiyo utajua mambo mengo ya haya nisemayo. Yaani hizi ni hadithi za wamama wa nyumbani wengi, hata wa ofisi wamo, cha kushangaza hata wasomi, aibu.

  Limbwata unalo mwenyewe tu. Kama mume ni mkali sana, wewe uwe mpole na mnyenyekevu na mume huyo ni lazima atabadilika tu. Zidisha mapenzi kwa vitendo (maneno yako hasa), yale ya kule nani hii ni ya mwisho kabisa (hapa mnanipata???). Kwa akina mama hebu jaribu siku moja (kama hufanyi kwa sasa) upike chakula kizuri sana, mpokee mume wako kwa upendo na maneno ya kufariji, kaeni kidogo sitting room mpige story za utani, tena mkumbushe alivyokuwa anakulilia wakati wa uchumba, mkiondoka kulala mikono kiunoni hapo ndo koridoni mnaelekea chumbani. Mkifika hapo chumbani haki ya nani......Fanya hivyo kila wakati utaona mume wako atabadilika. Kama alikuwa anarudi saa za Chenge basi atakuwa anawahi Dinner, Kama alikuwa arudi anakaa sitting room anasoma gazeti na ku watch Tv, basi atakuwa anakuita darling maliza basi haraka huko jikoni uje upumzike hapa. Kama alikuwa ana......... yaani utabadilisha yote. Na wanaume tusichoke kuwabembeleza na kuwasifiwa wake zetu, hii ni fimbo kuu ya limbwata, kila huduma itakuwa exceled.!!!! Mwe msiinite baba/mama wa kitchen party!!!!
   
 11. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ngojeni niwaambie Libwata lipo,
  ni hivi mimi nimewahi kushuhudia haya mambo tena hata siku hizi wanaume wanawapa wanawake wao limbwata siyo wanawake tu wanawapa.
  1. Ni hivi kuna limbwata ( dawa za kienyeji) ambalo mwanaume anapewa ili awe mjinga kila analoaambiwa na mwanamke wake anakubalia yani anakuwa mjinga kabisa hiyo ni mbaya
  2. Kuna wanaume au wanawake ambao hawajatulia kwa hiyo wanawapa wapenzi wao ili watulie waachane na wanawake au wanaume wa nje. huyu hana nia mbaya hampelekeshi wala hamsumbui (huyu kinachomsumbua ni wivu uliopitiliza) na kwa upande mwingine anamsaidi mwenzake.
  TATIZO
  Tatizo ni kwamba haya mambo ni ya muda tu yanaisha na yakiisha hali inakuwa mbaya zaidi kuliko mwanzo.
  Na inakufanya uwe na wasiwasi muda wote maana mtu akija na mawazo yake sijui kakorofishwa kazini unaanza kuwaza sijui dawa imeishakwa hiyo hutakuwa na amani.
   
 12. kisale

  kisale Senior Member

  #12
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani niwaambie limbwata lipo, tena muwe makini kabisa na haya mambo!

  Kuna ishu moja ilitokea huko mkoani Iringa mama mmoja aliamua kumpa mume wake limbwata kwa vile alikuwa anapata hela nyingi ila hatulii nyumbani kabisa.

  baada ya kumuwekea hayo madawa aliyopewa kwa mganga mwanaume alitulia ndani kupitiliza,akawa haendi kufanya biashara zake,akawa hataki hata kutoka ndani ya nyumba,kunya humo humo,kukojoa humo humo,hata kuoga,baada ya miezi 3 kupita hela zikaisha mwanamke akaanza kuhangaika,alivyorudi kwa mganga ,mganga akamwambia yeye mwenyewe hawezi kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida kwa sababu alizidisha dawa tofauti na kipimo alichoambiwa na mganga.

  ilikuwa shughuli pevu ndugu wa mwanaume walivyokuja kugundua ndugu yao yupo ndani miezi 3, wao walifikiri kasafiri, walipoenda kumtembelea ilikuwa shughuli kumtoa ndani,alikuwa anaonekana ana akili timamu ila hataki kutoka nje ya nyumba, walisaidiana wanaume kama 10 hivi ndio wakafanikiwa kumtoa nje.

  yule mwanamke akachapwa viboko akamtaja mganga aliyempa dawa, nae akakamatwa na wanakijiji ila tatizo alikuwa hawezi kumrudisha kwenye hali ya kawaida. mpaka mzee mmoja alivyojitokeza akampa jamaa midawa ya miti shamba akawa kawaida kabisa.

  ilibidi amfukuze mke wake na mganga akalipa faini ofisi ya kijiji.

  Kwa hiyo wana jamii hii ishu acheni masihara ipo.Ni kuomba Mungu uliye nae asije kukuwekea hilo Limbwata la ukweli.Ila mimi mwenyewe naona hii kitu sio nzuri hata kidogo.
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Nadhani kuna watu wameingiwa na uzungu sana hata wanasahau mila za kwao, unadhani kwa nini ndoa za zamani zilikuwa zinadumu sana?mje mtutafute wataalam tuwafanyie limbwata. Kama kuna msichana narudia msichana haamini kama kuna limbwata ani PM anipe details zake halafu atakuja kuwahadithia wenzake wanao bisha.
   
 14. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wadau nataka kufahamu maana ya limbwata....
   
 15. GP

  GP JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mnh, swadaktaaaaaa
   
  Last edited: Aug 25, 2009
 16. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wadau nataka kufahamu maana ya limbwata....
   
 17. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Ujinga wa kumpenda mwanamke kupita kawaida!!!
   
 18. M

  Msindima JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Laligeni umenichekesha,je mwanamke nae akimpenda mwanaume kupita kiasi nayo inaitwaje?
   
 19. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2009
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kama hicho. Hadith tu
   
 20. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Msindima nao ni ujinga pia!!!
   
Loading...