Facts: Kwanini Rais Magufuli atashindwa vibaya

Facts: Kwanini Rais Magufuli atashindwa vibaya

Kwani katika scenario 2 zifuatazo ipi ni nafuu:-

1. Zinaingia meli 100 na 50 zinalipia ushuru na 50 nyingine zinakwepa kodi na hivyo serikali hukusanya kiasi cha shilingi 50; au
2. Zinaingia meli 5 na zote zinalipa ushuru na Serikali hukusanya kiasi cha shilingi 5.

Hesabu si uchumi lakini jua uchumi ni hesabu.
Hizo ni kiosk economics. Uchumi wa nchi huendeshwa kwa kufuata maadili.
 
Well said Mkuu.

Nafikiri kuna watu akili zao zimenasa wanahitaji electric shock ili wazinduke. Uchumi haukui kwa matamko, kupambana na ufisadi, wapinzani au watumishi hewa bali sera nzuri, mkakati, financial displine, siasa safi na diplomasia. Je tunavyo kwa sasa, tunatekeleza hayo


Tanzania nakupenda kwa moyo wote
 
SONGOKA:

1) Msomi hujenga hoja kwa takwimu wala siyo kwa dhana, nadharia zikisukumwa na hisia.

2) Nchi si ya Magufuli ni yako, yangu, yake na yetu sote.

3) Ungehitimisha kwa mapendekezo ya kuborosha pale unadhani Magufuli anafanya vizuri na ya kurekebisha mabaya.
 
Great thinkers nasubiri mwenye kuzipangua hoja alau kwa namba kama alivyopangilia mtoa hoja MM Mwanakijiji Okoa jahazi.
Hakuna hoja ya kumjibu huyo "msomi uchwara"kwa sababu badala ya kuchambua mwelekeo wa bajeti ya kwanza ya Serikali ya Magufuli (ndo kwanza inatekelezwa) anaishi kwenye ndoto (matukio yaliyopita)·

Angekuwa msomi kweli angechambua uhusiano (correlate) wa hatua anazochukua sasa hivi Rais Magufuli, km watumishi hewa, na kufanikiwa kwa bajeti yake.
 
Oyaa, nchi huwa zinaendeshwa kwa uchumi, uchumi unaosimamiwa kwa kutumia tried and tested principles.
Huwezi ku-substitute hizi principles na badala yake ukaendesha uchumi kwa kupambana na rushwa na utendaji mbovu. Tanzania katika awamu hii haina economic strategy elewa hilo, hizi imani za mitishamba mlizo nazo kwamba haya maigizo ya kutimua watu serikalini yatainua uchumi ni sawa na kujisugua na jiwe bafuni ukitarajia litatoa povu la sabuni.
"Can you please suggest any economic strategy, Mr Economist!" Au wewe ni 'mchumi uchwara' na bingwa wa kulaumu!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Jana nilikua nasikiliza J.Koinange live kwenye KTN alikua anazungumza na MD wa KPA..Kenya Port Authority...aliulizwa kama Dar es salaam ni tishio kwao kwenye biashara ya bandari. Yule mama MD kwa kujiamini kabisa akasema Dar kwa sasa sio tishio wala mshindani wao...wao misigo wanayo shusha ni mingi sana na haiyoweza Dar kuifikis in near futere. Na service zao zipo juu na wateja wanaridhika.
Kwa container moja la local ndani ya masaa 5 litakua nje limetoka . Mizigo ya transit wamejiwekea maximum siku 9 liwe limetoka.
Jamaa anasema wao kwa sasa wanaangalia vipi bandari yao itafikia kiwango cha Dubai, Singapore au Hongkong..na sio Dar..
Kipindiuoi cha nyuma wakati wa JK kulikua improvement bandarini mizigo ikaongezeka, na mradi wa Bagamoyo ulikua na nia ya kuongeza misigo na kuleta ushindani...lakini sijui kama utaendelea....kwa hali inavoelekea.
Kenya wako na nia ya dhati kuanza New Lamu port na katika mipango yao ya mbele wataunganisha central africa na Bandari zao, wana nia ya kufika chad , hadi cameroon. kwa njia ya reli.....
Tatizo letu Elimi na ujamaa jamaa..nafasi hizi za Bandari MD anatakiwa mtu alosomes mambo haya ya bandari na usafiri wa bahari...leo yunachaguana kwa u class mate...tuna safari ndefu sana
 
KUONGEA NA KUANDIKA VITU TOFAUTI,KUNA MTU ANAKUA ANAONGEA VIZURI SANA MPE MTIHANI ANAFELI,NA MWINGINE KUONGEA HAWEZI UKIMPA MTIHANI ANAFAULU.YAANI KINGEREZA CHA KUANDIKA NI MZURI CHAKUONGEA MBAMBAISHAJI
Jamani hebu tuondoeni mawazo mgando hayo tuwemahiri katika mambo yetu, watz tusione kawaida kwa msomi wetu ambaye amefundishwa kwa kiingereza tangu form 1 hadi versity akajua kuandika lkn hawezi kuongea mbona hao wengine waliopita shule km yeye wanajua kuongea. Hayo ni mapungufu ambayo inabidi tuyaondoe katika elimu yetu, tusione ni kitu cha kawaida.
 
Kukosorewa hataki maana ww mwenyewe unahitaji kukosolewa.
 
Back
Top Bottom