Facts: Kwanini Rais Magufuli atashindwa vibaya

Facts: Kwanini Rais Magufuli atashindwa vibaya

Wasomi wa bongo mna mambo sana. Eti wasomi!!!!! Hahahhhahhha. Wasomi wasiwasi umetujaa. Dah. Haya msomi fisi anayesubiri mkono wa binadamu udondoke apate kitoweo.
Wapo wasomi feki kama Prof Lipumba, huyo anaitwa msomi lakini matendo yake ni Aibu hata wa darasa la pili hawezi kuyafanya.
 
Atashinda kwa kishindo watanzania tuliomba kupata Rais kama huyu.
mkuu hajamaanisha kushinda uchaguzi labda kasome vzr amekuambia ndani ya miaka mitano maana yake hikibkipindi alichonacho atafail nyanja nyingi za kimaendeleo ,hv watz kuitwa vilaza mnaona sifa?bandiko liko straight forward kuanzia heading mpaka para zake na bado hukuambulia kitu?
maskini nchi yangu ,maskini watz wenzangu!
 
mmoja wapo akiwa Mwenye PHD pale magogoni"
Ben sanane alihoji hiyo PhD kwa undani mpaka Mtukufu akakereka na kumtuma Maliyamungu Bashite awaamuru kikundi chake cha wasiojulikana kimfiche sehemu akae mpaka azekee humo huku Heri Kisanduku akimchapa viboko kila asubuhi.
 
SONGOKA:

1) Msomi hujenga hoja kwa takwimu wala siyo kwa dhana, nadharia zikisukumwa na hisia.

2) Nchi si ya Magufuli ni yako, yangu, yake na yetu sote.

3) Ungehitimisha kwa mapendekezo ya kuborosha pale unadhani Magufuli anafanya vizuri na ya kurekebisha mabaya.
Mkuu kama umesoma kea makini mleta hoja ameonesha njia ,ni kwamba serikali ifanye knyume na shutuma zilizowasilishwa hapa!
 
Utasubiri sana. Utashindwa wewe na familia yako. Na iwe hivyo kama nilivyoandika. Nchi itasonga mbele. Amen
nchi Ina magurudumu"" mpka sasa imesonga nini ""? sasa??
 
"Can you please suggest any economic strategy, Mr Economist!" Au wewe ni 'mchumi uchwara' na bingwa wa kulaumu!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Mleta hoja hajabase kwenye uchumi tu bali nyanja tofauti ambazo ni vichocheo vya uchumi
 
wakati wananchi wakimshangilia Rais Magufuli kwa matamko yake yasiyoisha, wasomi wasiwasi umetujaa kwa sababu tunaona atafail vibaya ndani ya miaka mitano. Sababu ni zifuatazo
  1. Mapato ya nchi hayaongezeki kama alivyotegemea, ukizingatia kushuka kwa mapato ya bandari kwa hali ya juu kuwahi kutokea nchini, kupungua kwa mizigo, na kushuka kwa sekta ya Utalii ambayo ndo inaongoza kwa kuingiza fedha za kigeni (25%). Mpaka sasa sekta imeanguka kwa asilimia 5%
  2. Kuongezeka kwa matumizi yasiyokuwa ndani ya bajeti, (matumizi mkurupuko) kwa mfano kulazimisha serikali kuhamia Dodoma huku kukiwa hakuna hiyo bajeti. Rais kugawa fedha bila mpangilio wowote wala idhini ya bunge.
  3. Rais kutofuata mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa na serikali yake bungeni. Wakati kilimo ikiwa bado ni sekta ya kipaumbele katika mpango huo, mpaka sasa hatujaona msisitizo wowote katika sekta husika ambayo ndo inaongoza kwa kuajiri nguvu kazi ya taifa , zaidi ya rais kusema wilaya itakayopatwa na njaa atamfukuza mkuu wa wilaya na mkurugenzi (hii inaongezaje tija ya kilimo kwa mkulima??)
  4. Rais kuingiza siasa katika shughuli muhimu za kitendaji, kwa mfano kuteua wakurugenzi wa wilaya na mikoa wasio weledi na makada wa ccm, wakati akitambua hawa ndo msingi wa usimamizi wa maendeleo na utaalamu katika maeneo yao, kwa
  5. Wahisani kujitoa katika mipango ya maendeleo, MCC ni mfano mzuri
  6. kufifia kwa demokrasia kwa wapinzani kuzuiliwa kufanya mikutano na shughuli za kisiasa. Ikumbukwe wapinzani wamekuwa whistle blower wazuri katika ufisadi na ubadhilifu huku skendo zote kubwa katika nchi hii kuwa ziliibuliwa na wapinzani. Kuwafunga midomo ni kuwapa mianya mafisadi kujenga syndicate mpya za kupiga pesa, lakini pia rais anayefanya kazi bila challenge huishia kujisahau na kuharibu
  7. Rais kuchukiwa na watumishi wa umma, ikumbukwe rais tangu aingie madarakani amekuwa akiwasema vibaya watumishi wa umma huku akiwashushia tuhuma collectively utafikiri wote ni mafisadi. Mpaka sasa preliminary observation inaonyesha rais magufuri ndo rais unpopular among public servants kuliko rais yoyote Tanzania
  8. Rais kukiri mbele ya wananchi kuwa angejua ugumu wa kazi hiyo asingegombea, hii inaonyesha hakujiandaa au ali underrate kiti hicho, hivyo mpaka sasa hajui namna ya kuji adjust
  9. washauli wa rais kugeuka washauliwa, hii utachanganua mwenyewe
  10. Mawaziri kuwa waoga kiasi cha kukurupuka katika kusapoti maamuzi na statement yoyote atakayosema bosi wao hata kama wanajua haifai kwa wakati husika
  11. Mwisho, Kutokuwa na sera ya kimataifa kama nchi,huku uhusiano wetu na nchi kubwa kiuchumi duniani ukianguka vibaya sana. hatujui mpaka sasa mlengo wetu kidiplomasia ni upi
Hayo yoote ukiyajumlisha na kuangalia multiplier effect katika taifa hili na mwenendo wake ndani ya Miaka mitano, utakubaliana na mimi we are going to a hell of economic roller-coaster haijawahi tokea.
Can be a fact but not truth
 
Wewe na familia yako nyie ndiyo mtashindwa vibaya sana. Magufuli alishashinda, atatunzwa na kodi zako yeye na familia yake maisha yake yote hadi kifo kitapomchukua. Kama ni issue ya kisiasa, ategemei tena kura yako ili aingie madarakani. CHAPA KAZI KWA BIDII ILI NA WEWE USHINDE KWA KIWANGO CHAKO.
Wewe utakuwa umepata mgao wa Trillion 1.5 kama si 10% ununuzi wa ndege na 10% kuikomboa ndege pamoja na tenda za kujenga uwanja wa ndege chato.
 
Hakuna hoja ya kumjibu huyo "msomi uchwara"kwa sababu badala ya kuchambua mwelekeo wa bajeti ya kwanza ya Serikali ya Magufuli (ndo kwanza inatekelezwa) anaishi kwenye ndoto (matukio yaliyopita)·

Angekuwa msomi kweli angechambua uhusiano (correlate) wa hatua anazochukua sasa hivi Rais Magufuli, km watumishi hewa, na kufanikiwa kwa bajeti yake.

Leo unasemaje mkuu, muda kidogo umeshapita
 
K
Hapo hakuna hoja ni mawazo mfilisi. Hii nchi ni yetu siyo ya Magufuli. Kwanza umekosea kuanzia kwenye kichwa cha habari. Ukisema atashindwa, maana yake ni Tanzania itashindwa je, atashindwa kwa lipi wakati yeye anafanya kwa sehemu yake nasi tunafanya sehemu yetu. Hakuna raisi hatayetokea ili ashinde, tukifanyakazi kwa bidii tutaifanya nchi ishinde. Tutalipa kodi ya kutosha si kama sahivi, tunapolipa kodi vijisenti coz tunazalisha kidogo na wachache ndiyo tunachangie uchumi wa nchi. Wengine mnashindwa kwenye keyboard kutwa.

Kodi ikilipwa haijulikani inakoenda, CAG ameonyesha matumizi ya trilion 1.5 ambazo hazina maelezo.
 
Uzi una miezi 21 na kilichotabiriwa kuhusu huyu dhalimu ni ukweli mtupu nchi imemshinda vibaya sana kabaki kufoka foka na kusema uongo kila kukicha na story zake za uongo kuhusu Scandinavian Countries na China. Kajisemea Mzee RUKHSA nchi inaendeshwa kama gari bovu haina sukani. Bado kuna miaka miwili na nusu hadi 2020 I hope wataona hili balaa kubwa la huyu mtu hivyo 2020 wamswage arudi Chato akafuge punda.
Yaani nimeamini jiwe hazimtoshi kichwani.
 
K


Kodi ikilipwa haijulikani inakoenda, CAG ameonyesha matumizi ya trilion 1.5 ambazo hazina maelezo.
Pato la Taifa baada ya kulipa mishahara ya watumishi wa Umma huzichukua pesa zinazosalia na kuzitumia kwa mambo ya hovyo hovyo yasiyo na tija kwa Taifa ikiwemo kuwabambikia kesi Wapinzani kuwakomoa kukandamiza Demokrasia
 
Uchambuzi mzuri sana, japo "Boot Lickers" wanaubeza lkn una-reflect ukweli kabisa ya yanayojiri nchini.
 
mkuu hajamaanisha kushinda uchaguzi labda kasome vzr amekuambia ndani ya miaka mitano maana yake hikibkipindi alichonacho atafail nyanja nyingi za kimaendeleo ,hv watz kuitwa vilaza mnaona sifa?bandiko liko straight forward kuanzia heading mpaka para zake na bado hukuambulia kitu?
maskini nchi yangu ,maskini watz wenzangu!
Tuna hali mbaya ndg,jamaa uliemquote hapo ndio wasomi wa nchi hii kwa kweli bado tuna safari ndefu
 
Back
Top Bottom