Facts: Kwanini Rais Magufuli atashindwa vibaya

Facts: Kwanini Rais Magufuli atashindwa vibaya

Huyu bwana kwa sasa anatumia madaraka yake kudhibiti kila aina ya taarifa inayotoka kwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari,Bunge,wapinzani na whistleblowers kwa ujumla.

Matokeo ya hali hii ni yeye sasa ndio anaibua kashifa tofauti na huko nyuma ambapo kazi hiyo ilifanywa na Bunge,media,wapinzani na wadau wengine, hali ambayo sasa haipo ingawa mambo haya yanaendelea kama alivyotuthibitishia siku chache zilizopita pale alipoibua kashfa fulani.

Swali la kijuiliza ni hakuna mengine anayoyajua na ambayo kaamua kuyakali kimya?

Binafsi sitaki kuamini kuwa wanahabari za uchunguzi na whistleblowers wengine kwa ujumla wakiwemo wanasiasa walikuwa hawajui kuhusu hili, ila naamini wako baadhi walikuwa wanajua ila wakachagua kukaa kimya kwa usalama wao(kumbukeni ya ndege kudakwa huko majuu na kamanda wetu alietuhabaraisha kuhusu hilo).

Kutokaa na hali hii,hivi sasa Bwana huyu na wasaidizi wake wana-enjoy hali hii kwa wao kuamua nini kiende kwa umma na nini kisiende lakini wanasahau kuna siku watatoka hapo walipo na wakati huo ukifika,kila kitu kinachowahusu kitawekwa wazi maana kila mwanasiasa siku zote hutaka kupata credit kwa mambo ya aina hii(kuanika uozo wa wenzake hata kama yeye anafanya yale yale).

Hata hii habari ya madini wanayotutangazaia ukweli wake utakuja kujulikana siku wakitoka pale mikataba husika itakapowekwa wazi au kuvujihwa ili tu umma ujue ukweli kwani wanajikweza mno huku kila kitu ni siri yao.

Hivyo,tuwaombee maisha marefu,siokwasababu tunawapenda,ili waje washuhudie ukweli ukiwekwa wazi na waweze kuhukumiwa pale walipodanganya.

Uzuri siku hazigandi na muda wao wa kukaa ofisini unazidi kupungua hata ikitokea wanarudi tena ofisini kwani ndio itakuwa kipindi chao cha mwisho kwa maana ya wao kujiandaa kukabidhi ofisi kwa wengine.
 
Hakuna aibu atakayo ipata kwasababu katiba inamlinda na kwakuwa siai tupo wasahaulifu sana, basi tarajia kwamba wapo watasikika na wakioaza sauti kwamba "waacheni wastaafu wapumzike" kwamba walifanya mengi mazuri katika kipindi chao.

Minadhani hapa kikwazo kikubwa ni katiba
 
Nikwambie tu huyu anaweza kuja kuumbuliwa hata na wanalumumba wenzake mbali na wapinzani.
 
Hahaha mnaendelea kupiga ramli, kumbe ndo maana Dikteta Mbowe hataki kuachia Madaraka chadema? Kwa kuwa Mbowe anaiba Hela za Chama mnafikiri kila mtu ni mwizi?
 
Kila zama na kitabu chake. Piga kazi JPM.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Afrika.
Asanteni kwa kunisikiliza.

macson
 
Hahaha mnaendelea kupiga ramli, kumbe ndo maana Dikteta Mbowe hataki kuachia Madaraka chadema? Kwa kuwa Mbowe anaiba Hela za Chama mnafikiri kila mtu ni mwizi?
Anahofia ile mikopo hewa kwa chama na fedha za wafadhili alizoanzishia miradi binafsi kuwekwa hadharani.
 
Salary Slip usikonde wala kuhangaisha sana mawazo yako. Unadhani kuwaita viongozi wote wa ccm Dar Jana kama alivyo waita watendaji ni bure? Hapana, ukisikia kauli zake ni kuwa keshaona maji shingoni.

Muhimu hawa viongozi wa upinzani waache blabla sasa ni kukomalia Tume huru ya uchaguzi hata ikibidi uchaguzi ucheleweshwe hadi mwakani ni sawa tu
.
Baada ya hapo, lazima ccm itabwagwa au itakosa 2/3 ya bunge na nchi itakwenda bila kuburuzana wala udikteta na maovu yote ya 2015-20 yayawekwa hadharani kabisa.

Akiondolewa hiyo ndio itakuwa safi zaidi maana yale ya Chiluba yaweza kufanyika hapa, unaondoa kinga kwa muda then kama kuna la mahakamani unampeleka hata kama ndani ya cage kama Mubarak

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akitoka utasikia serikali itakayoingia itakavyomponda, utasikia serikali iliyopita ilikuwa ya kibabe sana...
 
Chakaza,
Mkuu,huyu bwana mimi haniumizi kichwa kwani naamini kwa sasa anakimbia tu akiwa ndani ya chumba mbio ambazo mwisho wake huwani ukingoni.
 
Toa rubbish zako hapa. Mambo mangapi Rais kama taasisi anaweza kutoa baraka siyo lazima bunge? Je wkt udom na shule a kata na JKCI na mlonganzila zinajengea..upupu wako huu mbona mbona hatukuona..haya yalipit bungenj kwa baba yako Zitto? Wivu utakumaliza wewe na kwa sbb ndugu zako wametumbuliwa Ndiyo maana unatuletea ushuzi hapa kila siku. Hivi baba yako mbowe hizo hela za ruzuku na wafadhili huwa humuulizi? Tana mlisitahili kufungwa kabisa. hata aibu unakuja hapa kuleta porojo huku
 
Hili povu linathbitisha ukweli umekuchoma!!
 
Back
Top Bottom