Mie sina Cha maswali wala Cha majibu.. Niongee direct Na Zuberi my young brother and I know unaufiatilia Uzi huu Na unajiandaa kujibu maswali ya wananchi Kwa mlengo unaoujua.. AMA kweli au uongo potelea mbali mradi wadanganyika waridhike..
, kumbuka ulipoutwaa Ubunge the first time uliniambia ni fedha Za wauza karanga, mihogo, Dagaa Ndizo Zilizokupa power ya kupiga kampeni hadi Ushindi. Na Kwa maana hiyo ulipoingia bungeni kuna Jamii ambayo si ndogo mpaka Sasa inathanini Na kujua ukifanyacho mjengoji.. Bidii hizi si Za kubeza hata kidogo, matamshi yako ya Juzi si ya kizalendo hata kidogo, Kusema huna mpango Wa kugombea Ubunge Tena 2015 utagombea kuteuliwa kinyanganyiro Cha Urais Na ukaweka wazi kupitia CDM, ingawa umekwenda nje ya utaratibu lakini bado hujavunja sheria yoyote ndani ya KATIBA ya CDM, Na Mtu yeyote asiyejali anaweza Kufanya Kama ulivyofanya lakini mimi sikulaumu Kwa kuropoka hivyo lakini naumia Kwa wewe kwenda mbali zaidi Na Kusema kama CDM haitakuteua Basi utaunga Mkono Mwingine atayechagulia Na kukaa benchi lakini Ubunge No tena, ulichokifanya huwezi Kufanya zaidi ya Hapo.. Which means uwezo wako Wa kiuongozi umeishia hapo, ni sentensi Za Mtu aliye kata tamaa..
Ni kweli Hutaki kuwa Mbunge tena wala Kiongozi tena, Na Inshu kubwa ni Maradhi.. BWANA Mdogo maradhi tumeumbiwa binaadam, usikate tamaa mapema.. Mbona wagonjwa wengi tu lakini wanapeta wanasonga mbele maisha yanaendelea.. Unamuona Leigwanan, Mtu yuko hoi, hata kutembea anavibrate Mwanzo mwisho, bado haitoshi viharusi vinambamiza kila kukicha lakini mzee yupo tu, bado anapiga kelele ntagombea Urais kupitia magambazz, Na masauti yake of which najua hata akipewa hawezi kuzungukia mkoa hata mmoja lakini makelele yake magamba hawalali.. Kidume husifiwa Kazi Na bora yakukute huko mbele Kwa mbele kuliko kukaa bench.. Ukikaa benchi Kwa siasa zetu utasahaulika haraka Kama Moto wa makaratasi..
Wewe mwenyewe unajua 100% CDM hawawezi kukupitisha ugombee Urais, Unafanya fujo tu ili ustaafu uongozi Kama Mtu aliyediriki kufanya Jambo.. Hata Kama CDM wakipuliziwa sana Na ukapita sidhani kama watanzania watampatia uongozi Mtu bachelor asiyejua uongozi hata wa familia ukoje.. Uongozi siku zote huanzia nyumbani babaa.. Sikulaumu kwamba huwezi oa lakini Unafanya viroja sana brother..
Acha makelele, chapa Kazi, ukifika Muda wa kugombea huo URAIS Basi gombea ukishindwa Basi gombea Ubunge tuendelee kupiga Kazi.. Sio kwamba unayo mabaya tu, unayo mazuri mengi pia.. Bado Kigoma Ina mengi ya kufanyiwa.. Serukamba ni mpinzani si Adui, still meza moja mwaweza kaa Kwa maendeleo ya KGM..