EXCLUSIVE Interview with Zitto Zuberi Kabwe at Jamii Forums [Coming Soon]

EXCLUSIVE Interview with Zitto Zuberi Kabwe at Jamii Forums [Coming Soon]

Status
Not open for further replies.
Naomba kukuuliza maswali mawili.
1. Kama tayari una msingi wa mahojiano hayo (kwenye nyekundu), je unaonaje ukaorodhesha baadhi ya controversial statements ambazo labda ZIMEKUFANYA UWE NA NIA YA KUMHOJI ONE ON ONE? ili watu waweze kuchangia controversies zaidi wanazoziona?

2. Muda?? Ana muda gani? Ili tuweze kujua maswali mangapi na majibu ya kina kipi yanategemewa?

Mwisho naomba nikuulize hiyo interview itakuwa kama town hall meeting with you as a moderator? au kama interview ya TV/Radio? Gazeti?
Kwa sababu mimi binafsi nina maswali mengi na nataka nijue lipi au yapi yatafaa.

Swali lako la kwanza ni la msingi ila kwa upande wangu sioni kuwa kuna haja ya mimi kuweka hizo controversies kwa kigezo kuwa inaweza control the nature ya maswali ambayo yanaweza ulizwa na members. Good enough kumekuwa na an exemplar ya hilo kwa kupitia kipengele ambacho kilizungumzia kuto entertain maswali binafsi juu ya Zitto ambacho nilikuwa nimeweka na sasa kimetolewa. How ever nikadadafua kwa kina kwa kupitia post # 20 ya hii thread - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...t-jamii-forums-[coming-soon].html#post5054464.

Swali lako la pili:-
Nimemuomba kuwa kutakuwa na mlolongo wa maswali tosha… Nikamuomba pia kuwa uwepo wake utahitajika na a lot of his time taken huku nikimsisitiza kuwa ni too early kujua time frame ya kuweza kutosha kujibu hayo maswali (baada ya yeye kujoji time). Kwa kifupi Zitto kaahidi kujitahidi kadri ya uwezo wake kujibu maswali yote kama nilivyo muomba. That is to say swala la time naomba likae pending kwanza.

Kawa muktadha huo mkuu Kobello, wasilisha maswali yako uliyonayo usiwe na shaka; ANGALIZO ambalo naweza toa ni kuwa ni wazi Zitto is a busy bee... Tokana na kwamba kakubali kwa moyo mmoja - Naamini he will give his Best na ataweza jibu maswali. Sijui una maswali mangapi... Genuinely I hope not a hundred.

Namna itakavyo endeshwa itakuwa kwa mtindo huu... Tafadhali pitia hii Link ni mfano halisi. https://www.jamiiforums.com/great-t...ew-with-jamiiforums-founder-maxence-melo.html
 
I am glad this is cleared…

I am curious… Unaposema kuwa hatasema ukweli una maana umesha ji' tune kuwa lolote atakalo ongea likiwa nje ya lile unalo AMINI tayari juu ya hilo itakuwa sio sawa? Hilo la Uswiz nashauri panga maswali yakiwa directed to him then uone kama hatajibu…

I believe I am prepared. Inawezekana sio kwa ubora kama mtu ambaye tayari mzuri katika anga ya Siasa BUT prepared enough. Hayo mahojiano hayatakuwa maswali na majibu baasi! Kama swali lina utata, ataulizwa swali juu ya hilo swali ili atoe utata huo. Hii ni moja ya sababu kubwa ambayo mimi nilitaka ushirikiano wa members… Kama kawaida kutakuwa na side thread ya members kutoa comments kuhusiana na interview itakayo kuwa inaendelea.

Jmushi1 umezugumza kwa kirefu aina ya maswali… Hivi sijaelewa maybe; ina maana bado kuna maswali unayo na unaona hayataulizwa sababu hayapo valid or hayajibiki? So far naona kuwa that is clear.



In Blue; Jibu ni ndiyo. Ila take note kuwa atanipa time frame yake ya mda gani anaweza kuwepo, maswali mfuatilio ni muhimu ila yataangaliwa kama ni ya msingi na siyo yote hasa penye hoja ambayo atakuwa amejibu na imepwaya.

In Green; labda kama sijaelewa... So far hakuna limitation ya maswali, unaposema dondoo una maana ipi? Kuhusu maswali personal kama mwenyewe ulivyo kiri kuwa nimetolea ufafanuzi. Hajanipa limitation ya the kind of questions za kumuuliza.



The above para naona sasa kuna maswali ya kuwasilisha hapo... Will do so mkuu.
Ninaposema dondoo,nikwasababu unasema maswali yatakayojibiwa ni yale ya msingi.Sasa kila anayeuliza swali huwa anaona kwamba achouliza ni cha msingi(unless stated otherwise by the moderator).

Na ili kuondoa huo utata,ndiyo maana nikasema kuwepo na dondoo,ama kwa maana nyingine,u clarify kwamba atajibu maswali ya aina gani,ili kama yakijibiwa tofauti na vigezo vilivyowekwa,then tunaweza ku conclude kwamba maswali hayo si ya msingi.

Mfano labda mseme ahojiwe kuhusiana na issue za ufisadi,katiba mpya,misimamo ya chama chake,issue za kiuchumi,na pengine pia social issues(just mifano).Kwasababu utapima vipi kwamba swali siyo la kimsingi bila kuiweka hiyo misingi?

Kwa mfano swali kama anaamini chama chake ni cha kidini,linaweza lisionekane kama swali la msingi,lakini kwa wengi ni la msingi kabisa kwasababu alishasema nia yake ya kugombea urais ni ili aondoe hiyo migawanyiko na kwamba yeye ndiye mgombea pekee mwenye kuweza kufanya hivyo,and so therefore ndiyo maana nikauliza uwezekano wa follow up questions kwasababu sasa nitamwuliza atafanyaje kuuondoa huo udini?Je anadhani kama chama chake kimepewa sura ya kidini(kama haamini kuwa ni cha kidini),je nini kifanyike ili kuondokana na hilo?Maana kiukweli hata ccm hutumia hilo popote pale anapopingwa na wanachadema wenzake.Pia hata kushauriwa kwake asigombee uenyekiti last time.

Kama ulivyouliza kwamba nimesema maswali mengine yatakwepwa ama kutojibika,ni mfano wa swali la ni kwanini hakuwataja majina wenye akaunti za uswisi.Hilo nitasubiri jibu kwa hamu kubwa...

Na pia swali kama lile ambalo tumeshauliza mara nyingi,kwamba ni kwanini alimuunga mkono JK kwenye ugombea urais badala ya mgombea wa chadema given that vyama hivyo vinatofautiana sana na pia imani kwamba ccm ni mafisadi na ufisadi ndiyo umetufikisha hapa tulipo?Je alitofautiana kiasi kikubwa hivyo na mgombea wa chama chake hadi kuhamishia sapoti kwa ccm?Sanasana nisikufiche,atakachojibu ni kwamba "Siasa si uadui",sasa hapo kwangu hilo si jibu.Hilo tayari ni sawa na kutosema ukweli.

Wengine wameuliza kuhusiana na kutokuwepo kwake kwenye hizo movement za chadema,kiukweli,kuna watu wameshamjibia,especially wanaomunga mkono ndani na nje ya chama ikiwemo waandishi wa habari.Wao wamekuja na tahmini zao,na watu wanaamini hivyo ndivyo anavyofikiri yeye kwasababu hajawahi kuzungumzia wala kukubali kujibu maswali ya aina hiyo.Na ndiyo maana unakuta waandishi wamebakia kujibizana,wengine wa upande wake na wengine wenye kuona tofauti.

Kiukweli sina mashaka na uwezo wako wa kupick up maswali ama hata uwezo wako wa kujitayarisha.Nina imani kwamba mjadala utakuwa vyema kama ni kweli atajibu maswali yote.Kwasababu uliposema kuhusu maswali ya msingi,nimejiuliza kama unawasiliana naye kumwonyesha maswali uliyoya pick na kuona kama atakubaliana nayo,ama ni kwamba hajui maswali utakayoyachaguwa?Maana hapo kuna utofauti.Siyo kila mwasiasa ni mvumilivu wa kuulizwa maswali asiyoyataka,maana swali lisilo la msingi kwake anayeulizwa linaweza kuwa la msingi kabisa kwa mwulizaji na hata msomaji.
 
Na swali moja tu kwa Zitto Kabwe.

1. Swali langu kuna uwezekano mkubwa Watanzania tukaingia kwenye uchaguzi mkuu na katiba hii iliyopo kabla ya katiba mpya kuwa tayari. Je utafanyaje kuhusu nia yako ya kugombea urais umri utakuwa umekubana kutoka na katiba iliyopo sasa. Wakati umeishawambia jimboni kwako Kigoma Kaskazini kuwa mwaka 2015 hautogombea tena ubunge utagombea urais.
 
Last edited by a moderator:
Ametangaza nia ya kugombea urais, je atakua vipi rais bila ya kua na mke au katiba haimbani?
 
Mkuu naomba uwakilishe maswali yangu kwa Mh Zito kama ifuatavyo;

-Mh. Zito anajua kwamba katiba ya sasa ya Tanzania haitamruhusu kugombae nafasi ya urais 2015 kwa sababu atakuwa na umri wa miaka 39, umri ambao katiba haimruhusu, lakini yeye yuko radhi kupambana kufa na kupona kubadili kipengele hiki cha katiba ili kupunguza umri na kumruhusu agombee;

je haoni kwamba huu ni ubinafsi mkubwa kubadili kipengele cha katiba kwa manufaa yake binafsi?


-Mh. Zito, je asipoteuliwa nafasi ya kuwania urais CHADEMA atahamia chama gani?

Je atahamia chama chake alichokiasisi cha CHAUMA,
Atajiunga na ADC ambako mazingira yake ya kuhamia yanaandaliwa, au
Atakwenda CCM kwa wanaomtumia kusambaratisha CHADEMA?
 
Mh Zito,

CCM ina reform kwa kasi, inaonekana ikawa kwenye nuru mpya kabisa hadi kufikia 2015.

1. Unaona tofauti ya msingi kati ya CCM na CHADEMA ni IPI?

2. Nini kinakuvutia ndani ya CCM amabcho hakipo CHADEMA?

3. Bado unafikiri wewe kuwa CHADEMA ni tija kwa jamii kuliko kuwa Chame kingine say CCM?
 
Zipo tetesi kuwa hoja aliyoiwasilisha bungeni hivi juzi kuhusu fedha za watanzania wachache kwenye acc huko Uswisi ni hoja ya Membe ila yeye alitumiwa .Pia inasemekana kuwa ushaidi wote alipewa na Membe hivyo akaogopa kuwataja wahusika coz ushahidi ulikuwa na mashaka na chanzo chake.

NAOMBA KUTHIBITISHIWA/KUKANUSHIWA HILI JAMBO..
 
Asante Dada AshaDii kwa mada hii!

Naomba nianze kwa maelezo kabla ya maswali,

Kwanza nianze kwa kukupongeza kwa kazi nzuri uliyoifanya ya uchunguzi na upelekaji wa hoja binafsi Bungeni!

Hivi juzi tu kikao cha bunge kilichopita, Bwana Zitto alitoa hoja murua ya kulitaka bunge letu tukufu liunde tume kuchunguza tuhuma zinazowahusisha watanzania kuficha MABILIONI nchi za nje kinyume na utaratibu wa sheria za nchi yetu,

Kufumba na kufumbua kunataarifa iliyotufikia hapa jf kutoka serikali ya USWISI ikitoa masharti kwa serikali ya Tanzania ili iweze kupatiwa orodha ya Watanzania wenye MABILIONI katika nchi hiyo,

Kwa mtazamo wa haraka na aina ya serikali tuliyona masharti yale ni magumu kutekelezwa,

SWALI

(1) Kunaukweli wowote kuwa taarifa ile ya USWISI kuiwekea masharti Tanzania, ilitoka ndani ya serikali ya USWISI au ni mkakati wa mafisadi hawa kuzima jaribio la kurejesha pesa hizo?

(2) Kama taarifa ni yakweli, Je kuna nafasi ya nchi yetu kufanikiwa kuyarejesha mabilioni hayo ambayo ni kodi ya wanachi?

(3) Kwanini umependekeza kuundwa kwa tume, nakuendelea kumaliza pesa za watz wakati kimantiki ripoti yako ilikuwa ni yakuiwasilisha TAKUKURU tu, na ikiwa hawajaridhika, nao TAKUKURU kwa utaratibu wao wa ndani waendeshe uchunguzi na kuchukua hatu?

(4) Ikumbukwe kuwa, tangu nchi hii itumbukie ktk ufisadi mkubwa, chombo chetu TISS kipo kama hakipo, na kama kipo basi ni kwa msaada wa mafisadi tu, Katika mtazamoo na tafsiri ya ripoti yako, taasisi ya Usalama wa Taifa (TISS) Unaiweka katika mizani ipi?

Ni hayo tu mheshimiwa naomba majibu!
 
Ni haki ya rai yeyote kuaomba kuchaguliwa au kuchagua ili mradi ana vigezo vyote. Lakini kwa kupitia vyama, kila anayeomba achaguliwe lazima afuate taratibu za chama husika, ikiwa na maana wapi aeleze nia yake hiyo, lini aleze nia yake hiyo ndani ya chama chake.

Pia, kwa kuzingatia taarifa zilizozagaa kuwa Zitto anatumiwa na intelijensia via ccm ili kukigawa chama chake ili hali hata ccm wenyewe hakuna aliyetamka hadharani nia yake ya kugombea urais 2015 hadharani, hadi kwenye vikao halali vya chama.

1. Kutangaza nia yake hadharani tena kwa kurudia rudia (nadhani, ili viongozi wakuu wa chama chake watolee tamko hoja yake ili mgawanyiko uanze rasmi), ni kwa faida yake (Zitto) binafsi au Chama chake?

2. Chama chake CDM kina taratibu zipi kwa yeyote anayetaka kugombea urais na utaratibu alioutumia?

3. Kuishi au kuwa na mke siyo jambo jepesi, linahitaji uvumilivu na busara nyingi sana, kama vile ilivyo kuishi na mume. Kama hili limekushinda, vipi utaweza kuwaongoza watanzania wote wake kwa waume?

4. Huku ukijua serikali haina nia ya kuwataja walioficha fedha mabenki ya nje huku wewe ukiwa na majina; unayashikilia hadi sasa ili nini na kwa faida ya nani?

Kibanga Msese
 
AshaDii,

..kwa sasa sijaandaa maswali ambayo ningependa umuulize.

..lakini naomba usiimuulize swali lolote lile linalohusiana na nia yake ya kugombea Uraisi.
 
Last edited by a moderator:
SWALI
[1].Mkakati gani wa anaouona kuwa unaweza kutambua vipaumbele vya kuondokana na umasikini wa Tanzania.?
[2].kwa nini Tume ya Bomani,ambayo yeye alikuwa mjumbe,Taarifa yake haijawekwa wazi kwa Umma?au kuna haja ya kuunda Tume nyingine,ili iwe huru zaidi katika kufanya kazi na kutoa Taarifa kwa umma?
[3].Kama kijana,ametembea nchi kadhaa duniani,je?ni nini tunakosea kama Taifa,na nini?viongozi,wanasiasa,vijana na wananchi wanakosea?
 
1. Kwanini anatoa hoja nzito bungeni hazisimamii au zinapewa majibu rahiisi kwenye maswali mazito halafu anakaa kimya mf.EPA,HELA ZA USWISS,BOT,FEDHA ZA RADA zimerudishwa nchini je zimefanya nini cha maana eti zimenunua vitabu ktk shule ngapi kama sio wizi tu hadi inakera.

2.Haoni kugombea urais sasa hivi ni mapema sana ukilinganisha na age aliyonayo namaanisha baada ya kumaliza awamu yake ya utawala atarudi kuwa katibu mwenezi au amejiandaa vya kutosha kuikabili fainali uzeeni.

3.Analizungumziaje suala la kuwa na utitiri wa vyama vingi vya siasa vinavyokula pesa za walipa kodi halafu havina tija wala mchango wowote kijamii zaidi ya kutufilisi,je kuna umuhimu wa kuifanyia sheria mabadiliko ili kuwe na limitation mf,vyama vitatu tu.

4.hizo kashfa zinazokuandama kuwa unatumiwa na chichiem zina ukweli wowote na mbona sijaona unazitolea ufafanuzi mbele ya hadhara kuna nini nyuma ya pazia?

5.unatarajia kugombea urais mission na vission yako ni ipi kuikomboa TZ kwa sababu tuko chini ya wakoloni wa kiafrika tunahitaji revolution ya kweli una chochote cha kusema.

Ngoja ninywe kwanza maji ntarudi baadae ila tu haya maswali ya utangulizi yamfikie bila editing coz hakuna typing error hapa.
 
AshaDii,sitaki niifanye kazi yako kuwa ngumu.Nitaridhika tu na maswali utakayoyachaguwa bila kinyongo.Mimi siyo anti Zitto,ila ningependa tu ajibu maswali kama akitaka,na asipotaka,kusema ukweli sina nia ya kupinga ama kuonyesha kutokuridhika,maana hata nikifanya hivyo haitabadilisha chochote.

Madhali kuna member wengine wenye maswali,basi sitaki kuwa mbinafsi.Nitajifunza pia kwa kuyasoma maswali na majibu yatakayopatikana,and so eventually we will move forward.

Sitaki kuwa negative wala kuwa kikwazo,kwasababu umejitolea kufanya shghuli hii na pia Zitto amekubali kushiriki,basi kuna wengi watanufaika.Na kutokuridhika kutatokea,lakini sidhani kama ni sahihi hilo kuwa ni kikwazo kwa juhudi zenu.

Kwasababu mimi si mwanachama wa chadema,lakini Zitto ni mmojawapo wa viongozi waliopelekea mimi kuwa mshabiki wa chama hicho,na ni matumaini yangu kuwa nitakuwa mwanachama wa chama hicho siku za mbeleni.

Kama vile ambavyo wewe husema...Pamoja saana!
 
1. Kwa nini Tanzania haina uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme?

2. Tanzania ifanye nini ili iwe na uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme?

3. Itaichukua Tanzania miaka mingapi kuwa na uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme?
 
Swali langu umetangaza kwamba hutogombea ubunge hutagombea urais 2015, ana una utakuwa na umri wa miaka 39 2015,je katiba yetu ya sasa ina ruhusu hilo? Na je kama haitabadilishwa utafanyaje?
 
Kwanini Zitto anaongozwa na falsafa ya KUJIJENGA YEYE BINAFSI kisiasa? Anaugonjwa mkubwa wa kutofanya kazi kama TEAM WORK.
Kauli na matendo yake haweki link yeyote kwa kukuza Chama chake.
 
Kwa nini viongozi wengi wa Chadema hawajaoa.Au ni chama cha mabachela
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom