I would have believed that line if I did not know of your capability on this... I should say I would genuinely be SO dissapointed if you do not present any of your questions. Nadhani in this unakosea... Ilitakiwa utoe maswali; then uangalie if what you think is what will eventually happen hivo kukupa jibu kuwa your pessimism was valid.
Naomba ushirikiano wenu...
Ok mkuu,ushirikiano utaupata tu wala usijali.Ila kwasababu umeshakuja na disclaimer,wengi wana wasiwasi kuhusiana na hayo maswali ya binafsi.Kwakuwa umeshatoa ufafanuzi wa hayo maswali binafsi ambayo hayatakiwi,basi nimekuelewa.Nilidhani kwamba maswali binafsi ni kamavile kuhusu kutajwa kwake kwenye umiliki wa akaunti uswisi(alishapinga hilo na sitegemei jipya),pamoja na umiliki wa magari ya kifahari(nayo alishapinga licha ya wengi kudai kwamba ni kweli),however huko nyuma,alishakubaliana na hilo,na akasema kuwa aliamuwa kuyauza kwasababu ni ya kifahari na kwamba ni gharama sana kuyahudumia.
Kwanza kabla hatujaenda mbele,ebu tuanze na misingi ama nguzo za maswali tunayotakiwa kuyauliza,hapo chini umesema hivi...
Kwa mukatadha huu - hii inakuwa kama 'golden chanc'e kuweza kuitumia kwa wale wote wenye kiu ya kuuliza maswali kwa kutaka kujua juu ya yale ambayo Zitto anajua/fikiria/panga.
Niliposema sitegemei majibu kwenye maswali muhimu ama magumu,ni kwasababu ya msingi/nguzo ulizoziweka kuhusiana na uulizaji ama aina ya maswali hayo.Kwa mfano wengi wetu tunaamini kwamba hatasema ukweli(ndiyo maana ya kuwa pessimistc),kwasababu wengi tunajuwa(upon looking on what he says and believes) yale anayoyajuwa,kwa mfano tunajuwa kwamba anajuwa kuna watu wenye akaunti huko Uswisi,lakini tunajuwa kwamba hataki kuwataja(kama alivyoahidi)
Tunajuwa anayoyajuwa na ndiyo maana sasa ni kama tunafahamu anavyofikiri,pengine anafikiri kuisema hoja hiyo bila kuwataja hao wenye akaunti kutamsadia yeye?Maana sioni hilo lina msaada gani kwa mtanzania yeyote yule.Kwahiyo sijui kama ukimuuliza ni kwanini hawataji kama takuwa na jibu la uhakika.
Je kuhusu anayopanga?Again,wanasiasa ni watu ambao wanajuwa sana kukwepa,na ndiyo maana mambo yasiyo ya wazi ama ya kijanja janja yanahusishwa na siasa.Yani kwenye mawazo yetu,siasa ni jambo linalochukuliwa vyema.Hilo ni kutokana na tabia ya kukwepa kwepa ama hata kuficha ficha ya wanasiasa walio wengi.Ndiyo maana mara nyingi maswali yanakuwepo kwa wanasiasa,lakini wanapolizwa,wakiyajibu inakuwa kama vile majibu yao yameongeza utata zaidi na maswali zaidi.
Hilo linanifanya niamini kwamba maswali hata nikiuliza leo,siyo kwamba ndiyo ukweli wenyewe.Given that wanasiasa pia wana ukigeugeu mara nyingi tu.Kwa mfano Zitto mwenyewe keshazungumza mara nyingi sana kuhusiana na future politics.Lakini majibu yake yamekuwa yakibadilika mara kwa mara.Na hivyo utakuta kuna wananchi wanaodhani wanajuwa mipango yake,ama hata kuwepo na wananchi wenye kumfahamu kwa namna za tofauti kutegemeana na uelewa wa wananchi hao.
Naomba nitadhaharishe kuwa maswali yawe ya msingi, ya kujenga na vilevile kuweza kupata majibu ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.
Ni ukweli kuwa tunaweza kutegemea kwamba tutapata majibu ya kujenga,however hilo linategemeana sana na aina ya maswali.Kwasababu mara nyingi wanasiasa wako busy zaidi kujinjenga wao binafsi.Ni muhimu sana tukafahamu tofauti kati ya kujenga vs kujijenga.Yote siyo mbaya.Lakini nina amini kuwa maswali ya kujenga ndiyo yatamjenga mwanasiasa.Whereas majibu ya kujijenga mara nyingi yanaleta migawanyiko zaidi pamoja na ukweli kwamba yanafanya situation kuwa too polarising.
Kwa mfano watu wanaweza kuja na maswali kuhusiana na ugombeaji urais,halafu maybe akaulizwa swali kuwa ni kwanini hashgulikii issue ya kuhusiana na kipengele cha umri kwenye katiba.Sijawahi kuona akijishughulisha kujibu hayo.Badala yake kumekuwa na washabiki wengi wakidai kuwa ni mkwaruzano wake na chama chake kwasababu chama chake ni cha kidini.(polarising).Kwahiyo tunapokuwa hatupati majibu kamili kuhusiana na msimamo wake kuhusu mtizamo wa mashabiki wake kuwa chama chake ni cha kidini,utakuja kuona kwamba uanasiasa ni kitu kibaya na ndiyo maana wengine tunakuwa pessimistic kama nilivyosema hapo awali.
Kwamfano pia,wale wanaomtetea kuhusiana na hatua yake ya kutokuyataja majina ya walio na fedha uswisi,wanasema kuwa ni jitihada zake binafsi za kuyapata majina yale na hivyo asisumbuliwe kuyataja bali ashukuriwe kwa jitihada hizo.Na pia hata yeye mwenyewe alishasema hivyo,kwamba ni jitihada zake na kuwa majina hayo yalikuwa yakiuzwa ghali kwenye cd's,sasa hapo inamanisha kuwa anataka manufaa binafsi?Je ni yapi?Anaziuza na yeye hizo cd zenye majina?Je kuna mtu ambaye hatopenda kuzinunuwa kama yumo kwenye list?
Je kuiepeleka kwake hoja ile kule bungeni kuna utofauti wowote ule vs kuyataja majina hayo?Binafsi ninaamini kuna utofauti mkubwa sana,na pia ninaamini kuwa kuipeleka hoja hiyo bungeni kuna nia ya kutaka kujisafisha kwake kwamba hayuko kwenye listi ile,maana wananchi watasema kuwa kama angekuwepo kwenye listi ile,basi asingepeleka hoja hiyo.Lakini wananchi hao hao hawajui kuwa kuna utofauti mkubwa sana na kwamba kutaja vyeo si sawa na kuyataja majina(vyeo haviwezi kushitakiwa wala kuhojiwa,bali majina).Hoja hiyo itakufa kama ambavyo nyinginezo zilishawahi kujifia.Na mwanasiasa atakuwa amekamilisha nia yake(kupumbaza wananchi kwa kutumia siasa).
Wanachama wengi hupenda kuongea kwa niaba yake kana kwamba wamjua (it may be true or not); na kuwasilisha hoja zao kana kwamba ni za mwisho (final say).
Hapo juu kwa mfano,hayo huwa yanatokea kwasababu ya utata wa wanasiasa.Watu kupendelea kuongea kwa niaba yake kana kwamba wanamjua,ni kwasbabu tu ya kukwepa kujibu maswali na kudharau.Hilo linapelekea watu kuongea kutokana na vile wanavyoona kuwa ni matokeo ya misimamo yake na hata maamuzi yake.Mara nyingi tu huwa anachaguwa kukaa kimya pale ambapo wengi tulidhani angesema jambo.Hilo linapelekea hisia za tofauti.Kuna maswali mengi tu keshaulizwa humu,si kwa utaratibu kama huu wa kwako,lakini kwenye threads mbali mbali ambazo either alianzisha yeye mwenyewe,ama member mwingine alianzisha.Ninakubaliana na wewe kuwa maswali yenye kejeli na matusi hayana nafasi,lakini si yote aliyowahi kuulizwa yana matusi na kejeli.Pengine cha muhimu ni member kujitahidi wajuwe namna ya kuuliza maswali.Kuna maswali ya muhimu sana lakini ni namna ya uulizaji ndiyo inakuwa shida kwa wengi wetu.
naomba tutumie hii fursa kuweza jua what Zitto is all about, what he thinks on certain issues, what he stands for, what he believes in AND why he thinks/ believes/stands for what ever it is that he postulates especially on what defines him... i.e POLITICS.
Hapo juu,ushauri wangu,ni kwamba hicho kipengele ungemtumia ili aandike makala ama essay inayoonyesha ama kusummerize hayo uliyoyasema hapo juu.Hilo litasaidia kwasababu tutakuwa tumeanzia kwenye higher standard given the fact that kunauwezekano mkubwa kukawepo na follow up questions.Na kwasababu style ya maswali na majibu inategemeana na wewe kuyachaguwa maswali,hilo halitaweza kutu guarantee kwamba follow up question zinaweza kuchukuliwa.(Najuwa kwenye "disclaimer",umeshasema kuna wasioridhika).Hivyo sidhani kama follow up questions zina maana ya kutokuridhika peke yake,ama haina maana kwamba kutoridhika basi ni jambo baya.Kwasababu ninakuhakikishia kuwa hatajibu maswali yote,na kuna ambayo atajibu kisiasa zaidi.Hilo ni kutokana na ukweli kwamba wanasiasa wanategemea kusikilizwa na wafuasi wao peke yake.Mara nying hawapendezwi na critics.Hilo huwa linachangiwa na ulevi wa madaraka ambao huwapa kiburi na kutokujali na madharau.
Pengine kwa kumalizia nikuulize,je follow up questions zitakubaliwa?Na je kuna idadi ya maswali ambayo mmepanga kuwa yatachukuliwa/kujibiwa?
Pia je kuna umuhimu wa kuweka dondoo za maswali ambayo atayajibu?Kwa mfano umetolea mifano ya maswali ambayo ni "personal",je umehsamwuliza limitation ya hayo maswali kuwa yepi haswa ni personal na yepi siyo?
Vinginevyo,nadhani angetuwekea misimamo yake kuhusiana na issues zinazoligusa taifa letu kwasasa ie udini,ufisadi,katiba mpya na mengineyo.Je anafikiri ni kweli kuwa chama chake ni cha kidini?Na kama ni kweli,tatizo hilo lishghulikiwe vipi?Je kama anafikiria kugombea urais,atalimalizaje tatizo hilo la udini?Mipango yake je?Ana mpango wa kuyataja majina ya wenye akaunti uswisi?Kama hapana,ni kwanini?Je akifanikiwa kuupata urais endapo atagombea,ana mpango wa kuwashughulikia mafisadi mara baada ya kuwaondoa madarakani?Je hilo litawezekana vipi ukitilia maanani ushirikiano wake na serikali ya ccm na wale wenye kutuhumiwa kuhusiana na ufisadi?
Pia aliposema mikataba iwekwe wazi,alikuwa na maana gani?Je ana maana kwamba ikiwekwa wazi hata sisi wananchi wa kawaida tutaweza kuiona?Ama alimaanisha ni wabunge peke yake?Kama ni wabunge peke yake,hilo litaleta utofauti gani kwenye bunge ambalo wabunge wake wanapiga kura za maamuzi kutokana na chama na si maslahi ya taifa?
Niishie hapa kwasasa.