EXCLUSIVE Interview with Zitto Zuberi Kabwe at Jamii Forums [Coming Soon]

EXCLUSIVE Interview with Zitto Zuberi Kabwe at Jamii Forums [Coming Soon]

Status
Not open for further replies.
Mh Zitto 2015 unagombea URais vip mpango wa Ndoa lini? au Katiba itabadilisha umri wa Urais na masharati ya Ndoa?
 
nimeona twitter moja toka kwa mtu anayejiita Daud Balali, akisema kuwa yuko hai, ila anaogopa kujitokeza hadharani kutokana na usalama wake. Na kwenye twitter hiyo aliitabiria kifo chadema na kusisitiza kuwa kabla ya 2015 Zitto na wenzie watatu ambao hakuwataja watahamia CCM. Nini msimamo wako kama kiongozi wa chadema?
 
Asante sana AshaDii kwa jitithada hizi,
Nimetumia muda wangu kupitia kwanza maswali ambayo watu wameshauliza kabla sijauliza maswali yangu, kwa bahati nzuri maswali yangu yote kwa Mhe Zitto yameshaulizwa kwahivyo sioni haja ya kurudia.
Tunasubiri kwa shauku kubwa hayo mahojiano....
 
Pamoja sana Ashadii..Mie swali langu litapatikana hapo hapo nikiwa nafatilia mjadala
 
zitto amekuwa aki-shine sana kama mbunge na waziri kivuli wa fedha bungeni,

je jambo gani la kujivunia alilolifanya kama naibu katibu mkuu wa chadema kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita?
 
AshaDii naomba umuulize Mhe. Zitto kutoka kwangu kama ifuatavyo:

1. Mgodi wa chumvi wa Uvinza uliouzwa kwa bei ya hisani kwanini hawalipii yale maji ya chumvi ambayo yapo aridhini toka kugunduliwa kwake miaka ya 1800's ("Brine") kwa kutumia "flow meter" kama mwananchi wa kawaida wa Kigoma Mjini ambaye analipia maji ya KUWASA kutoka ziwa Tanganyika? Je, wawakezaji hao waliuziwa hata mkondo wa maji ya chumvi yaliyopo aridhini wakati wao hawakuwa wagunduzi?

2. Pamoja na kuuziwa kiwanda hicho kwa bei ya hisani, kwanini bado wanaendelea kutumia nishati ya kuni kutoka kwenye miti asili ambayo hawakupanda wao badala ya kutumia nishati mbadala?

3. Namtakia afya njema!
 
ZITTO,ZITTO,ZITO........NANI KAMA ZITTO(Wangapi wanaweza kukubali kujitokeza hapa kuhojiwa maswali ya aina yoyote kama zitto)
Thanx ASHDIII kwa jitihada zako,Lakini pia Zitto wewe ni kiongozi wa mfano na kuigwa kwa hili.
SWALI LANGU LA MSINGI KWAKO RAIS WANGU WA KU-MOYO
>KWENYE SAFARI YAKO YA KUGOMBEA URAIS MWAKA 2015 KAMA UTAPITISHWA NA CHAMA NI MGOMBEA GANI WA CCM AKISIMAMISHWA UNADHANI ANAWEZA KIDOGO AKAWA MSUMBUFU.
otherwise,najivunia kuwa upande wako siku zote za Maisha yangu.
Mungu akupe afya njema,hata hili la kuhojiwa hapa ni ushindi wa heshima​
 
Good initiative;

Lakini kwa nini iwe yeye.....kwa nini tusingeanza na opinion pole ya nani tunamtaka in this time and space kati ya hao wanasiasa halafu wewe uchukue task ya kumtafuta huyo ambaye tungempendekeza badala ya kumleta yeye moja kwa moja na kudhani eti ni Golden Chance.............kama kweli ulikuwa unalenga golden chance basi ungewapa wadau nafasi ya kumchagua huyo golden occupier .......... I have a serious problem ya hii methodology yako!!!!!!

Katika huo mjadala majibu yake tuyachukulie kama.........

1. Objective truth???
2. As per his experience?????
3. Rationality?????
4. Convention????

Sababu ya maswali haya ni jinsi ulivyosema kuwa aulizwe maswali ya kujenga.......mjadala utakuwa moto...na kupata majibu ya kuridhisha

Mytake;Tusipokuwa na rationale juu ya haya mambo then the whole interview is subjected to a hell lot of criticisms and very prone to political inclination............or rather be subjected to and used as a political bridge...........!!!!!!!!
 
Nikiri kuwa mimi pia nina maswali ya kumuuliza na hata nikipata nafasi ya kukaa naye face to face tukizungumza tu yaliyo msingi na ndani ya maswali ambayo ninayo inaweza chukua sio chini ya masaa mawili ama zaidi. Naamini ningefanya jitihada zaidi hiyo nafasi ningepata...

Kwa muktadha huo Sijajihami Mkuu... Nimeona ni kheri nitoe tahadhari mapema sababu ni mpitaji mzuri tu hapa JLS, najua ni namna gani watu wanakuwa na sumu kali wakiona jina la Zitto ama lolote lihusulo yeye. Najua kuwa bila tahadhari basi tunaweza kuwa na pages za kejeli na tusipate yaliyo msingi. Nakuhakikishia kuwa maswali yote nitawakilisha na ndiyo maana nikaona nisiwe mchoyo wa hiyo nafasi nihusishe na members pia. Hivo Tukutuku kama una swali uliza na litafikishwa...

Karibu sana
.

Ili zoezi hili lionekane nila kidemeokrasia na hakuna uchakachuaji na kuwapotezea watu muda.
Zingatia hili .
1. Kabla ya muda wakufunga zoezi hakikisha unaweka maswali yote ambayo yako sawa kadri ya uhitaji wa hoja yako page ya kwanza kabisa ya tread hii.

2. Maswali yote yaliyoonekana ya kejeli nayo unayaweka ili members wawezekuyapima na kuona kweli si ya staha au la!
3.Itapendeza kama maswali utayaweka kwenye mtiririko mzuri ilikuweza kufualia vizuri maoni na mtazamo wa anayehojiwa (Zitto) (Maswali -1.Siasa,2.Uchumi,3.Elimu na Afya,4.Sheria(Usawa mbele ya Sheria,Katiba) .........

Naomba kuwasilisha.
 
kwa nini asjie tu hapa wenye maswali wakamuuliza? Yaani kwa nn maswali 'yachujwe' kwanza ndipo yeye aje (kama atakuja hapa au atayajibu kisha ww utuletee majibu sijajua) ayajibu?
 
Kwanini maswali yawakilishwe kwanza kwako kisha wewe ndio umuulize?Huoni mtakuwa mmeshaandaa
majibu?Kwa kuwa maswali yenyewe siyo yakuhitaji vielelezo toka kwa mtu mwingine,kwanini siku hiyo
asije mwenyewe hapa JF akaulizwa maswali na kuyajibu?Mbona Esther Wassira aliweza kufanya hivyo?
 
Bramo umeniacha njia panda kidogo... Tokana na maelezo yako hayo niliyo bold na ku color yanaenda tofauti na number-pointed points zako. Niwasilishe? Maana hayo yoote ni maswali na sio ushauri kama unavyodai... Ila itapendeza tuyawasilishe hivo hivo kama hutajali kama maswali.

Asha Dee, Namaanisha sio Kumuuliza tu bali na Kumpa ushauri, hayo maswali yangu kimsingi ni ushauri tosha kabisa, e.g badala ya Ni lini utaacha kutumiwa na CCM Kuidhoofisha CDM ningeweza kusema Tunakuomba uache kutumiwa na CCM kudhoofisha Nguvu ya CDM, ila nimeamua kutumia tafsida, kwa mtu mzima atakuwa amefikiwa na Message
 
Naomba unisaidie kumuuliza haya maswali mawili tu:

1. Kuhusu ndoto zake za kugombea urais,
je amefanya research ya kina kama kweli watanzania wanamuhitaji kuwa raisi wao? Au anasukumwa na hisia zake binafsi?.

2. Kuhusu matatizo lukuki za watanzania na waafrika kwa ujumla wao,
je nani ni tatizo, ni watanzania ama waafrika wenyewe kwa maana ya waongozwa ama viongozi wao?.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Tupate mda mwingine wa maswali mengine, ila kwa leo iwe ni juu ya fwedha za USWISS, tunataka majina, na jina la JK na Riz 1 lisikose plz
 
Asante sana kwa taarifa, kama mwanachama wa blog hii, napenda pia kuwasilisha maswali 2 ya kumwuliza Mh Zitto Kabwe.Na maswali yenyewe haya hapa chini japo yapo katika lugha ya kingereza. Nadhani hii si tatizo kwa kuwa Mh Kabwe anafahamu na kuzungumza kingereza kwa ufasaha. Si nia yangu ya kumtaka ayajibu kwa kingereza, kama ataweza kuyajibu kwa kiswali, kwangu mimi ni furaha zaidi, kwani lengo ni watanzania wajue. Au desk lenu kama litafanya jitihada za kuyatafsiri sawa lakini kuweni makini msije mkapoteza umaana wa maswali haya.
Qn 1. Tanzanians have lost faith in the Kikweteadministration on key issues like economy, foreign and domestic policies thatdon’t work for Tanzanians. From your experience as politician, can you tellTanzanians why the Kikwete administration has been slow or completely failed toprosecute corrupt officials? Could it be out of fear that those officials aredigging their own graves? What Chadema has to offer as an alternative to this chronic problem that escalates dayafter day if Chadema is to be elected in 2015. Here I mean those officials who weredirectly involved in Richmond, EPA, Meremeta, Kiwira, recent the ivory seizuretrade that implicates Tanzania in the international arena.Qn 2. Up tonow our country is relatively in a stable political and social atmosphere. Buti worry that this relative stable environment has been distracted following thediscovery of oil and gas where already some government officials have benefitedillegally (refer to your private motion in the HOUSE few weeks ago), UAMSHO hascampaigned hard to make sure that Zanzibar is independent from Tanganyika wherechaotic injustices have been occurred across the country, churches were burntand Tanganyikans were also attacked in Zanzibar. We know that there are hiddenhands on those issues I mentioned above. When will your party start interferingin order to restore country’s peace and unity. I need to know from yourpersonal point of view as well as your party’s position. What is your position toward the killings of DaudiMwandosya and your reactions to those report released by Mr. Nchimbi’s committeeand Human Rights report on the same matter? By JoshuaBukuru,Brussels -Belgium
 
ZITTO,ZITTO,ZITO........NANI KAMA ZITTO(Wangapi wanaweza kukubali kujitokeza hapa kuhojiwa maswali ya aina yoyote kama zitto)
Thanx ASHDIII kwa jitihada zako,Lakini pia Zitto wewe ni kiongozi wa mfano na kuigwa kwa hili.
SWALI LANGU LA MSINGI KWAKO RAIS WANGU WA KU-MOYO
>KWENYE SAFARI YAKO YA KUGOMBEA URAIS MWAKA 2015 KAMA UTAPITISHWA NA CHAMA NI MGOMBEA GANI WA CCM AKISIMAMISHWA UNADHANI ANAWEZA KIDOGO AKAWA MSUMBUFU.
otherwise,najivunia kuwa upande wako siku zote za Maisha yangu.
Mungu akupe afya njema,hata hili la kuhojiwa hapa ni ushindi wa heshima

Tunataka maswali ya live, haya maswali ya kupelekewa inakuwa kama kupanga matokeo, halafu wewe ushabiki wako kwa Zitto hata Zitto huwa anachukizwa na wewe
 
Tatizo langu nilishampuuza na kumdharau Zitto, wala sina muda wa kumuuliza lolote Kijana anayejiona ni Unique na mwenye akili kulliko wengine.
 
Jukwaa pekee la vyama vya upinzani kuibana serikali baada ya uchaguzi ni bungeni, bungeni ni mahali panapohitaji watu wenye uwezo binafsi wa kujenga hoja zenye mashiko na uwezo wa ku-analyse different issues.
Ukiacha wabunge waliogombea kwenye majimbo ambako vigezo vya kupita huko viko nje ya control ya chama, nafasi pekee inayobaki ambayo chama cha upinzani kinayo kuingiza vichwa vitakavyoibana ccm bungeni ni wabunge wa viti maalumu, kuna mkakati gani wa chama kuhakikisha kinapata wanawake wenye uwezo binafsi wa kujenga hoja zenye mashiko ili kuweza kuziba pengo pale waheshimiwa wengine (tuliowazoea) wanapokuwa hawapo au nafasi zao za kuchangia zimeshapita, na kuna issues muhimu zinahitaji kuongelewa.
Hii nimeiona katika vikao vingi, hawa wabunge wa viti maalumu wa chadema, ni wachache sana wanaoweza kujenga hoja kwa uwezo wao binafsi, hivyo serikali imejikuta inapumua mara nyingi sana pale wabunge wa viti maalumu wanapochangia, kwa sababu mara nyingi hata vitu wanavyoongea hata wao wenyewe hawavielewi, yaani kwa chadema naona afadhali ya mashishanga, ila ukianza na naomi kaihula na mngodo in wachemfu balaa, yaani wataongea mambo ambayo hata hayaeleweki. Hawajui kuwa nafasi hizo ni muhimu kwa vyama vya upinzani kuiumbua selikali. Wengine hata kuchangia siwaoni.
Hizi nafasi za viti maalumu ndio nafasi pekee chadema wanaweza kutafuta suplement ya kina mnyika, zito, wenje, mbowe, tundu lisu.
Otherwise mtu akiangalia list ya wachangiaji akakuta hao hawapo basi anabalisha channel
 
2.Unafikiri chadema uliyoiasisi na kujitolea kwa nguvu zote kutaka kiwe chama makini ndiyo hii ya sasa au kuna mabadiliko?Kama kuna mabadiliko ni yepi na unafanya nini kufanya chadema iwe kama ambavyo ulitaka iwe?
Ni tangu lini Zitto ni Muasisi wa Chadema!? unajuwa maana ya Muasisi? huu ndio ujinga uliojaa kwa watu walioijuwa Chadema kuanzia mwaka 2005.

Steven Wassira ni miongoni mwa wasisi wa Chadema na si Zitto Kabwe.
 
Mh. Zitto amesikika akitangaza nia ya kutaka kugombea Uraisi kwa kupitia CHADEMA 2012,sasa maswali yangu ni kama ifuatavyo

1.Je haoni hii ni mapema zaidi kutangaza lengo hili kwa kuwa sasa hivi ni muda wa kujenga Chama?.Je, haoni kwamba inaonyesha ana uroho wa madaraka,na pia anavuruga harakati za chama kufikia malengo yake ya kufikia wanachama wengi zaidi?
2.Je,ikiwa 2015 hatateuliwa kuwania hiyo nafasi atachukua hatua gani?.
3Inasemekana kwamba Zitto anatumiwa na CCM kuivuruga CHADEMA,je,yeye anasema nini?.
4.Je,haoni umaarufu wake unapotea siku hadi siku kutokana na yeye kuropoka hovyo hovyo bila kufuata utaratibu wa chama?.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom