Ningekuwa Lowasa kujibu lile swali la usingekatwa kwenye chama chako ungekuwa unayasema unayoyasema sasa?
Ningejibu hivi "Kila anayeamua kufanya jambo fulani huwa na maono yake binafsi,maono yangu yalikuwa kubadilisha hali ya uchumi na maisha ya watanzania kwa ujumla.Hivyo ili kufanikisha maonoyangu niliishapanga watu ambao ni makini lakini hawapewi nafasi kuonyesha uwezo wao wa kiutendaji,hawa ningewapa uwezo wa kufanya maamuzi kisheria,lakini wenzangu walihofia hilo wakakata jina langu ili nisiuvunje mfumo uliopo,nalazimika kuyasema ninayoyasema sababu hawawaambii watanzania ukweli bali wanaishia kunichafua badala ya kusema ukweli"
Huu ni mtizamo wangu,lakini nampongeza EL,kwa uwezo wake wa
kujieleza na hii ndo dawa kama vyombo vya habari ndani ya nchi vina mizengwe
tumieni vyombo vya nje,achana na story za midahalo haina tija
watu wanaposema duniani kote watu wanafanya hivyo
sisi siyo duniani kote,sisi ni Tanzania,mbona nchi tunazotaka kuziiga kufanya
midahalo hatuziigi mbinu zao za kukuza uchumi na kukomesha rushwa?
Sisi ni nchi ya kipekee,yenye muungano wa nchi mbili ukazaa nchi moja yenye serikali mbili na marais wawili.
Ni nchi pekee yenye amani lakini wenzetu albino wanaishi kwa hofu kuu.
Ni nchi pekee ambapo raia wa maisha ya chini huadhibiwa
kwa sababu ya makosa ya wafanyabiashara wasiowaaminifu kama njia ya kuwadhibiti
wafanya biashara hao, refer bei ya mafuta ya taa kupanda bei.