Ewura: Bei ya gesi ya kupikia imepanda kwa kati ya Tsh 2000 hadi 5000 kutokana na kupanda kwenye soko la dunia

Kwanza tuliambiwa hiyo gesi mabomba yanaelekea ulaya, halafu tukaambiwa sio yetu tena, kwa haya yanayoendelea sasa naamini hizo kauli, seriously kuna mtu anatakiwa kutolea maelezo hili suala la gesi, utawala wake uliacha maswali mengi sana kuhusu hii gesi yetu.
 
Hapo mliozamia dar mtakoma.. Naomba wapandishe iwe 80,000 na lita ya petrol iwe 4,000 huku nauli zikiwa 800 kwa safari ili mbowe, lisu, cov 19, mnyika na chadema wakome. Ccm hz bei hazimahus au nasdma uong6 ndg zng?
 
Atafutie wapi hela wakati anafukuzwa mjini anaambiwa Anachafua mji?

Usimcheke ukadhani wewe uliye na visenti kidogo vya kubadilisha mitungi ya Gess uko salama.

Tambua kwamba nguvu kazi hii ikikosa maali pakutafutia kipato kwa kufukuzwa na migambo watarudi kwako na mtagawana hicho kidogo ulichonacho.
Tafuta hela wewe uache kulialia kama mbweha kwa vitu vidogo vidogo
 
sio kweli..
.
kuna vitu inakulazimu ufanye sio kwa sababu unavimudu bali ni kwa sababu ni basic need yani bila hivo maisha hayaendi.
Remember the invisible hands of the market which controls,supply of goods and demands of goods prices.
 
Gas si inachimbwa mtwara hapo sasa imepelekwa huko kwenye soko la dunia ndio ikaletwa huku au?

Nimewaza tu kwa kutumia tumbo
 
Atafutie wapi hela wakati anafukuzwa mjini anaambiwa Anachafua mji?

Usimcheke ukadhani wewe uliye na visenti kidogo vya kubadilisha mitungi ya Gess uko salama.

Tambua kwamba nguvu kazi hii ikikosa maali pakutafutia kipato kwa kufukuzwa na migambo watarudi kwako na mtagawana hicho kidogo ulichonacho.
Waje tu niwagawie.
 
Wauza gesi hawafurahishwi na uwepo wa misitu nchini na wamedhamiria kuona miti iliyopo inakatwa Kwa ajili ya kuchoma mkaa! Huenda hata kwenye biashara ya mkaa wamewekeza ili kutengeneza faida kwenye nishati ya mkaa na gesi!
Serikali itupie jicho upande huu wa gesi ili kuokoa misitu yetu ambayo ni chanzo Cha mvua na moto. Vinginevyo nchi itageuka jangwa na kuzidisha mgao wa umeme na maji uliopo Sasa!
Ikimpendeza Rais atengue uteuzi wa meneja wa eura Kwa kushindwa kwake kuitetea miti yetu na badala yake anawatetea wauza gesi ambao watasababisha ukame na mgao wa maji na umeme! Gesi ipangiwe bei elekezi ambayo ni rafiki Kwa mtumiaji! Inawezekana hata Kama serikali itajenga kiwanda Cha kuisindika gesi hiyo na kuuza Kwa bei tahafifu!
 
Ukiona mfanyab8ashara amepandisha bei ya kitu na bado watu wananunua tu, ujue watu wanamudu.

Watu wakishindwa kununua kwasababu ya bei maana yake, itabidi wafanyabiashara washushe bei ili mzigo uende.

Hilo ndio soko huria.
Tumia akili kidogo...kuna vitu hata vikipanda bei bado watu wanalazimika kununua ila kwa maumivu makali.
 
Gas si inachimbwa mtwara hapo sasa imepelekwa huko kwenye soko la dunia ndio ikaletwa huku au?

Nimewaza tu kwa kutumia tumbo
Gesi ya mtwara ni gas asilia
Ilibidi tuunganishiwe direct bila kuwekwa kwenye mitungi
Hii ya kwenye mitungi inatoka wanapochimba mafuta huko
 
Gas si inachimbwa mtwara hapo sasa imepelekwa huko kwenye soko la dunia ndio ikaletwa huku au?

Nimewaza tu kwa kutumia tumbo
Gas ya Mtwara ikiisha kuchakatwa inaitwa LNG (Liquified Natural Gas) hii iliyokuwa ikijadiliwa hapa ni LPG (Liquified Petroleum Gas) inatoka huko yanakochimbwa mafuta jamii ya petroli.

Hii ya kwetu bado haijaanza kuwekwa kwenye mitungi midogo midogo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Sana sana wapo wateule wachache wamefungiwa miundombinu wanapelekewa Gas ya Mtwara/Lindi mpaka majumbani kama maji ya Dawasa.
 
Back
Top Bottom