vampire123
JF-Expert Member
- Apr 17, 2016
- 1,310
- 869
Samaki anatapatapa nchi kavu
Bwana Huyu baada ya kulalamika kwamba biashara zake zinamwendea kombo ,kupunguza wafanyakazi na kuhamia kwenye ofisi ya bei rahisi,sasa naona anajikomba kwa watawala angalau wamkumbuke uDC!Nawewe unataka kuwa mjinga.Hata kama Rais kasema, mihimili mingine inaweza kulisimamia hili swala kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.Au sheria inasemaje?
Mkuu, huyo unaejaribu kumpa uelewa hawezi kukuelewa ng'oo, hapo ndipo iq yake ilipoishia, usimjaze zaidi atapata kifafa cha ubongo, hebu soma comments zake itajua nini nakwambiaUkosefu wa akili na busara ni jambo baya sana.
Wewe huoni mnazidi kuwarahisishia kazi yao hao mabeberu kwa juhudi zenu za kuwatengeneza unaowaita "vibaraka?"
Mtu kama unayo akili nzuri na unajua tabia za hao wanaokuzonga, utafanya kila juhudi za kuwanyima fursa hiyo. Unafanya mambo yako bila kuzalisha vibaraka.
Sasa, kwa mifano uliyotoa hapo juu, matokeo yake tunayajua. Kama mtaendelea kuzalisha 'vibaraka' na nyinyi mtakumbwa na kimbunga kile kile kilichowakumba Ghadafi na Saddam.
Mnaandika propaganda nyiiingi hata zisizo na maana badala ya kutuambia ni vipi tutajaza nakisi iliyopo kwenye bajeti yetu bila kuwategemea hao, mnaowaita "Mabeberu". Hayo ndiyo tunataka kufahamu sio mambo ya umbeya umbeya haya uliyoandika. This is utter rubbish, we want solution not propaganda or rhetorics.Historia huwa haipotei na kamwe haidanganyi. Wananchi wa Libya waliambiwa na Mabeberu kwamba Ghadafi ni tatizo na iwapo akiondoka madarakani wananchi wa Libya wataishi maisha mazuri sana. Hebu tujiulize: Wamarekani waliongoza mapambano ya kumuua na kumuondo madarakani Rais Muamar Ghadafi, JE, Libya wana maisha gani mazuri leo hii zaidi ya mateso makali?
Walibya waliahidiwa kwamba Ghadafi akiondoka madarakani nchi ya Libya itakuwa na Demokrasia safi na ya kweli. Hebu tujiulize: Iko wapi hiyo Demokrasia nchini Libya baada ya Mabeberu kumuua Ghadafi? Hakuna Demokrasia zaidi ya mateso nchini Libya na maisha magumu.
Tusisahau yanayowakuta Iraki na Siria kwa Bashar Asad ambapo mabeberu wanataka kupandikiza vibaraka wao ili wachote rasilimali ya mafuta kwa manufaa yao. Kote huko ni mateso makali. Walimuua Rais Saddam Hussein na kuwahakikishia wana dunia hii kwamba Iraki itakuwa na Demokrasia na maisha mazuri. Tujiulize yako wapi maisha mazuri Iraki zaidi ya machafuko yasiyoisha tangu Mwaka 2003 hadi leo hii?
Watanzania tunapaswa kutumia yanayowapata Walibya na wairaki kujifunza kwamba kamwe Mabeberu wa Ulaya na kwingineko duniani hawawezi kusimama na serikali yetu pale wanapoona tunajenga uchumi wetu ili tujitegemee. Lazima tufahamu kwamba watatuchonganisha na kupandikiza vibaraka wao nchini wakiwemo waafrika wenzetu ambao leo hii tunawaona wakidiriki kupigia upatu Mashinikizo yao ya kijinga yakiwemo ushoga, Mara wanatetea demokrasia yetu nk.
Wameshindwa kuisadia Libya na Iraki kama walivyoahidi na kuaminisha ulimwengu kwamba kuna matatizo makubwa ya kidemokrasia katika nchi hizo nk, hakuna amani huko zaidi wamesababisha machafuko makubwa katika nchi hizo; watawezaje kutusaidia sisi watanzania tena Taifa letu ambalo tuko salama sana, hatuna matatizo kama wanavyoeleza mabeberu na vibaraka wao?
Mabeberu hao wasiofaa hata kidogo wamekaa kimya kuhusu yanayoendelea nchini Ufaransa kana kwamba hawaoni kitu. Watu wanaandamana mwezi mzima kumshinikiza Rais Emmanuel Macron aondoke madarakani lakini tujiulize ni lini Mabeberu wa EU na vibaraka wao walitoa tamko lolote kumshinikiza beberu mwenzao aondoke madarakani? Watanzania sharti kustukia maigizo ya mabeberu na uonevu dhidi ya mataifa ya kiafrika.
Kudhibiti Makinikia na biashara harama za kutupora madini yetu haijawapendeza wazungu hata kidogo na kwa hiyo basi wameamua kupambana na sisi kwa namna mbalimbali ikibidi hata watufarakanishe ili nchi yetu ipoteze mwelekeo na isitawalike. Mabeberu wanatueleza wanapigania demokrasia ndani ya nchi yetu wakati wanajua fika walitoa ahadi ya aina hiyo kwa Libya na kwingineko duniani lakini hadi leo hii Libya hakuna demokrasia wala amani bali machafuko.
Walibya wanajuka kukubali kuhadaiwa na mabeberu, wanamkumbuka ghadafi na kujuta sana kuuawa kwa Rais Muamar Ghadafi. Wanakumbuka fadhila za Ghadafi aliyekuwa akiwapatia malipo ya chakula kila mwezi wananchi masikini, leo hakuna malipo hayo. Wanamkumbuka ghadafi aliyekuwa akiwalipia mahali za kuoa walibya masikini lakini leo hakuna fadhila hizo. Wanamkumbuka ghadafi aliyeapa kupambana na ubeberu ili usiitawale afrika. Ghadafi alijipambanua kama kiongozi asiyetaka kuona Afrika inaonewa na kushikizwa kufanya mambo ya kijinga kwa maslahi ya mabeberu.
Watanzania tupeuke mtego uliowamaliza walibya ili tusije kujuta kama walibya leo hii. Hawa vibaraka na vijakazi wa mabeberu wanaopiga kelele kwamba Tanzania tunaenda vibaya hawana mana kabisa bali wanatumikia mabeberu wanaotaka kututawala ili wapole rasilimali zetu. Hawa vibaraka na mabeberu wao tuwaogope kama Ukoma.
Pinga UBEBERU NA VIBARAKA wao wote kwa maslahi ya Taifa hili.
Maazimio ya EU yanapaswa kutafsiriwa kuwa ni uingiliwaji wa masuala ya Taifa Huru. Kwa nini hawakutoa azimio dhidi ya Donald Trump kwa kauli yake ya kupinga ndoa za jinsia moja? Wana njama dhidi ya Waafrika na wanashtushwa na utekelezaji wa Rais Magufuli
Unamjua aliyekupa uhuru?Maazimio ya EU yanapaswa kutafsiriwa kuwa ni uingiliwaji wa masuala ya Taifa Huru. Kwa nini hawakutoa azimio dhidi ya Donald Trump kwa kauli yake ya kupinga ndoa za jinsia moja? Wana njama dhidi ya Waafrika na wanashtushwa na utekelezaji wa Rais Magufuli
Wakifi.wa wao mnaumiaje nyie?Huo ndio ukweli ...muungano wa vyama vidogo vidogo vya kutetea mashoga vimetumia mwamvuli wa EU kuandaa Resolutions zenye ajenda ya kutulazimishia Ushoga.
Hatutaki hiyo tabia watuletee hukuWakifi.wa wao mnaumiaje nyie?
kwa hiyo ulitaka tusipewe uhuru?Unamjua aliyekupa uhuru?