Ni upumbavu mtupu, kurupuka ya kapuku
Uzamivu wa wivu, uza mbivu kwa saba buku
Baba kakaba LUKU, siasa kahaba shuku
Sio Wamakonde Maraba lakini kwa mahaba ya kuku
Tutakula mpaka panya buku chukuchuku
Dukuduku, OSS, aliye juu mpandie, usimngoje hukuhuku
Chai kwa pipi, sukari kiki
Elimu bure vipi huku redio unafungia?
Misukule pipi wenzio unatuungia?
Idi Amin asiye makini, nyama la baharini
Majina manne ubini, diva kwini, kingi wa magirini
Pol Pot, Ze Comedy Joti, baba mkusanya noti
Gusa shoti, samasoti, mwendo wa speedboti
Baba bwabwaja, jinga la haja, baja kaja
Paji kaa paja, Opobo Jaja, Black Maharajjah
Bwabwa kiporo, watu kihoro, limelala doro
Chini godoro, Dar mpaka Moro, twapitia Muhoro?
Serikali kali, bila uhalali, kwa mtaji wa shari
Hii manuwari, itenda muhali, vipi hadi dahari?
Chama mrama, ndama kapama, maziwa yahama
Hili drama la karma kama Obama na Osama