Eti uchochezi, uchochezi gani?

Eti uchochezi, uchochezi gani?

Huu uzi unazungumzia ukweli na uwazi yani nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi ila nasikitika hautadumu kwa sababu ya mikwara iliyopigwa mitandao na media.
 
Anaweza akawa Rais wa awamu moja.

Watu kama akina January usione wapo kimya, waswahili wanasema ukiona Kobe kainama ujue anatunga Sheria.

Miezi 10 madarakani, kaharibu kila kitu. Wananchi, Wanasiasa, Wafanyabiashara hata Watumishi hawana amani na huyu jamaa!!
 
Napata wasiwasi sana mpaka sasa JF haijafungiwa. Sijuwi kama tutaweza Ku survive kutokana na huu mwenendo.
 
Maisha ni magumu sana kwa upande wangu,,sitaki kusikia lolote lile.tangu utawala huu uingie biashara zangu zinayumba vibaya sana.[HASHTAG]#uchochezi[/HASHTAG] huu#
 
Hil la Uchochezi ni tishio kwa upinzani na hata kwa wenye maoni tofauti... ngachoka
 
I saw this coming
kwenye kampeni alim praise Gaddafi..
you can imagine

akakataa kufanyiwa interview na BBC
akakimbia kabisa debates.....
hanishangazi kabisa

Unajua uhuru ni kitu kizuri sana maishani.

Watu hata kama wako maskini lakini wakiwa na uhuru watajisikia vizuri na watakuwa wenye furaha.

Sasa huyu jamaa hata mwaka hajamaliza tayari keshatengeneza hali na mazingira ya watu kujisikia hawako huru.

Kama kuna mchochezi namba moja basi usitafute mwingine zaidi ya Magufuli.
 
Hizi habari za uchochezi mimi sizielewi kabisa.

Hao watu wanaotuhumiwa sijui kuchochea, wamechochea kitu gani?

Kumpindua Magufuli?

Huyu jamaa asipoangalia anaweza kutumia muda wake mwingi kupambana na watu wenye maoni na hisia ambazo zipo kinyume na atakavyo au apendavyo yeye.

Katika viongozi ambao Tanzania imewahi kuwa nao tokea tuanze kutawaliwa na CCM huyu jamaa atakuwa anaongoza kwa kutokuwa na busara wala hekima.

Hovyo kabisa!

Sitashangaa JF nayo ikifungiwa kwa kupromoti uchochezi wa akina Ngabu😉.
Hata bila jf sauti zitafika tu
 
Kama huzielewi habari za uchochezi kwa nini usiende mahakamani kuuliza ili ueleweshwe?

Hekima na busara hazipimwi kwa kutumia hisia yako.

Rais hana hekima wala busara kwa mujibu wa nani?

Kuishi katika dunia ya fikra zako haina maana ndivyo dunia ilivyo.
 
Alipoanza kazi si mlisema anafuata ILANI ya chama chenu huyu?
Chama chetu kipi? Sina mahaba ya kipumbavu kwenye chama chochote cha siasa.nasapoti nachokiona ni sahihi .nilimpigia kura Magufuli na kwa upande wa utekelezaji wa Sera zake nakubaliana nao kama kuzuia rushwa, kupunguza matumizi ya serikali n.k . Lakini hili la kuwakamata wanaomkosoa, kuzuia mikutano ya vyama vya siasa sikubaliani nae.
 
Sorry mkuu but it wasn't ur reply nilikosea tu ilikua ya mkuu Nyani Ngabu
 
Kama huzielewi habari za uchochezi kwa nini usiende mahakamani kuuliza ili ueleweshwe?

Mahakamani wana idara au kitengo cha ueleweshaji?

Hekima na busara hazipimwi kwa kutumia hisia yako.

Kwa hiyo zinapimwa kwa kutumia hisia zako wewe?

Rais hana hekima wala busara kwa mujibu wa nani?

Kwa mujibu wa Nyani Ngabu.
 
Kiukweli sikuwa nafahamu kama CHADEMA wanatisha na wanaogopeka kiasi hiki, umarufu weka umepaa ndani ya wiki tatu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kuliko wakati mwingine wowote tangu kusajiliwa kwake, mbinu hii imefanikiwa kwa 100%.
 
Mi nachochea kitandani tu. Hao wengine wanaokamatwa sielewi wanachochea kitu gani.
 
Back
Top Bottom