Eti Pisi (Wanawake) wa JF ni wabovu? 🙆🏿‍♂️

Eti Pisi (Wanawake) wa JF ni wabovu? 🙆🏿‍♂️

Tatizo watu wana matarajio makubwa sana juu ya watu walio mitandaoni bila kujua kwamba tuliomo humu ndio tupo na mitaani. Wanatamani member wa jf tuwe wazuri kama malaika😌😌😌.

Ila ule uzi wa selfika ufutwe tu. Ukisoma ule uzi sio wanaume tu, hata wanawake kutwa nzima kutukana na kudhalilisha wanawake wenzao. Unakuta mwanamke kila siku ni ku body shame wanawake wenzao. Sasa kama sisi tu tunadhalilishana namna hiyo ndio iwe kwa wanaume?
We dada nimekupenda 💯
 
Wasalaam wakuu,

Kumekuwa na tabia mbaya humu JamiiForums ya baadhi ya vijana wa kiume kuanzisha nyuzi au kutoa comments za kuwakejeli na kuwabeza wanawake baada ya kuona picha zao kwenye jukwaa la Selfika.

Kwa kweli hii inasikitisha na inatufedhehesha wanaume.

Kaka, kama hujapendezwa na mwonekano wa dada fulani, pita tu. Si lazima kila unachokiona ukikosoe. Huna jukumu la kuwa jaji wa sura, miili au thamani ya wanawake wa JF.

Jiulize: Unapata faida gani kumdhalilisha mtu? Maisha yako yanabadilika? Unakuwa mwanaume bora? Au unajisikia tu vizuri baada ya kumuumiza mtu ambaye hakukufanya chochote?

Mwanaume mwenye kujitambua anajua tofauti kati ya preference na disrespect. Unaweza kusema “si aina yangu” bila kumdhalilisha mtu.

Na kabla hujaandika comment ya kumkejeli mwanamke kwa mwonekano wake, kumbuka nyumbani kwako kuna mama, dada, shangazi, mke au binti. Je, ungefurahia mwanaume mwingine akiwadhalilisha kwa namna hiyo?

Uhuru wa kuandika sio ruhusa ya kukosa staha.

Kijana, tafuta KISUDI cha maisha yako. Fanya kazi zako, biashara yako, familia yako na akili yako. Dunia ina mambo mengi ya kutatua kuliko kukaa nyuma ya keyboard kuwavunjia wanawake heshima.

Kumshusha mwanamke hakukufanyi uwe mwanaume zaidi.

Kama picha haikupendezi, scroll down.
Kama sio type yako, endelea na maisha yako.
Lakini heshima ibaki.

JamiiForums ni sehemu ya mijadala, sio uwanja wa kuwavunjia watu utu

Mwanaume wa kweli hahitaji kumdhalilisha mwanamke ili ajisikie yeye ni mwanaume
Fact
 
Kuna huyo Gunner kizibo na kuna mwengine anajifanya dokta uchwara sijui yupo Marekani mara analewa muda wote, lol, ukiwasoma michango yao unaona kabisa ni watu wanaohitaji msaada wa afya ya akili, hawapo sawa msiwazingatie sanaa
 
Yeah, miaka ya mwanzo ya ule uzi tuliufaidi sana interactions za picha na stories, mambo yalikuwa poa. Wakaja watu wapumbavu kazi yao kusimanga, kuteta wenzao na sisi wengine tukaondoka!
Nakumbuka kipindi hicho akitokea mwanaume amemsema vibaya mwanamke kwenye ule uzi wanawake wote walikuwa wanajoin forces huyo mwanaume ataukimbia tu huo uzi.

Sijui ni nini kilitokea hapa katikati sisi kwa sisi tukaanza kutafunana😌😌. Na baadhi ya wanaume wakapata nguvu ya kututumia sisi sisi wanawake ili tuwadhalilishe wanawake wenzetu huku wamekaa pembeni mikono misafi. Badala ya mwanamke kusimama kumtetea mwanamke mwenzake yeye ndio kwanza anamkandamiza kwa kutumia resources alizotumiwa na wanaume.

Wanawake tumejua kutumika kuchafuana. Sasa wanaume wakisema sisi ni wabaya haishangazi kwa sababu sisi wenyewe kila siku tunasemana sisi ni wabaya.
 
Sana. Mwanzo huo uzi haukuwa hivo kabisa.
Sasa hivi kama unapata trauma kuona mtu anadhalilishwa, anatukanwa kisa ni mfupi, kisa umbo baya, kisa mweusi, kisa mnene, kisa hana nguo nzuri, wala usijaribu kusogelea ule uzi utakuwa traumatized.
Ndio maana mimi niliukataa tangia siku ulioanzishwa 😁😁 trauma nilizozazo kwenye real life zinanitosha
 
Nakumbuka kipindi hicho akitokea mwanaume amemsema vibaya mwanamke kwenye ule uzi wanawake wote walikuwa wanajoin forces huyo mwanaume ataukimbia tu huo uzi.

Sijui ni nini kilitokea hapa katikati sisi kwa sisi tukaanza kutafunana😌😌. Na baadhi ya wanaume wakapata nguvu ya kututumia sisi sisi wanawake ili tuwadhalilishe wanawake wenzetu huku wamekaa pembeni mikono misafi. Badala ya mwanamke kusimama kumtetea mwanamke mwenzake yeye ndio kwanza anamkandamiza kwa kutumia resources alizotumiwa na wanaume.

Wanawake tumejua kutumika kuchafuana. Sasa wanaume wakisema sisi ni wabaya haishangazi kwa sababu sisi wenyewe kila siku tunasemana sisi ni wabaya.
Kuna crew ya wadada, ilipojimilikisha tu selfika nikaona hapa hapafai tena, wapo kutafuta mipira iliyokufa ili wapate topics.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom