Eti hatujui... kipimo gani kinatumika?


Carol,

Hapo kweli hakuna mahaba hata kidogo...Hizo elements ulizozitaja zikishapotea basi tu...Maisha yanabaki kuwa ya mazoea na malezi ya watoto!!

Nakubaliana na wewe kwamba mambo mengine ni sumu kuyajaribu tena kama umri wenye umeshachapa mwendo!
 

Wewe Moria sasa unaleta kionjo kipya kwenye mjadala...Kufanywa mapema unamaana kabla ya kuzama bedroom au kabla umri haujaenda?

Hebu tufafanulie kidogo,
 
Mhhhh...Sasa na wewe unataka kutoa mpya,

Hivi inawezekanaje uzae watoto (siyo mtoto) na mtu yule yule kwa kubakwa??? Halafu ukae naye mpala mnaona wajukuu!!

Bwana hapo mahaba yapo hata kama siyo kwa vigezo vyenu!!

Babu walioko kwenye abusive relationships wanawezakutoa ushuhuda juu ya hili. Haki zao za ndoa zinabakwa na wanajikuta wanalazimika kuendelea kuzaa kwa kuwa tu ni wajibu wao kama mke.
 
Wewe Moria sasa unaleta kionjo kipya kwenye mjadala...Kufanywa mapema unamaana kabla ya kuzama bedroom au kabla umri haujaenda?

Hebu tufafanulie kidogo,

DC mahaba lazima yaanze mapema kabla ya kuzama room...baba ni busara arudi kwake mapema apokelewe(zawadi)...amjulie hali mkewe atamweleza yaliyojiri huko..naye ataelezwa yaliyojiri home(w'ke hupenda kusikilizwa) hapa ndipo mke huangushiwa sifa za kutosha na mumewe pamoja na chokozi mbalimbali macho yakiwamo...kwa room nako mapema ni busara kuzungumza,kusifia,KUSIKILIZA,kubembeleza nk...maandalizi haya humsaidia mume kujicontrol(45min first half)..hapa mke huangusha kilio-huba cha ukweli..
 

Hapo kwenye zawadi hapo mpenzi wangu ndipo palipozua makubwa...............haya ukija na mboga kwa ajili ya chakula cha jioni si ni zawadi? au wajibu?

Huko kwingine mwe.......naomba niwe mwanafunzi wako tafadhali!
 
Ndiyoo...siyo Bosi tu..na sisi tumekuelewa..
 
Hapo kwenye zawadi hapo mpenzi wangu ndipo palipozua makubwa...............haya ukija na mboga kwa ajili ya chakula cha jioni si ni zawadi? au wajibu?

Huko kwingine mwe.......naomba niwe mwanafunzi wako tafadhali!

Mboga itategemea uspecial wake yaani imeletwa kama zawadi(chachandu)? la utakuwa ni wajibu tu ... zawadi ya mamaa shurti itengwe atii..na iwe na salam wakati wa kupewa..
 

....nadhani kwa jinsi utetezi wa kuletewa kuku na gunia la mkaa unavyoendelea hapa, mbu napata picha kinachotetewa hapa ni uhalalishwaji wa kwamba ni "wajibu wa mke" kutafuta kuni za kupikia chakula cha mumewe na familia, ndio maana siku akimuona mumewe kamtunuku kumletea gunia la mkaa ashukuru!

....hilo la kuku, linanikumbusha "jukumu' la mke" kutafuta
matembele, kisamvu , uyoga nk kwa mlo wa familia...
na siku mume akibahatika kuleta kuku basi firigisi, paja na kidari atatengewa mume....---na watoto waambulie shingo na vipapatio huku wakiambiwa 'furahieni sikukuu yenu leo....!'
 

Loh kwa tafsiri hii Mbu itanibidi tu nibwage manyanga chini na kusubiri mahaba.
 
Loh kwa tafsiri hii Mbu itanibidi tu nibwage manyanga chini na kusubiri mahaba.

....mfumo dume at 120km/h....

sio mjini sio vijijini...wa mjini ataachiwa shs 1000/= abajeti kila kitu, mkaa, ndoo ya maji, nyanya, mchele, nazi, vitunguu, na jioni mume akirudi akute chakula cha kumtosha, ale ashibe na maji ya kukoga tena ya moto yawepo bafuni...
ni juu ya mwanamke ku bargain huko na wauzaji gengeni/sokoni....

...mahaba hayo!
 

Mbu ni kweli tunashindwa kutofautisha wajibu na zawadi...pakiti ya karanga au korosho aliyofichiwa inaweza kuwa na matokeo mazuri kuliko hiyo migunia ya mkaa...mkaa umeisha ni wajibu baba ulishughulikie..
 
Duh..mitihani..
 
 

Hongera sana Brother,

Naona sasa umelielewa somo...Ningesikitika sana kama hii thread ingefungwa kabla hujakombolewa.....Waliobaki tutawakomboa kwa njia nyingine. At least wewe tumekulopoa huko ulikotaka kuzamia!!
 
Reactions: Mbu
Ha ha ha umepatia kabisa mie flat screen haihuu kabisa mie ni 6*6 ndo mpango mzima

Mimi nimewaeleza hawa watoto na sijui kwa nini haelewi...Kama mahaba yatarutubisha mbegu ili zizae matunda bora kwenye samba la 6x6 basi hayana maana hayo.....

Karibu sana na msaada wako kwa hili umekuwa-appreciated kuliko unavyoweza kudhani!!

Miss u so much though!
 

Hapa sasa unaongelea issues kama kile kisa cha Mpemba...Kwangu mimi hayo ni mahaba feki!!

Jibaba la nguvu linaacha 5000/- na likirudi linabeba mazagazaga mengine (eg. maandazi, vitumbua, ubuyu, machenza, miwa ya paketi n.k) ili mradi kila mtoto anayeenda kumpokea baba arudi ndani na kifurushi!!!!

...Hapo mama asifurahie na kuwa na mashamu shamu (yatakayokoleza mahaba) kwa nini? Labda kama ana gubu!!
 
Babu walioko kwenye abusive relationships wanawezakutoa ushuhuda juu ya hili. Haki zao za ndoa zinabakwa na wanajikuta wanalazimika kuendelea kuzaa kwa kuwa tu ni wajibu wao kama mke.

MJ1 pleeeease,

Hapa tunaongelea normal relationships na siyo hizo extremes....Hatuwezi kusema Watanzania wote ni wezi eti kwa sababu baadhi yetu tunaiba!

Hizo unazoongelea ni abnormal na kwa hiyo hapo hakuna mahaba....ama kuna biashara (win-win situation) au ukandamizaji kwa mhusika! Huo mjadala tuufanye siku ingine.

Leo tunaongelea mahaba kati ya watu ambao kila mmoja yuko happy na uhusiano unaoendelea. Swali ni kwamba anapata maximum gains katika mambo ya mahaba ?? Tuzame hapo kwanza.....!!
 

Hivi hata mimi na mzee mwenzangu tunategemewa kufanya hayo??? Na kama tukipiga story za vitega uchumi tunavyoandaa kabla ya kustaafu na kumalizia kwa kukumbushana enzi za ujana wetu hayo hayakubaliki??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…