umeona eh?
Yaani hawa wadada wanaelewa wazungu lakini sisi hawatuelewi....
Kama mahaba inamfanya mwenzio ajisikie special na tofauti......
Na kitendo cha kuja na kuku wanalia lia mtaa mzima ukiona kimewezesha hilo la kujiona special na tofauti...
Bado wanaita sio mahaba...funny ehh?
mimi boss tulishakubaliana kuwa kama si wajibu wako basi ni mahaba, kama ni wajibu inakuwa tabu kidogo kujua tofauti ya hivyo viwili.
Kama mkeo labda kwake ni luxury kupika kwa mkaa, basi nadhani gunia la mkaa linahusu sana tu. Pia kula kuku kama si wajibu wako, mmezowea kula dagaa, siku ukipeleka kuku inaweza kuwa ni something extra so ikakubalika.
romance=love, the feeling of being in love, a feeling of excitement and adventure especially connected to a paricular place or activity, an exciting, usually short, r'ship btn two people who are in love with each other (kwa mujibu wa kamusi ya oxford)
sasa hapo utaona nani ataangukia wapi....
mahaba mi sijui kama limetokana na neno romance.....na hata hilo nalo ningeomba nisaidiwe mtu awezaje kuonyesha mahaba kwa mzazi au mtu mwingine mbali na mpenzi (au mahaba=mapenzi=upendo?)
umenasa mtego nilioutaka unase......lol
kwa maana hiyo sio sahihi watu kusema watanzania tuko nyuma kwa mahaba...
Kumbe pengine ni uwezo,hasa kama mahaba yanayo maanishwa hapa ni pamoja na diamond rings..sawa?
very funny aisee.....
Sijui hata wewe kwa nini tu hutaki kutuelewa. Ukitimiza wajibu kama baba tutashukuru (you are a responsible hubby)
but when you go an extra mile to make your partner feel as if she is in heaven (haijalishi hiyo maili ya ziada ni ipi tofauti na majukumu ya mume) hapo ndo unapokuwa romantiki sasa. Nifate mtoni unisaidie kibuyu cha maji, nitanie tanie kwa manjonjo, niite majina yatakayonifnya nijiskie mi ndo malkia wa himaya yako.....aaah acha uguruguru bosi bana! Nini huelewei hapa?
...hhhaaahhhaahhaa! unaanza sasa.... 🙂
....in general term yes, lakini ukiingia deep mpaka ukagundua nini lililomgusa mwandani wako
mpaka atamani tena muwe pamoja, ni zaidi ya wajibu, hisia, na sex... ----hapa kila mtu atakuja na tafsiri yake---
hata nikimuuliza soulmate ni kitu gani kilichonipa maksi zaidi muda wote tuliokuwa pamoja, jibu lake halitakuwa sawa na langu, ndio maana majuzi nilimwambia na nina nukuu kama anakumbuka;
...mwisho wa kunukuu...
Ikiwa kila siku tunatumia mkaa ....ukileta gunia la mkaa hakuna mahaba hapo.
Ikiwa kula kuku ni kawaida............ukileta kuku hakuna mahaba hapo
lakini ukienda kuyatafuta mapera huko na huko kwa vile nayapenda ........hapo full marks za mahaba ila hamfanyi.
Nyinyi mnataka vile vitu vya wajibu vitambuliwe kama mahaba! wapi na wapi mkuu .......lol
ikiwa kila siku tunatumia mkaa ....ukileta gunia la mkaa hakuna mahaba hapo.
Ikiwa kula kuku ni kawaida............ukileta kuku hakuna mahaba hapo
lakini ukienda kuyatafuta mapera huko na huko kwa vile nayapenda ........hapo full marks za mahaba ila hamfanyi.
Nyinyi mnataka vile vitu vya wajibu vitambuliwe kama mahaba! Wapi na wapi mkuu .......lol
mbona na mimi namaanisha hivyo hivyo?lol
bosi ni msumbufu tu anatuchora nshamshtukia tayari
Unajua mkuu Mbu najua ni kwanini wengi wetu tunayatoa masuala ya wajibu na sex kwenye hii category ya romance, ni kwavile tunaona kila mtu anayapata haya mambo whether awe kwenye mahaba au hata nje ya mahaba, lakini tunasahau kwamba watu wako level tofauti katika kuwajibika (wajibu) na sex, mwengine anaweza akaenda extra mile kwenye wajibu wake na ikawa part of romance, kama alivyosema gaijin, kama mnakula dagaa kila siku basi kitendo cha kupapatua kuku kwako kumpelekea mwandani wako kinaweza kikawa romantic act, na linapokuja suala la sex ndio kabisaaa, unaweza ukawa unapeleka mauwa kila siku na kadi za bethdei lakini sex perfomance ikawa mbovu na ukadharaulika romantically. Hivi vitu haviepukiki tunapoongelea romance lazima tuvikubali tu
NB: siviongelei hivi vitu katika normal level but katika extra special level.
halaf uskute kuku wenyewe mtu umeiba au umekopa ili at least gaijin wako aonje protein na yeye.
Dah! Inauma aisee
honestly siwachori....
Ninachopinga hapa ni kuwa tuko nyuma kwa mahaba..
Kumbe tuna mahaba yetu na nyinyi mnayaelewa vizuri....
sasa mapera tunawaletea..but umesema tuongeze bidii....hapo vipi?
Ulimaanisha bidii ipi labda?
Sasa Mwalimu wangu, kwa mfano wako hapo, leoa nimekulete mapera imekua ni "mahaba" in a sense that its not normal, sasa kesho na kesho kutwa nikikuletea mapera inabaki kua mahaba au ndo imeshaisha maana sio extra tena ni normal. si ndio?
Sasa Mwalimu wangu, kwa mfano wako hapo, leoa nimekulete mapera imekua ni "mahaba" in a sense that its not normal, sasa kesho na kesho kutwa nikikuletea mapera inabaki kua mahaba au ndo imeshaisha maana sio extra tena ni normal. si ndio?
Mimi narudia Boss ....its all about customization, we want them things tailored just for us. Something extra from the normal routine. Something which will make me go "aaaaawwww thats so sweeeet".
Sasa gunia la mkaa linanifanyaje nende "thats so sweet" wakati kila siku ndo nnalolitumia?
Mh hapa naona itakua wajibu sasa..! Ngoja nifikiria kwanza! haya Mahaba haya mbona yatuchosha?lolUkiyaleta kila siku mkuu utanichosha, yatakuwa si mahaba tena hayo ......lol
Wewe maximum lete once a week, tena isije kuwa same day of the week, maana itageuka routine