Ester Bulaya akamatwa na Polisi jijini Mwanza

Ester Bulaya akamatwa na Polisi jijini Mwanza

Kwa hiyo Mkuu , ukiambiwa ua na bosi wako Askari Wewe unaua tu?Ikigundulika ya Kuwa umefanya mauaji Nani anashtakiwa?Wewe au bosi wako?
Acha kujidhalilisha.Askari hawezi kuhoji amri ya Bosi wake.Jeshi sio kijiwe cha haki za binadamu na wanaharakati.Hata ukiambiwa lala kwenye moto unalala haraka baadae kama unahisi kuonewa ndio utaomba kwa unyenyekevu kueleweshwa.Kimsingi,kwenye uwanja wa mapambano, ukikataa amri ya mkuu wako anaweza kuamuru askari mwingine akuchape risasi.
 
Masikini Esther, kosa lake ni kumshinda katika uchaguzi waziri mwandamizi wa ccm!
Lakini tuwekane sawa, Esther kura yake ilikuwa moja tu kama ya mpinzani wake hivyo waliomuondoa huyo waziri ni wananchi. Na wananchi hawakumuondoa kinyume cha sheria bali kupitia sanduku la kura katika uchaguzi ulioitishwa kihalali na kufuata sheria zote za nchi.
Lakini pia, kama kweli huyo aliyeagiza kukamatwa kwake ni kweli basi tusisahau kuwa ni huyu huyu aliyempiga mpinzani wake hadharani mpaka akazimia!

Umenena vema
 
Kuna tofauti kubwa tu. ...labda kama hujui. ...
Usiongee vitu kwa nadharia pasipo ufahamu wa kina


Wewe ndiyo haufahamu kama ipo hiyo tofauti mbali na niliyoisema itaje hapa!
 
Kuna tofauti kubwa tu. ...labda kama hujui. ...
Usiongee vitu kwa nadharia pasipo ufahamu wa kina
Kwenye swala la kutii amri hakuna tofauti.Hakuna Jeshi linaloruhusu mdogo kutokutii amri.Labda kama unaongelea genge la wauza unga.
 
Just in>>>>>>

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya, tayari amesafirishwa kupelekwa Dar es Salaam kutokea Mwanza chini ya uangalizi wa Polisi kwa ndege ya Precision Air

Serikali imepoteza hela leo kisa kesi za kijinga
 
Haujui unachokiongea na wala hauelewi chochote kuhusu Jeshi linavyofanya kazi, kama Mkuu wa Jeshi akisema upigwe risasi wewe pamoja na familia yako na itakuwa hivyo Askari hawezi kupinga Amri ya mkubwa wake hata siku moja na kama akifanya hivyo basi hana kazi na hiyo ni sehemu ya mafunzo yao na ndio maana unaona Marekani Raisi anatuma Majeshi kupigana Vita Iraki ingawaje kila mtu anajua kwamba ni illegal war lkn siyo kazi ya Askari kuhoji uhalali wa anachotumwa bali ni kazi yake ni kutii na kutekeleza tu, hivyo kama askari wetu walipewa Amri kwenda kumkamata Mbunge Bulaya watafanya hivyo bila hata ya kupepesa macho kwani siyo kazi ya Askari kuhoji sababu ya kukumata wao ni kutii Amri TU na si vinginevyo!

Rais wa Marekani hana kauli ya mwisho ya kutuma majeshi yakapigane au kutoa amri polisi wakamate au kuua mtu. Mifano mizuri sana unayoweza kutumia kwenye hoja yako inapatikana zaidi hapa Afrika.
 
CCM jamani uchaguzi wa meya dar Hati ya zuio fake mhusika yuko huru Ester Bulaya anasakamwa eti Na bunge Chadema fuatilieni mpaka mwisho uonevu umezidi
 
Jambo hilo ni kweli. Wamemkamata. Hizi chokochoko sasa zimezidi, wanawashinikiza wapinzani wakasirike baada ya kuona safari hii wamekuwa na uvumilivu wa ajabu
Sasa hivi Polisi inafanya kazi kwa maagizo kutoka msoga na Lumumba. Usalama wa Taifa na Jeshi ndiyo vipo chini ya Magufuli
 
Kwa hiyo kwa akili yako unadhani kuwa kilichompa ushindi Sugu ni ile mihemko ya bungeni? Subiri 2020 jinsi wabunge wako watakavyosombwa na maji
Hii kamata kamata inafaa hao polis nao wafunguliwe kesi Kwa sababu wamekuwa wakifanya kazi ya Uonevu wanamwacha aliyegushi Hati ya Mahakama , wanawakamata wadai haki , mfano ww Sasa umeamua kusaka cheo cha mkuu wa mkoa Kwa sloppy ya kubenea .
 
Sasa hivi Polisi inafanya kazi kwa maagizo kutoka msoga na Lumumba. Usalama wa Taifa na Jeshi ndiyo vipo chini ya Magufuli
Kilichobaki ni mawakili wa chadema kuwafungulia kesi polis Kwa kushindwa kumkamata Yule aliyegushi hati ya Mahakama wamebakia kujipatia umaarufu kupitia wabunge wa chadema .
 
Ni mambo ya kishenzi na upuuzi mtupu wanafikiri watawakamata nakuwafungulia kesi maeneo mbali mbali ili wawapangie tarehe ya kufika mahakamani siku moja wote alafu wanaitisha uchaguzi wa meya wa dar iliwapate goli la mkono
Kilichobaki ni kuwafungulia kesi wale polis wote ambao wanatumika kuwanyanyasa wapinzani na kumwacha Yule aliyegushi hati ya Mahakama , hiyo kesi ifumguliwe Mahakama kuu angalau itawafanya polis wajitambue kuwa wanachokifanya ni Udikteta hakisaidii kwenye Utawala wa haki Bali husaidia Utawala wa kidikiteta tu.
 
View attachment 329145

Mbunge wa jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza na kulazimika kulala rumande baada ya kunyimwa dhamana.

Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha kumpeleka kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Justus Kamugisha amesema hati ya kukamatwa kwake imetoka ofisi ya Bunge na kwamba Mbunge huyo anashikiliwa kama mtuhumiwa ambaye anatakiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.

Wabunge hawa pamoja na uongozi wa juu wa CHADEMA Wako jijini Mwanza kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold Crest.
huu Udikteta utakwisha lini ? Wasake Uhuru Mahakama au ikibidi wapeleke malalamiko Mahakama ya kimataifa The Hague .
 
Unaishi nchi gani wewe? Unapingana na Mwenyekiti wa chama chako na Rais mstaafu aliyepata kusema Polisi waache kubambikia watu kesi? Jee hata huyu waziri wa mambo ya ndani wa sasa hivi aliposema Polisi wamekisiri kwa kutunga kesi na atawashughulikia hilo nalo hujasikia?
Au kwako wewe kuwa mpinzani tuu sio raia mwema?
Tiba pekee ni kuwafungulia kesi za unyanyasaji Mahakama kuu.
 
Kitu mbaya sana
tena kitu mbaya sana.Mshana huyu dada kipindi yuko viti maalum CCM best wake alikua mdee,nilikua napata maswali juu ya hili lakini alipohama chama majibu nikayapata,kweli kawasoma vilivyo sasa kazi kwao.
 
Tunaweza kudhani kuwa tunajenga nchi kwa kutumbua majipu na kusahau kuwa tunaibomoa kwa kutengeneza usugu!!!!!!
 
Kapora mume wa mtu nini? Maana Esther Bulaya anakuwaga na hizo skendo
NDIO Maana Mkichanwa Ukweli Mnaomba Watu Wapigwe Ban!! Lkn Kwa Maneno Ya Kijinga Hivi, Mtaomba Saana Watu Wanaochana Makavu Wapigwe Ban!!! HIVI Kama Kamanda Wa Polisi Amesema, Amepewa Oda Ya Kumkamata Mh. Bulaya Toka Dar Na Imetoka Ofisi Ya Bunge!! SASA Hoja Ya Mh. Kuchukua Mume Wa Mtu Inahusika Vp Na Ofisi Ya Bunge!!! Au Bunge Limekuwa Jeshi La Polisi Na Mahakama!!!!!!!??? Ambayo Inashughulika Na Masuala Ya Jinai!!! Alafu Kusema Eti "Maana Ndio Zake Kuchukua Waume Za Watu " Bila Evidence Yoyote Tutaamini Vp, Hata Kama Na Ww Umechukuliwa!! Weka Tu Wazi Ushaidi, Ili Tumchape!!!
 
Back
Top Bottom