Ester Bulaya akamatwa na Polisi jijini Mwanza

NAPITA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
5,077
2,245
1.jpg

Mbunge wa jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza na kulazimika kulala rumande baada ya kunyimwa dhamana.

Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha kumpeleka kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Justus Kamugisha amesema hati ya kukamatwa kwake imetoka ofisi ya Bunge na kwamba Mbunge huyo anashikiliwa kama mtuhumiwa ambaye anatakiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.

Wabunge hawa pamoja na uongozi wa juu wa CHADEMA Wako jijini Mwanza kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold Crest.
 
Ule muendelezo wa kukamata kamata wabunge wa Upinzani umeendelea usiku wa kuamkia jumamosi kuelekea kwenye kikao cha Kamati kuu na Badae Baraza kuu la chadema baada ya Polisi wa Mwanza kumkamata Mbunge Estar Bulaya wa jimbo la Bunda mjini akiwa hotelini kwa maagizo ya Speaker wa Bunge, Job Ndugai.
Kwa agizo la spika?? Kakosa nini hadi agizo litoke Kwa spika? Hii siielewi hebu wenye kujua watueleweshe. Hili la spika. Tena kukamatwa usiku wa manane
 
Ule muendelezo wa kukamata kamata wabunge wa Upinzani umeendelea usiku wa kuamkia jumamosi kuelekea kwenye kikao cha Kamati kuu na Badae Baraza kuu la chadema baada ya Polisi wa Mwanza kumkamata Mbunge Estar Bulaya wa jimbo la Bunda mjini akiwa hotelini kwa maagizo ya Speaker wa Bunge, Job Ndugai.
Kulikuwa na RB na arrest warranty?
 
Mambo ya kukamatana kamatana kijinga siku hizi yamepitwa na wakati. Watanzania wana taka maendeleo na Rais kaonyesha njia kiasi kwamba hakuna Mtanzania makini anapoteza muda wake kufuatilia ujinga wa kina Ndugai na bunge lake. Hivi Change bado yupo jamani?
 
Ule muendelezo wa kukamata kamata wabunge wa Upinzani umeendelea usiku wa kuamkia jumamosi kuelekea kwenye kikao cha Kamati kuu na Badae Baraza kuu la chadema baada ya Polisi wa Mwanza kumkamata Mbunge Estar Bulaya wa jimbo la Bunda mjini akiwa hotelini kwa maagizo ya Speaker wa Bunge, Job Ndugai.
Nina mashaka na Hii taarifa
 
Hizi ndoto za usiku wa manane huwa zinavuruga akili. Ukitoka kuota ndoto mida hiyo msipende kushika simu zenu au kuongea ongea.

•Usiku mwema wadau. Ngoja nirudi kulala
Jambo hilo ni kweli. Wamemkamata. Hizi chokochoko sasa zimezidi, wanawashinikiza wapinzani wakasirike baada ya kuona safari hii wamekuwa na uvumilivu wa ajabu
 
Wee acha tu kuna wanachokitafuta
Ajabu ni kuwa wabunge hao wakipata umaarufu na kupendwa na wananchi wanashangaa tena bila kujua wanavyowatendea wananchi wanaguswa.
Ona kile kitendo cha kumshambulia Sugu bungeni ili kumdhalilisha, na wakatumia zile picha kwenye kampeni kuwa ni Mbunge wa hovyo kilivyo wagharimu.
Sugu ndio Mbunge aliyepata kura nyingi kuliko mgombea ubunge yeyote Tanzania. Kwa maana amekubalika na tena bila hongo. Kumpiga chura teke sio kumkomoa katika safari yake.
 
Jambo hilo ni kweli. Wamemkamata. Hizi chokochoko sasa zimezidi, wanawashinikiza wapinzani wakasirike baada ya kuona safari hii wamekuwa na uvumilivu wa ajabu

Mbona huyo sio mpinzani? Kafata ubunge juzi Tu huko CCM zaidi kuliko huko upinzani
 
Ajabu ni kuwa wabunge hao wakipata umaarufu na kupendwa na wananchi wanashangaa tena bila kujua wanavyowatendea wananchi wanaguswa.
Ona kile kitendo cha kumshambulia Sugu bungeni ili kumdhalilisha, na wakatumia zile picha kwenye kampeni kuwa ni Mbunge wa hovyo kilivyo wagharimu.
Sugu ndio Mbunge aliyepata kura nyingi kuliko mgombea ubunge yeyote Tanzania. Kwa maana amekubalika na tena bila hongo. Kumpiga chura teke sio kumkomoa katika safari yake.
Kwa hiyo kwa akili yako unadhani kuwa kilichompa ushindi Sugu ni ile mihemko ya bungeni? Subiri 2020 jinsi wabunge wako watakavyosombwa na maji
 
Hakuna kitu magamba wanatoa chati kwa upinzani kama hayo mambo ya kukamata kamata viongozi wa vyama vya upinzani.
Hata sijui akili zao huwa zinawatuma nini?! Upuuzi huu unaonesha wazi kwa raia kuwa magamba wanatumia nguvu ya ziada kuzima wapinzani.
Lakini magamba yenyewe wala hata hayaelewi, kila siku yanakamatisha wapinzani na kuachiwa, na kutoa headlines kwa viongozi wa upinzani.
Sijui kwanini ukiwa CCM unakuwa kama una akili haba?

Ova
 
Back
Top Bottom